Ijumaa, 8 Juni 2018

MWAKA NI MREFU HAUNA HAJA YA KUWA NA HARAKA;



Kwa tafsiri ya haraka haraka tunapozungumzia MWAKA tuna kuwa na maana ya jumla ya miezi kumi na mbili ( 12 ) hama siku mia tatu sitini na tano sawa na mzunguko wake katika jua.

Tafsiri ya mwaka kuwa mrefu au mfupi, mbali na asili yake, pia utegemea aina ya mtu husika kwani yako mambo kwa mtu ili yatimie yanahitaji muda zaidi/muda mrefu lakini jambo hilohilo kwa mtu mwingine anaweza kutumia muda mchache sana na jambo kutatuliwa/kupata ufumbuzi wa muda au wa kudumu.

Yako mambo mengine katika maisha ya mwanadamu anavyoishi kutokana fikra au akili za mtu husika uweza kuona yanahitaji haraka sana na bila hayo uweza kusababisha nafsi yake kuwa dhohofu ( uweza kuhisi kama akiyakosa uweza kuwa katika mazingira magumu sana ).

Japo wakati mwingi haipo hivyo tunavyofikiria ingawa “ mashaka yetu ndiyo utumwa wetu”.

Natukirejea kwenye kauli hii “ Mwaka ni mrefu” haina maana kuwa utulie tu maadam siku zinaenda nab ado unapumua, ni vyema kutambua yako mambo kimsingi yanahitaji uwe na umakini katika kuyaendea na sio yote yakupe kufanya kipaumbele wakati hayana haraka katika utekelezaji katika maisha yako.

Imekuwa ni kosa la watu wengi kwa kuona kile kinachovutia basi kina kinahitajika mapema/ haraka na kile ambacho akivutii basi kisubiri subiri kwanza pasipo kutambua uhitaji wa kitu hautegemei muonekano bali utegemea uhitaji wa msingi uliopo.

Ni muhimu kujiamini na kuamini unachofanya hasa kikiwa kimebeba kusudi jema na katika haki.

Huna haja ya kuitahabisha sana nafsi yako kama kifaranga aliyekosa mama kwa kuhofia usalama wake dhidi ya maadui wake maana kuna watu wakipatwa/ wakiwa na uhitaji wa kitu basi mkoa mzima utajua na kuhitaji sana apate msaada kana kwamba mtu aliyekatika maji anatapatapa ili kupata msaada.

Amini na tambua kwa uhalisia kila jambo kwa wakati wake linakuwa na radha nzuri ya kudumu, usiyachungulie maji ukatoa maamuzi ( usiyapime maji kwa macho ) kwa muonekano wa macho maji unaweza sema ni masafi pasipo kujua macho hayawezi kujua hayo maji yamechanganyika na nini? ( contain) ambayo inaweza sababisha majanga katika afya yako.

Ni kweli siku na miaka inaenda lakini sio sawa na maisha yanavyoenda unaweza fikiri hili jambo linahitajika leo kumbe maisha yajayo hilohilo jambo linaweza kuwa la maana zaidi na likafanyika katika utukufu wake.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………….0764 018535