Jumamosi, 12 Septemba 2020

NENO LAKE NDIO UTOSHELEVU WAKO!




Yohana 21:1…….
1 Baada ya hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi wake, penye bahari ya Tiberia, naye alijidhihirisha hivi.
 2 Simoni Petro, na Tomaso aitwaye Pacha, na Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, na wana wa Zebedayo, na wengine wawili wa wanafunzi wake, walikuwapo pamoja.
 3 Simoni Petro aliwaambia, Naenda kuvua samaki. Nao wakamwambia, Sisi nasi tutakwenda nawe. Basi wakaondoka, wakapanda chomboni; ila usiku ule hawakupata kitu.
 4 Hata asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufuoni; walakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu.
 5 Basi Yesu akawaambia, Wanangu, mna kitoweo? Wakamjibu, La.
 6 Akawaambia, Litupeni jarife upande wa kuume wa chombo, nanyi mtapata. Basi wakatupa; wala sasa hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki.

Masumbuko ya wanafunzi wa yesu yalitatuliwa baada ya kufuata neno lililotoka katika kinywa cha yesu “ litupeni jarife upande wa kuume wa chombo, nanyi mtapata”

Moja ya sababu za harakati za wengi hasa katika dunia tuliyopo ni hali ya kutafuta utoshelevu ( hali ya juu katika kukizi mahitaji binafsi ).

Kuna aina mbili ya utoshelevu katika dunia ( ulimwengu );
i.                    Utoshelevu wa nafsi
ii.                  Utoshelevu wa mali
Unaweza kuwa na kila kitu lakini bado nafsi ikajisikia bado ina uhitaji mkubwa, unaweza kuoneka kwa macho au wakufukirika tu lakini uhalisi unabaki kwako.

Unaweza kukuta mtu atulii kuanzia mwili hata akili, na hali hii uweza kumtokea katika harakati za kuhitaji kukizi uhitaji alionao ili utoshelevu uweze kudhihirika katika maisha yake.

Wako watu wanaacha kazi, huduma au shughuli binafsi baada ya kuona kitu anachokifanya akimletei utoshelevu anaoutaka, na hata wakati mwingine hata kule alikoamia kunaweza bado pasimpatie utoshelevu anaoutaka/alioukusudia akabaki kung’ang’ana tu.

Moja ya jambo au kitu kinachoweza kuwafanya watu kushindwa kufikia katika utoshelevu wa jambo lililokusudiwa ni mtazamo usio sahihi wa jambo husika ( matarajio ya kufikirika yasio na uhalisia ).
Wakati mwingine unaweza kukuta unaacha kitu sahihi ulichotakiwa kukifanya kilicho sahihi kabisa na ukaenda kufanya kufanya kitu kingine kabisa ambacho ukutegemewa kufanya lakini ukaona neema za Mungu zikizidi kukuzingira na kukupa mkate wa kila siku hali hiyo haina maana kuwa Mungu anafurahia.

Yohana 21:15…………..
Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda.  Akamwambia,  Lisha wana-kondoo wangu.

Baada ya yesu kuhakikisha simon petro ameshakula ndipo akamuuliza swali “ je! Simon wa yohana, wewe wanipenda…………………. Akamwambia chunga kondoo zangu” ( maana petro baada ya kupewa samaki na kula ndipo yesu akamkumbusha jukumu lake la msingi la kukaa na kuendelea kumsubiri bwana hata ujio wa Roho mtakatifu utakapofika au kuajilia.

-          Ndomana yesu anajaribu kumsisitizia asisahau kuishi kwenye kusudi lake hata kama hali ikiwa ngumu kiasi gani? Atulie hapo maana yeye aliyekupa neema ya kuwa hapo atakupa utoshelevu wake.

Uhitaji wowote ulio katika mwili ( uhitaji wa nafsi ) uwa hauna kikomo na ukisumbukia hauwezi kudumu katika lengo kuu uliokusudiwa na hivyo kupelekea kushindwa kupata utoshelevu usioisha.

Ni muhimu utambue utoshelevu uliobebwa na neno lililo katika kinywa cha yesu, anachosema ndicho kinachobeba utoshelevu kinachoshikiliwa na yeye mwenyewe.

Penda kuishi sawa na neno linalotoka katika kinywa cha yesu mwenyewe na sio sawa na wimbi la dunia linavyokwenda, kwakua linavyokwenda linakwenda  na kishindo cha kukutisha hama kukufanya uweze kupata wasiwasi juu ya mstakabali wa maisha yako husika.

Wewe ni asili ya NENO unapolikubali linaenda kutibua na kuanzisha utoshelevu wake na sio wa kufikirika katika akili?

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………… 0764 018535