Ijumaa, 20 Desemba 2013

MAUSIANO YENYE TIJA







MAUSIANO;

Duniani hakuna kitu kizuri kama kuhusiana na watu vizuri ili uweze kufanikisha uhitaji wako wakati wa uwitaji na uwitaji wao. (saidia ili nikusaidie)

Kuna misemo mingi unayotilia mkazo kuhusiano vizuri katika jamii inayozunguka; 

-ishi na watu uvae viatu

-kidole kimoja akivunji chawa.

-umoja ni nguvu.

-heri wawili kuliko umoja.

Kuna wakati unaweza fika hauta ona maana ya maneno/misemo hii bali utaona bora uwe pekee yako na wakati mwingine hutaona uwitaji wa kuwa na uwitaji na mtu yeyote.

Ukweli furaha yote inayotokana na mausiano kati ya mtu na watu yanaleta furaha ya kimwili na wala haigusi roho ya mwanadamu.(japo unaweza kuhihusisha)

Vitu vya kuongelea katika mausiano;

i.nini maana ya mausiano?
                                          
                                         ii.vyanzo vya mausiano.

 iii.namna ya kujenga mausiano/kuimarisha mausiano.
                                         
                                       iv.namna ya kuyabomoa mausiano.
  
v.dalili za kubomoa mausiano.
                                         
                                     vi.dalili za kujenga mausiano.

 vii.faida za mausiano yaliyoimarika.
                                     
                                  viii.hasara ya mausiano yaliyo vunjika.
 Ix.namna ya kuwa salama katika kila haina ya mausiano

Luka 21:15-19



i.Nini maana ya mausiano?

Mausiano ni jumla ya mambo mbalimbali, unaishije na jamii unayoizunguka,inaielewaje jamii inayokuzunguka na unaipa nafasi gani katika maisha yako.

Kwa kifupi utaelezea maana ya mausiano ni hali ya mwingiliano baini ya mtu na mtu au mtu na kikundi cha watu.

Mtazamo wako ulivyo tofauti baini ya watu wa jamii moja au tofauti inaonyesha namna mnavyo uhusiana.

Kuna mambo uwezi kufanya kwa mtu huyu na mtu mwingine unaweza kufanya hiyo inaonyesha namna mnavyo husiana.

Kuna neno unaweza kuliongea kwa mtu unayempenda( mpenzi) wako lakini uwezi kuliongea kwa mtu mwingine.

Mtazamo wako wako juu ya wako juu ya watu unaoleta mausiano unajengwa uelewa wako na ulikotoka.(chimbuko gani umetokea).

Kila mahali ulipo pana haina ya mausiano mathalani kazini,shuleni,kanisani na jamii inayokuzunguka(majirani) pia kunamgawanyo ya mausiano kama mtoto na wazazi, wapenzi, rafiki. Na nimtu mmoja anaweza 

kujihusisha na hayo mausiano.
Mtu alivyo kwako ndivyo utakavyo uhusiano nae,akiwa mchungaji lazima utambue usiano ukoje?

ii.vyanzo vya mausiano

siku zote msingi mzuri upelekea mwendelezo mzuri.

Lazima ujue kwanini na uhusiana na mtu uliyenae na katika yapi mnahusiana ili uweze kuunda uhusiano mzuri na ukiweka mipaka kulingana na uhusiano wenu.

Mnawe mkausiana katika jambo mmoja na mengine usimmuhusishe kabisa ili kulinda msingi wa mausiano.
Sio kwa kuwa amekufurahisha basi ukamuhusisha na mambo mengine ambayo haitaji kuhusishwa.
Usipokuwa mwangalifu katika vyanzo vya mausiano unaweza ukapoteza hatima yako.

Suleimani na wake.

Ikonjia hionekayo….mithali 14:12
duniani kila jambo linamwanzo kupelekea mwisho.kila mausiano lazima uangalie chimbuko gani mmekutana ili kutambua ustawi wake.

Nini kilichofanya mkutane katika mazingira ya aina gani yana uhalali au yasiyo ya uhalali.

Kwakua kitu kilicho waunganisha ndicho kitawafanya mwendelee hivyo kinategemea kinamwendelezo mzuri wa kiroho au la!

Mahali au hali tofauti zinaweza kuleta kuanzisha mausiano;

-sehemu ya matukio(msibani,harusi,hospitali)

-mazingira yaliyo na maumivu(kusalitiwa,kutengwa,kuachwa)
Wakati huu utegemea na mtu kipindi hiki ufanya moyo uwa umetulia na akili isiyo na maamuzi mamoja.

-sehemu za elimu(shuleni kwa ujumla wake-msingi mpaka chuo,ufundi)

Tambua kukutana na mtu katika mazingira yoyote sio lazima chimbuko lake liwe mausiano.

Mazingira hatarishi(vijiwe  visivyo halali(bangi,umbeya,madawa ya kulevya), biashara ya kuuza miili(ngono).
Kila mausiano yanauvuvio wake hivyo lazima utambue huo uvuvio ili kudumu au kutengana.

Mausiano yana leo na kesho.hayana kila siku katika namna moja lazima utambue mfano.mtakapo usiana mnapokuwa watoto sio mtakapo usiana mkiwa watu wenye hatua nyingine kifamilia,kihuduma na shughuli za kimaisha.

Kitu ambacho kimewapa nafasi kuhusiana lazima kipewe nafasi ya utekelezaji wake hasa kikiwa ni chema. 

