Ijumaa, 30 Agosti 2019

MBINGU INAJIWEZA!




ACHA UTENDAJI WA MBINGU UFANYE YAKE

Kuna mambo yanapotokea hisia, akili na mwili wote unahisi umesimama na haujui unatokaje!
Unaweza kukuta unaamini upotofu zaidi kuliko usalama maana uhakika wa njia sahihi hauna/ hauioni!

Na wakati mwingine hata mwenyehaki anapojikuta yuko hatiani uweza kufanya jambo lolote ili mradi maisha yake yawe salama pasipo kuzingatia usawa wa jambo husika.

Karibu sana!

Abramu alipokuwa na sarai  alipotaka kupita nchi ya ugenini alimwambia sarai mkewe aseme kuwa ni ndugu yake na sio mke wake…………!

Mwanzo 12:10 Basi kulikuwa njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa nzito katika nchi.
                      11 Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso;
                      12 basi itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na wewe watakuacha hai.
                      13 Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako.

Isaka alipokuwa akitembea , akamwambia Rebecca aseme kuwa ni ndugu yake na wala si mke wake!
Mwanzo 26:6 Isaka akakaa katika Gerari.
                     7 Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso.
                    8 Ikawa alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, akachungulia dirishani, akamwona Isaka anacheza-cheza na Rebeka mkewe.
                   9 Abimeleki akamwita Isaka, akasema, Yakini huyu ni mkeo, mbona ulisema, Ni ndugu yangu huyu? Isaka akamwambia, Kwa sababu nalisema, Nisife kwa ajili yake.
                  10 Abimeleki akasema, Ni nini hii uliyotutendea? Labda mtu mmojawapo angalilala na mkeo bila kufikiri, nawe ungalitutia hatiani.
                  11 Basi Abimeleki akawaamuru watu wote, akisema, Amgusaye mtu huyu au mkewe lazima atauawa.
Wote ( Abraham & Isaka) walikuwa wanaogopa kufa kwakuwa wake zao walikuwa wazuri sura na muonekano!

Kuna mambo yanatokea na kupata ufumbuzi kwasababu ni asili ya dunia ilivyoumbwa kwa namna yake na Mungu sawa na mapenzi yake mathalani mtu aliyeonewa kwa muda mwingi na kunyanyaswa na mwisho akapata haki yake hata bila ya kutoa rushwa mwisho atasema “ MUNGU MKUBWA”!

Hakuna kitu bora au kizuri sana kama mahali ambapo mbingu imeamua kusema ni wazi ardhi lazima itikie maana sauti ya mbingu ardhi uielewa vizuri sana.

Ni muhimu kutambua ili mbingu iweze kukutetea lazima wewe uwe ndani ya mbingu ili yenyewe ijidhihirishe.

Kuna wakati unaweza kuona ni nafasi ya akili ya kutumika maana umemngoja Bwana kwa muda mrefu bila mafanikio/majibu na hali inazidi kuwa mbaya!

Mambo yanatokeaga na yakaathiri furaha ya maisha yako na hasa ukajua haukuhusika kabisa katika kosa hilo, mtu wa namna hii anakuwa na msongo wa mawazo “ stress” akiangalia kile kinachomkabili na uhalisia uliopo lakini ujue inawezekana katika mwili hauja husika lakini katika ulimwengu wa roho una husika ili uweze kutoka hatua moja na kwenda hatua nyingine na hatimaye kung’aa zaidi.

Kuna urahisi mkubwa pindi mambo yako pale mbingu itakavyoanza kuhusika na jambo linalokuhusu wewe.

Kitu pekee kinachoweza ruhusu mbingu kutenda kazi kwa urahisi/wepesi ni pale akili yako itakubaliana na sauti ya mbingu ( Roho mtakatifu).

Ili mbingu iweze kuingilia teso lako ni muhimu mbingu iwe ndani yako nawe uwe ndani ya mbingu ili ikupe urahisi wa kutambua hii ni sauti ya mbingu na hii sio sauti ya mbingu.

Unapoishi maisha ya mbingu kicheko kinakuwa maisha yako uwa haucheki/ufurahi kwakuwa kitatokea au kikitokea bali kikianza ndani ya moyo wako basi unajua kimeshatokea.

Wakati mwingine unaona kama hauna maisha yako binafsi lakini muhimu sio kuishi tu bali usalama wa maisha katika mikono ya Mungu.

Warumi 8:14………
“Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu”.
Ni muhimu na ni bora usiende na mtu yeyote lakini hakikisha umeenda na mbingu hapo utafika salama.

Kutoka 33:14……….
“Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha”.

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………….0764 018535