Kwa wale walio darasani…………………. Uwa hatutatui au kupata ufumbuzi wa swali la hesabu kwa kuwa tuna akili nyingi la asha! Kwasabu tunaijua kanuni na kuifuata/kuitumia na ndipo hapo tunapata utatuzi au jibu la swali husika!
Ni kweli moja ya msingi mzuri wa kufanya jambo ni lazima uwe na kitu cha kupelekea hilo jambo lifanyike hama lianze kufanyika.
Ndomana watu wanahitaji kuwa na plan ( malengo ) strategic ( mikakati ) katika kuyakamilisha mambo mbalimbali, japo wakati mwingine hatua zote hizo zinaweza kufuatwa lakini bado unashindwa kukipata kitu unachotakiwa kukipata.
Wataalam wengi wanasema unapokuwa na wazo ni mtaji mkubwa kuliko mtu kuwa na mtaji huku hana wazo, lakini pia kusimamia mawazo yako na kuthubutu ni jambo la msingi sana.
Ndomana mambo mengi kabla ujayaingia yanahitaji maandalizi, watu wengi wanasema maandalizi mazuri upelekea matokeo mazuri japo si wakati wote hali hiyo inaweza kuwa hivyo.
Ni kweli kuwa na maandalizi mazuri ni msingi mzuri kufanya mambo yatokee kulingana na maandalizi yako, mathalani nchi nyingi za ulaya zinafanya mambo makubwa mengi kwasababu mambo mengi kabla hayajawekwa wazi yameshapitia majaribio mengi na hata kuchukua miaka ya kutosha kabla ya uvumbuzi wake kwa mfano. Uvumbuzi wa vifaa, program na hata matibabu ya magonjwa mbalimbali.
Ni kweli hata katika upande wa Mungu maandalizi ni kitu cha muhimu sana, ndomana ahuhitajiki ukulupuke pindi unapofanya jambo la Mungu au jambo lolote ambalo linalohusu maisha yako hasa ukiwa umeokoka na umemjua Mungu.
Maandalizi ya Mungu hayahitaji sana usishwaji wa akili za kibinadamu, hizo zipo katika matumizi yake lakini zisibebe jukumu lote katika utendaji wa jambo husika ( akili zisiwe mtendaji mkuu katika maisha yako maana kuna wakati zinashindwa kutoa majibu ).
Unapaswa kuelewa kuwa akili ya mtu ina mapana yake lakini uweza wa Mungu una namna yake katika kufanikisha jambo lolote lililo katika maisha yako.
Ni kweli unaweza ukaomba, kufunga na kufanya mambo mengi katika maisha yako lakini bado unaweza usiweze kuona kule kufika unakotakiwa kuwa.
Unaweza usifuate/ usifanye mambo mengi yanayoonekana kwa watu kama wewe unavyomjua Mungu lakini ukiwa makini na kufuata maelekezo ya Mungu katika jambo husika, basi hapo utayaona maisha kwa jicho la Mungu na kufika kusiko pingwa na chochote.
Unahitaji kutambua na kuelewa kuwa ushindi au kufika kwako akuja bebwa na kile ulichonacho mkononi fedha, mali n.k bali katika umakini wa kufuata maelekezo yake kwakuwa kila swali/jambo lina njia yake yakupata ufumbuzi.
“ Hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea “…………………… l wakorintho 10:13
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………… 0764 018535