Jumatatu, 15 Machi 2021

UMEMALIZA!

 



Namna sahihi ya kuona uzuri wa kitu ni kufanya kitu kisha ukamaliza au ukafikia hitimisho……….Na furaha ndani ya moyo wako ikasema “ hatimaye umemaliza au umefanikiwa “

Kitu chochote ambacho utakifanya kikashindwa kufika mwisho basi masikitiko na huzuni uweza kuukamata moyo na zaidi sana ukajutia kwanini umepoteza muda kufanya jambo ambalo alitafika mwisho au kuwa na mwisho ambao hauta upendelea wakati mwingine mwisho wa kitu ndio mwanzo mzuri kuzaliwa kitu kingine!

Karibu sana………………………………………………………………….!

Katika maisha ya wokovu kuna kitu cha msingi ambacho ndio muhimiri wake, ambacho kwa hicho ndipo unaweza ona radha ya wokovu na hatimaye kuufurahi hicho kitu kinaitwa Roho mtakatifu ( master key ).

Unapoishi maisha na Roho mtakatifu uwezi kushindwa katika kila kona inayohusu maisha yako ni lazima utaibuka mshindi.

Yohana 14:16-18

16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

 18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

 

Yesu alipokuwa anakaribia kuondoka alijua ili utawala wa Mungu uendelee katika ulimwengu hakuna shaka Roho mtakatifu inabidi awepo kama yeye alivyoweza kuishinda dunia ndivyo naye kupitia Roho mtakatifu waaminio waweze kushinda.

Roho mtakatifu ndio kiunganishi chako kati ya wewe na Mungu, yeye ndiye anamfunua Mungu katika akili yako.

1 wakorintho 2:10-11

10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

 11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu

“ hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu”

Unapojua namna sahihi ya kukaa na Roho mtakatifu basi hapo inakuwa ni rahisi kuubeba moyo wa Mungu, maana ndicho kipenzi pekee cha Mungu.

Mathayo 12:31 Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.

“ dhambi zote watasamehewa lakini si kumkufuru Roho mtakatifu”

Unapokuwa na Roho mtakatifu unakuwa ni sawa na mtu aliyepewa kibali cha kuingia ofisi yoyote na kupata unachotaka mathalani ofisi ya afya, uchumi, mahusiano na mengine mengi ukiwa naye huyo uwezi kukwama wala kupotea.

Ni muhimu utambue kila jambo lina wakati wake hauhitaji kuona unachelewa maana “ baba ugawa sawa apendavyo yeye”

Anapokuona unastahili atakupatia tu ili mradi umempa nafasi ya kutosha Roho mtakatifu katika uelewa sahihi.

Katika mambo yanayo muhusu Mungu uwa atustawi kwa jambo lingine lolote bali kwakuwa tunatambua na kuishi katika maongozi yake.

Japo wakati mwingine kuna kujisahau na kuanza kuishi kwa kujisikia sawa na utashi wako na wala sio kwa maongezi yake, tambua hali hiyo inapoanza kutawala kinachokusaidia hapo ni neema ya Mungu tu.

Uwezi kuishi sawa na jicho la Mungu lilivyokusudia nje ya maongozi ya Roho mtakatifu.

Na mungu ili akuamini kwa mambo makubwa anaangalia namna gani umejidhatiti na kujigharimu katika kutembea na Roho mtakatifu,

Matendo ya mitume 13:22……..

22 Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.

“ Nimemuona mwana wa yesu (Daudi ) mtu atakayefanya mapenzi yangu yote”

Hauhitaji kujitambulisha pindi unapokuwa na Roho mtakatifu yeye mwenyewe atajitambulisha na watu watajua yuko ndani yako.

Moja ya sababu inayopelekea changamoto nyingi wa kristo wengi wanazopitia ni hali ya kutompa Roho mtakatifu nafasi kamili katika utendaji wake.

Hapo unaweza kujitahidi sana lakini yeye anasubiri umpe nafasi yake naye afanye anayoyapaswa kufanya kwako.

Uwezi kuchoka wala kukata tamaa unapotembea katika njia zake.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………..0764 018535