ACHA NIUITE USIKU KUWA GIZA
Ni jambo la kawaida tu
pindi inapokuwa usiku basi watu hupenda kusema habari za usiku au usiku mwema……
wakiwa wanaenda sawa na majira yaliyopo, hali kadhalika pindi inapokuwa mchana
watu usema mchana mwema au habari za mchana, imekuwa ni kitu kimoja kizuri sana
katika utamaduni wa kusalimiana hasa waafrika,japo salamu ya mchana imekuwa
ikitumika sana kuliko ya usiku kutokana na wingi wa watu unaokutana mchana
kuliko usiku!
Ni vizuri kuita usiku
kuwa ni usiku ili uweze kuishi kulingana na hali iliyopo hasa mwanga unakuwa
hafifu hivyo unahitaji kuwa makini katika mwenendo wako katika usiku huo na pia
katika mchana lazima ukubali kuwa huu ni mchana yanipasa nitembee katika hali
stahiki nikijua kuwa huu ni mchana kila mtu nirahisi kuniona kwahiyo lazima
nitembee katika hali iliyo sawa kulinganisha na wakati.
Na ndomana watu wengi
katika ulimwengu wa sasa hasa huu wa utandawazi wamekuwa wakitembea na kuvaa
mavazi yanayo ashiria huu ni usiku na mchana (tunahita maendeleo) na pindi
ukavaa mavazi ya usiku wakati wa mchana bila shaka unaweza kuibua maswali kwa
jamii inayokuzunguka, kwakua jamii inategemea kila vazi linawakati wake na
jamii ya sasa imekwenda mbali kidogo kusema pia kila hali ya hewa inamavazi
yake mathalani majira ya joto, masika,baridi n.k kila hali inapotokea ina aina
ya mavazi yake stahiki ambayo kama binadamu anapaswa kuvaa pasipo kuchanganya!
Na unaweza kushangaza
watu pindi utakapoanza kuita usiku kuwa ni mchana hata kama kunataa zenye uwezo
mkubwa ambao mwanga wake unafanana kuwa kama mchana lakini ukweli utabaki kuwa
huu ni usiku ila taa zilizopo zina mwanga mkali sana.
Acha
niuite usiku kuwa giza nini maana yake!
Nipende kusema kuwa
usipokubali hali uliyonayo ni ngumu tu kuvuka sehemu nyingine iliyo hatua bora
katika maisha yako!
Wako watu walikuwa
wanaumwa sana na wakati mwingine magonjwa ya aibu mtu anaona hawezi hata
kumwambia rafiki yake anabaki kutumia madawa katika duka la dawa kununua dawa
za kutuliza maumivu hawezi kwenda hospitali wala kutafuta suluhuu ya tatizo
linalo mkabili kwa kuogopa kuwa ataweza kuchekwa au heshima yake itapungua
katika familia au katika jamii inayomzunguka.
Wako wanawake na
wanaume wanajua kuwa hawana uwezo wa kuzaa kabisa kutokana na ushahidi wa
kimadaktari lakini pindi wanapokuwa wamepata wenzi wao wanakuwa sio wa wazi
katika kueleza hali zao za kiafya na matokeo yake wamekuwa wakileta shida
katika jamii zao na hata kupelekea ndoa zao kuwa na wakati mgumu sana tofauti
na hali sahihi inayotakiwa kuwepo katika ndoa.
Wako na wanafunzi wamekuwa
na matokeo mabaya katika hali ya mwanzo kabisa katika masomo yao lakini
wamekuwa sio wa kweli pindi wanapoulizwa na ndugu zao au walezi wao na kukuta
kusema tofauti na hali ilivyo na mwisho hali ikawa mbaya sana na hata kupelekea
kufeli katika masomo yake.
Wako watu wengine
wamekuwa wakisema Mungu pekee yake anajua na ndiye ataye jibu na kunipa haja ya
moyo wangu lakini wakati mwingi imekuwa ni vigumu tu kuwa Mungu kushuka kwako
kwa namna unavyofikiri anaweza akamtumia mtu naye akawa jibu katika swali lako
linalo kukabili.
Usipokubali na kutambua
kasoro zako ipo siku itakuweka katika mazingira magumu sana na hata kukupelekea
kujuta kwanini ukuwa wazi toka mapema na hatimae yakakufikisha mahali ulipo
sasa ambapo kiukweli ukupatarajia.
Pindi unapokubali tatizo
sio kwamba unataka likae na wewe milele bali njia sahihi katika kulitambua
marefu yake na mapana yake ili iwe rahisi kutoka pale ulipo kwakua utajua
chanzo chake na utafanya akili yako
ifanye kazi katika hali ya utulivu na kupata jibu sahihi na ikawa suluhu ya
kudumu!
Na hali ya kukubali
jambo kuwa limekukuta sio ishara ya kuonyesha Mungu ameshindwa kuliepusha
lisikupate hapana kunawakati mwingine Mungu anataka wewe uwe ushuhuda kwa
wengine waone jinsi ulivyoteseka na hatimae ukaibuka kuwa mshindi.
Imeandaliwa
na:
Cothey
Nelson…………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni