Ijumaa, 27 Januari 2023

UTAMBULISHO WA KIMBINGU;

 



Katika dunia ya leo moja ya kitu cha maana kwa watu wengi ni namna anavyotambulishwa, vile unavyo mtambulisha itafanya ajisikie vizuri kuwepo na asijute kwanini nimekuja.

Kuna baadhi ya watu ukikosea kuwatambulisha kwa hadhi waliyonayo, usishangae ghafla akachukua maamuzi ya kuondoka au akavumilia ila baadae akakufuata na kukwambia “ sijapenda jinsi ulivyo nitambulisha “ hivyo utambulisho umekuwa jambo la msingi hata kuliko chakula cha gharama yoyote ulichomwekea.

Na katika dunia hii kuna utambulisho mwingi na wakati mwingine kila utambulisho unakuwa na sababu zake au msingi wake.

Kuna wakati unaweza kutambulishwa hata kama  hauna sifa hizo lakini yote ni katika ushawishi ufanye matakwa yao hama katika kukufanya utoe mchango au ahadi kubwa itakayo wafurahisha hao watu, na pindi utakaposhindwa kufanya matakwa yao huo utambulisho hautausikia tena ukitamkwa kinywani mwao.

Kwa asilimia kubwa utambulisho ubadilika kutokana hatua mpya utakayopiga katika maisha yako mathalani ulikuwa binti baada ya kuolewa utaitwa mke na baada ya kuzaa utaitwa mama, ndivyo hivyo hata upande wa elimu kadili unavyozidi kusoma kutoka hatua ya kwanza na kuendelea  ndivyo utambulisho wako utakavyobadilika mathalani kutoka shahada moja kwenda shahada ya pili hama kuongeza elimu katika taaluma yako na hata ukawa dokta hivyo ndivyo utambulisho wako utakavyobadilika kadili unavyoongeza elimu yako.

Naam hivyo kuna utambulisho unaotokana na ulimwengu hama dunia pia kuna utambulisho unaotoka mbinguni kila utambulisho una utaratibu wake ili ukufikie lakini utofauti mkubwa katika ya utambulisho wa mbingu na duniani ni kutokuwa na mipaka katika utambulisho wa kimbingu kwakuwa wenyewe ufanya kazi/utawala dunia hata mbinguni.

Ila ni maamuzi binafsi uishi katika utambulisho upi kama wa mbingu au dunia? Kila utambulisho una utaratibu wake, na kila maisha unayoishi yanaonyesha  utambulisho gani inabidi uambate katika maisha yako.

Utambulisho wa dunia unahitaji akili nyingi ( za kidunia ) katika kuujenga na kuutetea ili uendelee kuwa nao, ila utambulisho wa mbingu una namna yake wala ahuhitaji usaidizi wako bali unahitaji usaidizi wa kudumu katika maelekezo yake ili nao uzidi kushamiri ndani yako.

Na utambulisho wa kimbingu huu ni utambulisho ambao ulikuwa nawe kabla ujazaliwa au ujaja duniani ulishaunganishwa tangu tumboni mwa mama yako.

Yeremia “  Nalikujua tangu tumboni mwa mama yako………….”

Yeremia 1:5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Ukitaka kuushinda dunia lazima ukubali kuishi katika utambulisho kimbingu maana huo ndio utambulisho ulikuwa nao kabla ujazaliwa na baada ya kuzaliwa na hata hitimisho la maisha yako.

Utambulisho wa kimbingu unakufanya uishi maisha ya ushindi hapa duniani na kufanya uishi maisha yaliyo salama.

Pindi unapoishi maisha ya utambulisho wa kimbingu basi hapo udhihirisho wa nguvu ya Mungu katika hatua za maisha yako unakuwa dhahiri.

Uwezi kuufurahisha moyo wa Mungu endapo hautakubali kuishi katika utambulisho wa mbingu maana hapo hauwezi kutembea katika akili yake hivyo ushindi ni ngumu kudhihirika katika maisha yako.

Tamani na uwe na fahari katika kutembea ndani ya utambulisho wa kimbingu maana kwa huo utambulisho unakuwa vile Mungu anavyotaka uwe.

Utambulisho wa Mungu unatunzwa kwa gharama yoyote kwakuwa usipotunzwa unaondoka kwako hapo ni lazima ukubali kufuata maelekezo yake kwa gharama yoyote ili uendelee kuishi ndani ya utambulisho huo.

INAITWA SIKU| BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………….0764 018535

Ijumaa, 13 Januari 2023

UPANDE ULIOSALAMA

 



Upande ulio salama ni sehemu ambayo mtu umpa uhakika au matumaini wa kuiona kesho kwasababu leo anaweza kujiona yuko salama kwa kuwepo mahali hapo! Au ni sehemu ambayo mtu umpa uhakika wa kutimiza ndoto yake hama kukamilisha lengo lake.

