Ijumaa, 23 Juni 2023

UNAISHI KWENYE HATMA YA NANI?



Kuishi ni jambo moja na hatma ni jambo lingine, kwa maana unaweza ukaishi ila usiishi katika hatma yako.

Wakati mwingine kuishi kwenye hatma yako inakuja baada ya kujivumbua kwa walio wengi ila kwa upande wamchao Mungu unajikuta unamsukumo wa ndani zaidi katika jambo fulani kuliko jambo lingine.

Ili uweze kufurahia kuwepo hapa dunia unahitaji kuwa na furaha ya Mungu na furaha ya Mungu inapatikana pindi utakapoishi katika hatma uliyokusudiwa/ aliyokukusudia.

Na hatma ya Mungu inaanza kuchukua nafasi ndani yako mara baada ya wewe kuokoka, hauwezi kutembea katika hatma ya kimungu bila kuokoka!

Naam katika ulimwengu wa sasa na namna dunia ilivyochangamka watu wengi awatafuti hatma zao bali utafuta fursa ili maisha yaende.

Maana fahamu za watu ufikiri kuitafuta sana hatma yako inaweza kupelekea kuishi nje na wakati unaoenda kasi. ( huendi na wakati )!

Na baadhi ya fursa zinaua hatma za watu kwa kujua au kutojua.

Ni kweli hali ya dunia ya sasa ina namna yake ya kuishi ili ukubalike lakini maisha baadae yanategemea namna ulivyouitumikie hatma yako ya sasa na ustawi wake.

Hauwezi kuwa wa maana kwa Mungu kama utaishi nje ya hatma ya kimungu mbele zake.

Ni kweli duniani watu wameumbwa kutegemezana ndo mana kuna watu wako kwa ajili ya wengine zaidi na neema inakuwa juu yao.

v  HATMA ni kile kitu kwa hicho uliumbwa au kuzaliwa wengine wanaita “ talent” na kila mtu ana kipawa chake mwingine ni bora katika kuimba, kupiga vyombo vya muziki, wengine kuongea vizuri, kufariji, matendo mema na wengine kufadhiliana.

Wako wengine wanaonekana sana kuwa waongeaji sana, wengine wamepewa jina na kuitwa kilopo au wambea na mengine mengi. Lakini Mungu aliwakusudia kuwa ni watu wamuongelee yeye kwa watu wengine biblia inawahita wainjilisti,

Hatma inafanya kazi kwa ukamilifu mahali ambapo yeye yupo kwa kusema hivyo ni lazima uwe umeokoka ili Mungu ajifunue kupitia wewe.

Unahitaji kusimamia hatma yako haijalishi watu wanakuonaje ili usababishe furaha ya kudumu katika moyo wa Mungu.

Ili uweze kukitumia kipawa chako vizuri unahitaji uwezesho wa Mungu maana kwa yeye ulitokea na kwa ke utarejea.

Namna dunia ya sasa ilivyo na ushawishi mkubwa unaweza kuingia katika mkondo ambao sio wako kutoka na ushawishi unaotoka ndani yako au nje yako, katika hali hiyo unaweza kuwa na furaha kitambo labda kutokana na jambo hilo basi familia yako unaweza kuihudumia na hata watoto kwenda shule pasipo msongo wa mawazo lakini utakosa furaha kamilifu ndani yako.

Unapo pata neema ya kuishi hapa duniani usitake wewe binafsi uyafurahie maisha yako kwa kuishi maisha unayoyataka bali mfurahishe yeye anayekumiliki anapoyaona maisha yako kwa kuyafanya yale uliyokusudiwa,

Unahitaji kujua ni furaha ya Mungu wewe uishi kwenye hatma yake ili ajisikie vizuri kukupa hazina zake uweze kuziwakilisha dunia kama apendavyo yeye.

Unapoamua kuishi maisha ambayo ni burudiko kwa Mungu naye atafanya burudiko katika maisha yako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………..0764 018535

 

Ijumaa, 9 Juni 2023

UFAHAMU UKIPONA MAISHA YAMEPONA!

 



Moja ya utambulisho wa mtu ubebwa na ufahamu wake, kwakuwa yale anayoyatenda na kuyafanya yanatoa tafsiri kwa watu wanao mzunguka vile alivyo,

Uzuri wa ufahamu wa mtu udhihirika kwenye kuongea na zaidi sana kwenye utendaji wake.

Katika dunia ya sasa unaweza kuwa kivutio cha wengi kwa kujua kuongea tu,

Na unaweza kujipatia ajira kirahisi kwa kujua kuongea tu, waajiri wakiami kama una uwezo wa kuongea vizuri basi atakuwa na uwezo wa kuongelea vizuri biashara/shirika lao.

