Alhamisi, 29 Agosti 2013

utukufu wa Mungu ni nini?



 UTUKUFU WA MUNGU;

Utukufu wa Mungu ni dhana pana sana ambayo yote inamuelezea Mungu na mambo yake vile anavyoonekana katika namna mbalimbali kama apendavyo yeye kujidhihirisha.
Utukufu wa Mungu sio kitu kidogo kama watu wanavyoelewa namna ulivyo huo ukuu wa Mungu ndivyo mambo yake yatavyo kuwa.

Kwa maana hiyo uwezi kusema na uwogopa utukufu wake lakini yeye mwenyewe si muogopi kwakua katika yeye tunaona utukufu wake na huo utukufu uwa unayafanya yaliyo yake hivyo uwezi kumtenga yeye na utukufu wake.

Heshima unayompa Mungu ndivyo heshima ya utukufu wake utakayo mpa hakuna mbadilishano wowote vile alivyo ndivyo utukufu wake ulivyo.
Mahali ambapo utukufu wa Mungu unatua lazima mahali hapo pafanane na vile utukufu unataka na hakuna ugumu unaweza kuushinda utukufu wa Mungu.


UTUKUFU ni namna mbalimbali ambavyo Mungu anajidhihirisha katika kuonyesha uweza wake,mamlaka katika kusudi lake.
Na pindi utukufu wa Mungu unaposhuka utukufu mwingine unakuwa hatarini maana hakuna utukufu ambao utazuia utendaji wa nguvu zake.
Utukufu wa Mungu umebeba uwakilishi wa Mungu hivyo lile ambalo limekusudiwa linafanyika pasipo shaka yoyote kwa namna yoyote anavyopanga yeye.
Na hakuna mtu atauzoelea utukufu wa Mungu alafu ukabaki salama ni ngumu sana kwakua Mungu mwenyewe hazoeleki.

Utukufu wa Mungu ni kitu kingine pindi kinapo tuama mahali kinaweza jambo ambalo hata macho yako hayata amini.
Mungu si vile ambavyo unamuona bali ni vile alivyo kwahiyo ukimuona tofauti alivyo kamwe uwezi kuyafanya yale unayotakiwa.
Utukufu wa Mungu unafaida sana ukaenda kwa namna yake unavyotaka lakina kama utaenda tofauti utaona mateso na dhihaka na mateso siku zote.
I wafalme 6:11-13
Kwakua utukufu utenda yale ambayo Mungu anataka uyafanye katika utoshelevu wake ukienda kinyume jua usalama wako unaweza kutoweka.

Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
It  my pleasure to say in his glory we are safe……………………!!!!!!!!!!