Sehemu salama ni chaguo la watu wengi, waliotabaka la juu na hata la chini ( wenye uwezo wa chini na wenye uwezo wa juu ).

Kuna usalama wa akili, mwili na hata wa mazingira.

Hususa kuna usalama wa nje na usalama wa ndani!

Wako watu wana amini usalama unaweza kuwepo kutokana na aina ya watu alikuwa nao na wakiamini kwa kuwepo kwao basi hapo usalama utazaliwa kama sio kudumu.

Kwa mana rahisi upande uliosalama ujulikana kama upande wa ushindi ambao baada ya ushindi mwishowe uweza kujisikia raha.

Naam kuna usalama unaoonekana kwa macho na kukushawishi kusema kuwa hapa ni sehemu salama lakini mahali hapo panaweza kuwa na usalama hama pasiwe na usalama, pia inawezekana kwa kuona mahali unaweza usiuone usalama kwa namna uonavyo wewe lakini mahali hapo panaweza kuwa ni sehemu salama na yenye ushindi mkubwa kwako.

Na upande uliosalama au unaonekana ni salama ni kimbilio la watu wengi, maana wana amini mahali penye usalama amani itakuwepo na maisha yataenda.

Mtu yeyote mwenye akili upenda kuwa katika upande uliosalama/ushindi akijua ataikwepa aibu/fadhaa na kupata heshima.

Na moja ya teso kubwa katika maisha ya mwanadamu ni kuishi uku aibu ikiambata katika maisha yake pasipo kujali hiyo aibu imesababishwa na mtu binafsi au mtu mwingine lakini inapokuwa aibu tu inatosha kuwa usumbufu katika maisha yake na hata kumfanya kuwa mnyonge siku zote.

Hivyo upande uliosalama uweza kuwa chaka la kuficha aibu ya mtu,

Nipende kusema kwamba sio mahali penye watu wengi ndio itakuwa timu ya ushindi la asha! Bali kinachoashiria ushindi au usalama ni maarifa waliyonayo na vifaa walivyonavyo ikienda sambamba uzoefu pamoja na ujuzi wa kutumia hivyo vifaa.

Katika maisha ya kiroho ( waliookoka kweli ) mtu ubeba usalama na ushindi ndani yake, hivyo kama ndani yake ajabeba ushindi na usalama asitegemee kuupata nje yake.

Haijalishi kama umezungukwa na watu wenye nguvu sana ukafikiri basi hapo uko salama uharibifu unaweza kupita katikati yao na kukupata japo umezungukwa na watu wenye nguvu ila wewe huna nguvu ndani yako.

Mathalani unaweza ukawa mwanafunzi mwenye uwezo mdogo ( kilaza ) pindi ukaingia katika chumba cha mtihani ukapata bahati ya kuzungukwa na vipanga (watu wenye uwezo mkubwa ) na ikatokea usimamizi ukawa mkali hata ikitokea umedondosha peni uruhusiwi kuishika bali msimamizi anakuja kukupatia hata ikidondokea miguuni pako tu, naam hapo haijalishi utakuwa wa kwanza kutoka au wa mwisho pindi matokeo yatakapotoka kila mtu atavuna kile alichokipanda sawa na uwezo wake.

Hivyo kuzungukukwa kwa wale wanaosikia baridi usifikiri utaanza kusikia joto bali kila mtu atasikia hali inayotawala katika mwili wake na sio nje ya mwili wake.

Unapaswa kujua pindi unapokuwa upande wa nuru basi hapo giza uweza kutawanyika hama linakosa nafasi ya kutawala.

Wakati mwingi tamani uwe upande wa mbingu maana mbingu haitakuchoka kukunenea mema juu yako lakini ukiwa upande wa watu wengi watu watachoka, watasahau na zaidi ya hayo nao wana mambo yao kama sio maslahi yao.

Watu wanaweza kukushikilia wakati wana nguvu wakichoka watakuacha, maana watakukumbatia pale watakapoona kuna maslahi yao na pindi maslahi yatakapoisha watakuacha peke yako pasipo mahali pa kuegemea.

Unapokuwa na watu usikae na watu kana kwamba hao ndio pumzi yako pasipo hao uwezi kupumua ila unapokaa na mbingu ( Mungu ) uone hapo ndio umilele wako ulipo maana ni yeye tu pekee aliyekujua, anayekujua na ndiye anajua utakuaje maana alipangalo hakuna wa kulipangua.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson………………………………………………………….0764 018535