Tunapozungumzia wakati atuko mbali na majira, na uzuri kuwa majira yapo sio kwasababu tunapenda yawepo bali ni kwa sababu ya dunia kujizungusha katika muhimiri wake basi hapo majira hayana budi kuendelea kuchukua nafasi yake.
Na kawaida muda unapofika tu basi viashiria ni muhimu vionekane mathalani hauwezi sema hivi sasa mbili usiku na ukitazama jua linaonekana kama jua la sita mchana utaibua maswali mengi kichwani mwa watu.
Pia kila wakati kuna matazamio yake mathalani yai linapoatamiwa na kuku kuna wakati unafika linavunjika kama sio viza, hauhitaji kutumia kijiko ili kulilazimisha lipasuke ili kifaranga kitoke kama sio viza liache lenyewe maana ile asili yake inafanya hayo yote.
Unaweza kuwa mbabe wa vitu vingi lakini sio wakati mathalani unapopata neema ya kuishi miaka 90 ( tisini) uwezi tena kuishi kama mtu mwenye miaka ishirini (20) hata kama hatua/rika hii ulipenda kiasi gani!
Wakati unapofika tu kuna mambo lazima yatokee upende au usipende! Umejianda au ujajianda! Wenyewe wakati ukifika utafanya mambo yake sawa na unavyopaswa pasipo kuangalia huyu ni nani au anasifa gani?
Ni muhimu uazibiwe na mtu kuliko uazibiwe na wakati kwani utakuwa unapata adhabu pasipo kujua itaisha lini? Na wakati mwingine kukosa jibu nifanye nini ili nipunguze hii adhabu hama hiishe kabisa.
Naam majira yako ya ustawi yakifika haijarishi nini kilichokuwa kizuizi au tishio kwako bali yote yanafanyika tu pasipo shaka kwa majira yatatoa hali stahiki yakukuimarisha unayoiendea.
Usipende sana kutembea katika upepo bali tamani sana utembee katika majira yako kwani katika majira sio rahisi kupotea bali upepo uweza kubadili mwelekeo wakati wowote.
Na ushindani mwingi unatokea pindi mtu asipojua majira kwa kila tendo au jambo kwani kuna majira ya kusema na yakusikiliza, majira ya kufanya na kuacha! Na muhimu utakapo tambua majira na kutembea humo ni ngumu tu kujiwekea au kuwekewa kikwazo kwa kuwa wewe utakuwa makini na majira tofauti kabisa na kile kinachoonekana lakini si sawa na mtu anaye tembea nje ya majira yake mpaka mtu aje atambue uweza kujikuta yuko chini.
Kutembea katika majira ni rahisi pia ni ngumu katika mwili, tunasema ni rahisi kwakuwa Roho Mtakatifu uweza kukutambulisha kuwa wakati huu nini ufanye na ugumu wake katika mwili kwa kuwa mwili wakati mwingine unakuwa katika uhitaji wa haraka hivyo hali ya kusubiri katika yanaweza kuwa ni mateso katika mwili ndomana biblia imesema kuna kujikana.
Ushindi hauna kizuizi kwako kama wewe ni mtu unaye tembea katika majira yake ila furaha kubwa ni UNYENYEKEVU katika ushindi wako na sio kuanza kukomoa watu.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………0764 018535