Jumanne, 7 Machi 2017

IBADA YANGU KWAKE NDIO FURAHA YANGU!



MOYO WANGU UMWABUDU MUNGU!


Yohana 4:22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.

                 23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.

                24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Kuabudu kwa neno jepesi unaweza kuita/kusema ni ibada hama namna unavyoishi katika kuinua na kumtukuza/kutukuza miungu hama Mungu unayemwamini,

Kama unataka kuimarika na kuwa mshindi na hatimaye kuifikia hatima yako basi penda sana kujua namna ya kumwabudu Mungu katika viwango vyake yaani namna anavyotaka,

Kati ya kitu ambacho Mungu akipendi ni kuona watu wake wakiabudu miungu mengine na ukisoma biblia vizuri utaona Mungu tendo la kuabudu miungu mingine ameliita kuwa UZINZI/UASHERATI
Ezekieli 23:35 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa umenisahau, na kunitupa nyuma yako, basi kwa hiyo, uchukue uasherati wako na uzinzi wako.( ukipata muda soma sura 23 yote uone picha kamili kwanini Mungu apendi ibada yake ichanganywe na vitu vingine).

Majibu mengi ya maswali yanapatikana pale unapoamua kumwabudu Mungu naam burudiko la moyo wako linalobariki moyo wa Mungu linazaliwa hapo, maana burudiko linalokuja baada ya kupata hela au kuambiwa asante hama nakupenda linakuwa sawa na mtu anayejiachia akitegemea kimvuli kitamdaka,

Lakini jambo jema sana hakuna ufundi wa kumwabudu Mungu kwakua namna yetu sio namna ya Mungu, yeye anajua namna ya kuabudiwa kupitia Roho yake atatuchukua na kutupeleka kufanya ibada ile tunayopaswa la msingi wewe uweke tayari mwili na akili yeye adhirishe uweza wake kwakua wewe  wake na anaweza kuutumia mwili wako kama anavyotaka akiamua kuugalagalaza chini, kukurusha juu hama kuupiga magoti awe na uhuru kwako,

Na mara zote ibada inafanyika pale tu moyo wako utakapofunguka na kujenga imani ya kile unachokiamini kuwa ni kweli na kitakusaidia na huku ukiwa na imani kuwa ibada yako inafika sehemu husika,

Katika ibada hama kuabudu haiwezi kufanyika bila MOYO KUFUNGUKA  kwa maana hapo ndipo kunaruhusu ibada ipite kwenye damu, mifupa na nyama yaani pindi moyo wako unapokuwa umefunguka basi hapo mwili wako unakuwa sio mali yako tena yeye Mungu anaweza fanya chochote katika mwili nawe unaweza ukawa unajua hama ujue lakini kwasababu unakuwa moyo umefunguka kwake basi wewe unakuwa radhi tena katika hali ya kupenda zaidi sana kuridhika,

Na katika kufanya ibada hama kuabudu ambayo yeye vile anavyotaka inakuwa ni rahisi yeye kujua wewe ni wake nay eye atawajibika juu yako kwakua anajua furaha yako ni furaha yake na hata huzuni yako inakuwa yake kwakua kwake umesha mpa kila kitu na hakuna kificho kwake kwa  lugha rahisi wewe kwake hauna kauli hama pingamizi kwa lile analotaka maana wewe ni mali yako,

Kumbuka kuwa Mungu ni mungu mwenye wivu anajua kila kitu kinachoendelea mwilini mwako na hata katika mawazo yako na atajisikia vibaya kuona mali zake zinatumiwa na vitu/ watu wengine na wala sio yeye.( uwa apendi kuona penzi lake linachanganywa na kitu chochote).

Kuabudu ni hali ya akili kupotea kabisa, mawazo yaliyo jaa mapenzi kwake na mwili ulitayari kuyafanya yale tu atakayo na wala sio kitu kingine…………. usijali kama ujafika hatua hii ila jitahidi ufike hapo kwakua kumfurahisha zaidi ndipo hapo unaweza kumshawishi na yeye ahusike zaidi kwako,

Ni vizuri niseme kuabudu sio kunyoosha mikono hama kutoa machozi wala kugalagala bali ni kile kinachoendelea ndani yako kinacho mpa utukufu Mungu, japo kuwa hayo yanaweza kuwa ni ishara ya upendo wako kwa Mungu, sawasawa na mtu kukuchekea sio kukupenda japo inaweza kuwa ni ishara hama uongo.

Kuna mambo mengi yanafanyika pindi moyo wako unapoamua kumwabudu Mungu tu! Yako matengenezo, uimarisho na kuwa namna ya ajabu sana, na kung’aa sana katika maisha yako
Kuna vifungo vinakuachia, maswali yanapata majibu na moyo unahimarishwa na nguvu zake.

IBADA YANGU KWAKE NDIO FURAHA YANGU!

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………..0764 0185353