Discussion ya biblia ina hama  inaingia mapenzi hatimae mnaongezeka.

Yule ambaye mmehusiana kwa muda na pindi mkakutana nae baada ya kupotezana pindi mtakapo kutana zile hisia na akili inarudisha msingi wa mausiano. Na yale mliokwa mkifanya hii inaweza kuwa na hatari inategemea na akili yako. 


iii.Namna ya kujenga mausiano/kuimarisha mausiano

Mausiano yanapoanza uwasikuzote watu utafuta namna ya kuimarisha na kufanya yazidi kuwa mazuri au kuyaboresha siku hadi siku.

Ni kwelikunawakati ambao mausiano yanavunjika inawezekana kwa kila mtu kutosimama kwenye nafasi yake au kwa mpango wa Mungu. Lakini sio swala la kulizingatia au kulitia manani kama kipo uwakinakuja chenyewe.

Kuna mambo ya kuzingatia ili kuimarisha mausiano:

-jiweke wewe kwenye nafasi ya rafiki yako.

Lazima utambue thamani ya mwenzako kwa ukamilifu nauone kuwa furaha yake wewe una mchango wake.
Ona Mungu amekupa nafasi kuwa nae ili afanyike kuwa msaada kwako nawe uwe msaada kwake.

-tambua huduma iliyokuwa ndani ya mwenzako.

Ninyi ni wa Mungu lazima urafiki wenu ujumwihishe huduma zenu na utamani mkiinuana.
Mfano.Daudi na Jonathan

Msukumo wa urafiki wenu uwe ni yale mlio beba ndani sio ndugu au jamaa.

Lazima mjuane vizuri utendaji huduma zenu ili muweze kusaidiana vizuri.

Lazima hiyo huduma inakuwa katika utendaji wa Kimungu sio huduma ya kutimiza wajibu tu, ni huduma yenye mtembeo wa kimungu/inayo kua.

Lazima mjue mko wapi na mnataka kwenda wapi na mikakati ya kutimiza ndoto yenu.

-lazima mpeane nafasi ya kusikilizana.

Tamani kuona furaha/huzuni yake iwe yako kwa gharama yoyote ili mradi mnasonga mbele.

Hakikisha mnafurahiana katika kweli na sio kupakana mafuta tu.

-lazima mtambuane udhaifu wenu.

Udhaifu wenu muweze kukamilishana kwa upendo na kutakiana mambo mazuri.

Lazima uone kuhusika kwako kwa kila jambo linalo mhuhusu tena katika kiwango cha juu Sana.




Iv.Namna ya kuyabomoa mausiano.

Kuna mawili unaweza ukabomoa mausiano wakati unajua au wakati haujui, lakini yote hatima yake ni mausiano kuvunjika.

Kwa mtu uliye mpenda hautafurahia kipindi hiki(kipindi cha maumivu) ila katika mtu usiye mpenda ni wakati wa kuburudika/sherehe.

Hii hiko wazi namna mausiano yanaweza kubomoka haijalishi ulipenda au ulichukia.

Hiki ni kipindi ambacho kina gharama(lazima kunakujigharimu katika maisha yako) kwakua sio maamuzi ambayo yanajurudia siku baada siku.

Kama kuna wakati unahitajika uwe na maamuzi magumu ni katika kipindi hiki ambacho kitajenga historia mpya ya maisha yako.

Hii hatua kama usipoamua vizuri inaweza kugharimu katika maisha yako na doa likabaki ndani ya maisha yote yalio baki.

Kuvunja mausiana haina maana chuki kuchipuka,kumuombea mabaya au kufurahia mabaya yakimpata au kuchukia mazuri yanapomkuta.

Mausiano yanavunjika katika hali mbili yenyewe au walio katika mausiano.

Mtu anaondoka mahali pengine au nchi nyingine,kufa(mausiano yanavunjika yenyewe).

Kuumizana au kusalitiana,(mausiano kuvunjika kutokana na wahusika).

Kuna mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kuvunja:

a)Mmenufaishana katika hali njema.

Yapo mambo mabalimbali yalitukia yakatingisha uhusiano wenu, lakini angalia mchango wake maisha yako.
Sio alikupa hela wakati shida au kukuunganishia kazi(mtu yeyote anaweza kufanya utegemea na moyo wake) kitu ambacho kitaweka alama katika maisha yako.

Lazima kiwepo kama mtu unaye uhusiana kwa kweli na kwa moyo ulio safi wa hali endelevu.

b) Mnatambuana nafasi zenu mbele za Mungu.
Lazima pawepo na mwingiliano kati yenu ambao mnakutanishwa na kutokea kitu chenye nguvu.

c) Nyakati sahihi.
Ni kweli wakati huo sasa unaweza kusimama na ukaendeleza kile ambacho Mungu amekiweka ndani kwa mafanikio.

*Msikilize  Roho mtakatifu ili ajaze nafasi iliyo wazi ndani yako.
Huu ni msingi ambao unakulinda sio sheria kwamba lazima upitiehapo ili ufike hatima ya maamuzi yako.
Baada ya hapo maamuzi ya kuvunja ya chukie nafasi:

*MUONDOE KWENYE AKILI YAKO PASIPO HOFU.

Hakikisha amani imeingia ndani yako ili muone kama kiungo katika mwili wa kristo.


imeandaliwa;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com