Utulivu kama ungekuwa ni bidhaa basi kila mtu angependa kuwa nayo!
kwa namna yoyote utulivu umekuwa ni kitu adimu katika ulimwengu tulio nao, na hivyo imepelekea kutafutwa sana na watu wengi……………! Na kwa kawaida bidhaa adimu inapelekea gharama kuwa juu.
Maana katika dunia ya sasa wazazi/ walezi hama ndugu wana penda wawaozeshe/ kuwaoza watoto wao na watu ( wenzi) waliotulia, hivyo kutulia imekuwa sifa ikiangaliwa kwa namna ya pekee kutokana umuhimu wake wanao ufikiria, wengi wana amini kuwa wakimpata mtu mwenye utulivu ( aliyetulia) itapelekea kuwa na ndoa nzuri yenye maelewano na hatimaye kupelekea mafanikio katika maisha yao, mbali na swala la ndoa hata inapotokea unapokuwa na rafiki aliyetulia bila shaka watu wenye akili njema watakupongeza na kukushauri usimwache.
Japo kwa asilimia kubwa imetafsiriwa kuwa utulivu wa mtu ni ishara ya ubora wake, basi ni muhimu kutambua utulivu wa kweli na wa muda (feki).
Na hapo ndipo swali linakuja nini maana ya utulivu? Namjuaje kuwa huyu ni mtulivu? Bila shaka majibu unayo kutokana na mtazamo wako maana binadamu anayo fulsa ya kuwaza!
Japo wengine wanaweza kutafsiri neno utulivu katika hali inayompelekea hama kuonekana kuwa mzito katika kuongea na kutenda nadhani kwa wengi wazo hili linaweza kuja kwa haraka pindi unaposikia kuwa mtu huyu/yule ni MTULIVU, Na kwa watu wengi mtu mwenye sifa hizi ( mzito katika kusema na kutenda) awapendelei sana kwa kuwa wanaona anaboa.
Bali mtulivu kwa maana ya mtu anayeweza kutumia akili kiufasaha na katika hali ya wepesi na kusababisha matokeo makubwa na mazuri ni hali iliyo kivutio na inayopendwa na watu wengi kama sio wote.
Utulivu katika hali ya kimahusiana maana inayokuja hapo kwa wepesi ni mtu asiye mcharuko anaye maanisha anachosema anayemuheshimu na kumpenda mtu mmoja maalum mwenye nafasi maalum katika maisha yake na hali hii kila mtu uvutiwa nayo sio mkristo au mwisilam hama asiye na dini na pengine hata mcharuko mwenyewe apendi apate mcharuko mwenzake.
Ø NI KWELI MTU ALIYE TULIA NDIYE BORA?
Ni muhimu kujua nini maana ya neno bora! Na ni kweli kila kilichotulia kina ubora ndani yake? Na huo ubora ndio unao uhitaji? Asante kwa majibu mazuri yanayoendelea katika kichwa chako sasa tunaweza kuendelea…………………….!
Japokuwa wakati mwingine utulivu unakosa maana pale tu kama hakuna kinacho kuvutia ( ubora) mathalani mtu anaweza kutulia kwa muda mrefu katika ndoa hama urafiki lakini ukosefu/uhaba wa fedha hali hiyo kwa watu wengi uwa inakosa maana kwakuwa hakuna kitu ( ubora) unaofanya afurahie utulivu wake.
Lakini unaweza kukuta mtu anazo hela za kutosha lakini pindi ukiwa naye ujisikii utulivu japo kuna ubora ( fedha) unaweza kushangaa mtu anajitahidi kuwa hapo hata kwa gharama yoyote.
Unakuwa wa maana sana kama kwako utulivu na fedha vinapatikana basi hapo unaweza kuwa lulu kwa watu wengi; wamama, wababu, vijana na hata kwa watoto ( unakuwa kipenzi cha wengi kwasababu…..)
Utulivu ni kama nyumbani kwenu, unaweza ukapakimbia kwasababu uoni umuhimu wake wakati fulani lakini pindi yatakapo kufika utatamani tu urudi nyumbani ( nyumbani ni nyumbani).
Nakubaliana kuwa utulivu ni bidhaa adimu sana na watu walioambatanisha : UTULIVU+ NIDHAM+ UAMINIFU + BIDII= walifika mbali sana.
Utulivu usijifanye/usiwe nao kwasababu haujui bali yawe ni maisha yako yenye kukupa mwanga na hatua bora zaidi.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………….0764 018535