Ni muhimu kujua kwamba unahitaji sana ufahamu kuliko kitu kingine chochote,

Na ufahamu ndio unaleta vitu na sio vitu vinaleta ufahamu!

Mtu anaweza kukuibia kila kitu na unaweza ukawa salama na maisha yakaenda lakini sio ufahamu maana ufahamu ukiharibika basi maisha yameharibika.

Mambo mengi yanayoendelea duniani, yanaitingisha dunia kwa namna moja au nyingine hasa hili wimbi la ushoga na usagaji haya ni matokeo au mafanikio ya watu kuweza kupenyeza uharibifu wao katika ufahamu watu na watu kuona hayo mambo ni sawa tu tena ni haki ya msingi ya binadamu, japo uharibifu huu unaweza kupata nafasi katika maisha ya mtu ukihusianishwa na tamaa ya maisha mazuri yasio fuata utaratibu ulio sahihi.

Na mtu akiweza kupitisha sumu katika ufahamu wako basi ameshayaharibu maisha yako na endapo mtu akiweza kupitisha uzima au nuru katika ufahamu wako basi hapo maisha yako yako usalama.

Ni muhimu kujua kuwa unahitaji kwanza ufahamu kabla ya kufanya kitu chochote, mathalani katika upande wa kilimo unaweza kuwa na kila kitu kinachohitajika kwenye kilimo ili uweze kupata mavuno makubwa kama vile eneo lenye rutuba, maji ya kutosha, mbolea pamoja na vifaa vya kisasa vya kilimo lakini endapo ufahamu wako utakuwa hautoshi katika eneo la kilimo basi hapo unaweza usipate mavuno ya kutosha au ukose kabisa.

Ni kweli kuwa na ufahamu mzuri bila fedha ni mateso ni sawa na kubeba sufuria iliyo na maji ya moto sana ukitegemea hayata kuunguza badala yake yatafanyika kuwa baridi,

Lakini katika asilimia kubwa ukiutumia vizuri ufahamu unaweza kukupa njia ya kupata fedha.

Na ili uendelee kufanya yale mazuri unayo yafanya  na yenye tija katika jamii unahitaji kudumu katika ufahamu huo na ili uweze kupiga hatua yoyote ni lazima uanzie hatua hiyo kwenye ufahamu wako,

Ufahamu ukipiga hatua basi na mambo yako yatapiga hatua ni kama vile ambavyo ukibadilisha gear hata mwendo wa gari nao unabadilika.

Ili uwe bora unahitaji ufahamu uliobora na sio kitu kingine maana nje ya ubora wa ufahamu hakuna kitu kitakuwa bora labda kiendelee kuwepo tu pasipo ongezeko.

Daniel 6:3 Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.

 Ilihitajika akili ya ubora iwe ndani ya Daniel ili afanye mambo yatakayo kuw majibu ya maswali ya mfalme au teso la jamii husika.

Ni muhimu ujue kuwa ilihitajika mwenye akili mmoja ili aweze kuleta mabadiliko makubwa katika dunia, kwa akili ya mtu ndege ikapatikana, umeme ukatokea, meli ikavumbuliwa kama chombo cha usafiri wa majini na mengine mengi.

Na unapoongeza ufahamu basi hapo umeongeza nguvu ya kuendelea na kuwa wa maana zaidi.

Mtu aliyetengeneza simu mpaka sasa imekuwa kitu chenye umuhimu mkubwa katika dunia ya leo alihitaji ufahamu kwanza kabla ya fedha japo ufahamu ulipotumika fedha ikahitajika na baadae yeye mtengenezaji kuanza kuvuna pesa.

Unahitaji ufahamu kwanza kuliko chochote kwakuwa vyote vinazaliwa katika ufahamu.

Na hata tatizo linakuwa na nguvu  kwako au linakosa nguvu kwa sababu ya maarifa uliyonayo.

Wataalamu wengi wa kisaikolojia wanachofanya zaidi ni kutia nuru katika ufahamu wako uliokosa nuru ili uweze kuona kuwa hilo jambo sio mwisho wa maisha yako, mathalani katika kipindi cha mwanzo mtu anapoenda kupima na kugundulika kuwa ameathirika na virusi vya ukimwi basi hapo wagonjwa wengi uweza kuona mwisho wa ndoto zao lakini wanapokutana na mshauri baada ya kuwapa mwanga basi hapo uweza kuona kumbe maisha yanaweza kuendelea.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………………………..0764 018535