SUBIRA ISIYO NA KIKOMO!
Ni vizuri kuwa na moyo wa subira lakini sio kila kitu cha
kusibiria mathalani uwezi ukajenga moyo wa subira kuwa labda kuna wakati maji
ya bahari yatakuwa hayana chumvi!
Uwa sio ajabu kuona mtu anakwambia hapa nimekaa muda wote kuna
kitu nasubiri! Au mwingine akasema nasubiri aseme tu mimi nimalize! Na mwingine
atasema na subiri ajikwae tu mimi nichukue mzigo! Na mwingine akasema nasubiri
ajipendekeze tu ni mpe yake! Na mwingine atasema nasubiri ajikoroge tu alafu ni
mnyweshe! Hatari.
Japo tunajua kuwa SUBIRA kama hali ya kungojelea kitu, ila
inakuwa na maana sana kama hicho kitu kinachongojelewa kina sifa ya
kungojelewa/ kungojewa………usiwe ukawa unaenda mbugani kutaka kumuona simba akila
manyasi kwa hiyo ukapoteza muda, fedha ili kwenda kuona tu ipi siku nitamuona
akila majani au ukawa unasubiria kwa hamu kubwa kuona bundamilia mwenye mistari
siku mistari hiyo itakapofutika kwahiyo ukawa unakesha na kumuomba Mungu
ukitarajia kuwa hipo siku utaona mistari ya pundamilia ikifutika kwa hiyo
ukajikita katika kusubiri ukatazamia yasiyo tazamika.
Ni kweli sikatai kuwa kweli subira ya vuta heri lakini ni
jambo muhimu kujua kitu unachokisubiria kweli kina sifa ya kusubiriwa au
kinasifa ya kupotezewa ni muhimu utambue sio kila kitu ambacho watu wanasubiri
basi nawe unabidi usubiri mathalani mtu, ndugu yake akiwa amesafiri inawezekana
yuko nchi nyingine hivyo anaenda kituo cha basi au cha ndege kwa ajili ya
kumpokea ndugu yake basi nawe ukaenda kituoni kwenda kumpokea kitu
kisichokuwepo kwa hiyo ukakaa pale kituoni watu wana wapokea ndugu zao lakini
wewe upo tu mpaka mwisho unafika bado upo tu.
Ni vizuri kutambua
kuwa subira ni kitu kizuri ila unasubiri nini ni jambo la msingi ilikujua huu
ni wakati wake wa mimi kusubiri hichi kitu au nianze shughuli nyingine nachojua
mimi hakuna kitu kinacho umiza sana kama kitu unachosubiria kikawa tofauti na
vile ulivyo tarajia mathalani mama mjamzito anapokuwa ana hamu ya kumpokea mtoto
wake lakini yale matarajio yake yakawa sivyo hivyo akaingia katika ulimwengu wa
maumivu makali baada ya kukosa furaha yake, pia katika ulimwengu wa mapenzi
unaweza ukasubiri mtu wangu ipo siku tutafunga ndoa lakini ghafla amebadilika
atakikusikia tena habari za ndoa hata ukaendelea kusubiria labda kuna siku
ataamka vizuri lakini wapi hatimae ukashuhudia bahari na nchi kavu vikiachana.
Wako watu wanasubiri hadi wanapata magonjwa katika miili yao (
pressure,stroke etc.) na wengine hata kuwa vichaa kwa kutegemea ipo siku
atabadilika au mazingira yatabadilika na bado yamekuwa magumu tu tofauti na
ulivyokusudia na wengine atakufikia
hatua ya kujiua kwa kuona subira yangu haina maaana kwani ninachosubiria sicho
kinachotakiwa kusubiriwa.
Kwa kweli watu wamekuwa na hali ya kusubiri kwa vitu vingi
pasipo kujua na hivyo vitu kweli vinawasubiri wao , kwani unaweza ukasubiri
embe mpaka lina oza bado wewe unasubiri tu kuwa ipo siku embe lile nitakula tu!
Niseme pole sana kwa wale walikuwa wakisubiri vitu vingi
pasipo kutokea au vikawa tofauti na matarajio yao, huna haja ya kuchukua maamuzi
yatakayo dhuru nafsi yako au kujenga kisirani maadam unaishi jua kila kitu
kitakuwa sawa maadam Mungu ( muumbaji wako yuko nawe).
Mambo ya kuzingatia:
l. Jifunze kitu kutokana na hali iliyokutokea
ll.tembea katika njia sahihi
lll.weka imani thabiti kwa Mungu
Tambua sote ni kazi ya mikono yake! Anatupenda atakama tukiwa
wachafu kiasi gani aliye ruhusu utoke duniani analo jambo jema na maisha yako.
Ni kweli watu wanaweza kukukatia tama lakini kamwe si Mungu! Ifurahie siku
yako. Asante!
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson…………………………………………………..0764 018535