ACHA JANA IPITE
Ni jambo halisi sana
kwa baadhi ya watu katika maamuzi yao ya leo yalitokana na jana yao…mathalani
siku moja nilimsikia polisi akisema kipindi sijawa polisi nikiwa mdogo nili
nyanyaswa sana na polisi hivyo niliapa kuwa endapo na mimi nikiwa mkubwa lazima
niwe polisi na hatimae akawa sawa na na lile kusudi alilowaza katika moyo wake
na sio huyo tu bia hata mtu katika kusoma udaktari au sheria kuna mambo walio
yapitia katika jana yao na kunuwia kusoma hiyo fani.
Japo ni kweli ni muhimu
usome jambo ambalo liko ndani yako ambalo unalolipenda pamoja na hayo pia kuna
ushawishi wa kimazingira ambayo yanaweza kusababisha kuingia katika fani hiyo,
pia tukubaliane wako watu wengi wanasoma sasa sio kwasababu wanapenda au hiko
moyoni ila inawezekana kutokana ndio nafasi iliyopatikana na hata wengine kuona
ndio yenye mshahara mkubwa na wengine uweza kuona kuwa ndio fani rahisi katika
kupata kazi na kuanza maisha yake binafsi.
Napia kunawakati unaweza
ukupenda kuingia sehemu fulani au fani fulani lakini baada ya kuanza kufaidi
matunda yake unaweza kusema hivi kwanini sikuwaza jambo hili kama kipaumbele
changu cha kwanza kwani sasa nafaidi matunda yake! Inaweza kuwa vizuri ukaanza
kuifurahia au kuwa vibaya hata ukaanza kuchukia wakati mwingine yote ni
kutokana na matokeo ya hiyo fani katika kazi unayoifanya.
Acha
jana ipite maana yake nini?
Ni kwali siku inaweza
ikapita lakini wewe bado unaishi katika jana yako japo unahiita leo kutokana
kuzama na kuchomoza kwa jua lakini ukweli wewe binafsi bado unaishi jana japo
unaonekana leo, yale yote yalioendelea jana katika maisha yako yamekuwa ndio
dira ya maisha yako ya sasa kama katika hali ya maumuvu ndio yamekuwa ndo
maisha yako ya kujikataa na kuona ndio maisha Mungu alinichagulia ya mimi
kuishi.
Mtu kama huyu anayeishi
jana katika leo mtizamo wake haubadiliki kile alichojiaminisha ndicho
kinachoendelea hadi leo na anakipenda kwakua amekipa nafasi katika maisha yake
na kuwa hivyo ndivyo maisha yake.
Kuna watu wakikumbaka
jana basi wanalia tu siku nzima inaweza kuwa ilikuwa nzuri kuliko leo mathalani
mtu katika maisha yake ya awali alikuwa na kazi yake nzuri na kuishi maisha ya
kifahari sana lakini kutokana kuachishwa kazi na ndipo maisha yako yakawa chini
hata usijue lakufanya tena bali kilio chako kikawa ndio maisha yake.
Ni vizuri sana kuanza
upya hata ukiona itachukua muda gani katika kutimiza malengo yako! Wako wengi
wanajihukumu na kujilaumu sana kutokana na yale yaliyosababisha kuwa hapo tena,
Iruhusu
jana ipite ili leo ije!
Hizi ni siku mbili
tofauti na kamwe hauwezi ukazifananisha na kamwe haziwezi kuingiliana kama leo
ipo basi jana ilishapita na kama jana ipo basi leo bado haijaja ziko hivyo
hakuna mbadala wake tena hiko kama ilivyo, ndomana wako watu wengi wanatembea
leo lakini ukweli hawaoni fahari ya leo zaidi yakujisikia vibaya kwa jana
iliyopita.
Usipokuwa makini
unaweza ukakuta unamlaumu Mungu muda wa wote kumbe wewe unaishi jana katika
leo…………ukapoteza muda na hata kukata tama!
Ni vizuri kutatambua
jambo likisha pita limepita hata kama ulikuwa hauamini lakini sasa inabidi
uamini tu haijarishi ulikuwa unampenda kiasi gani? Ulikuwa unamwihitaji kiasi
gani? Au alikuwa wa muhimu kiasi gani? Au kazi ilikuwa inakunufaisha kiasi
gani? Au nyumba ilikuwa inakusitiri na kujivunia kiasi gani? Lakini jua limeshapita kinachotakiwa hapo ni
maisha yaendelee kwakua kwakua kesho itakuja na pindi itakapo fika hautaita
kesho bali utaita leo.
Na kila siku kuna baraka
zake na hili uzipate unahita uishi kama siku hiyo ilivyo kama ni jana basi ishi kama jana na kama ni leo ishi
kwa siku hiyo ukifuta yaliyopita yaani jana yako, na sio kwa upande wa ubaya tu
watu wengine wanajisahau kwakua waliweza jana kufanya jambo fulani basi
wanaamini pia hata kesho wataweza pasipo kujua kesho na jana ni vitu tofauti na
kamwe haviwezi kulingana, maandalizi ya jana yanaishia jana na maandalizi ya
leo yanaishia leo.
lazima uwe mwepesi
katika kusoma mabadiliko ili uweze kuimarika na kuwa hodari.
Imeandaliwa
na;
Cothey
Nelson……………………………………………0764 018535