Ijumaa, 20 Desemba 2024

ANAKUACHA ILI UIVE

 

Kuna ladha nzuri ya chakula unaipata au unaisikia katika kinywa chako pindi chakula kinapokuwa kimepikwa na kuiva vizuri.

 Bila shaka hata hamu ya kula itaongezeka.

Na ili chakula kiweze kuiva vizuri unahitaji kukipa muda mzuri kwa kila hatua ya upishi wako, usifanye haraka hata ikapelekea kuunguza chakula au kutoiva vizuri, maana kinapoiva vizuri hata ( ubora ) ladha yake utokea katika kiwango chake.

Hivyo hivyo Mungu hana haraka katika kukuondoa katika mazingira yanayokuzinga!

Pindi anapokuona uko tayari anaweza kukuachilia ili uweze kufanya yakupasayo kufanya,

“ kaeni humu hata Roho hatapo wajilia” yesu

Luka 24:49 Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.

 

“ haraka haraka haina baraka “ dunia

 

“ polepole ndio mwendo “ dunia

 

- hizi ni kauli za dunia zikiwa zimebeba namna subira imebeba matokeo chanya katika maisha ya mtu.

Pia ni muhimu kuwa na angalizo kuwa kuna wakati unaweza kujiona kuwa uko tayari lakini kimsingi unaweza usiwe tayari.

Mungu anapenda ukamilike katika ubora wake ( uive ) uwe tayari kukabili changamoto/ upingamizi wa dunia.

“ kaeni hapa mpaka mtakapo pokea nguvu “ yesu

Matendo 1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Kuna namna utakuwa pindi hiyo nguvu utakapo kuvaa na kuanza kuaminika kufanya upasayo kuyafanya.

Hali hii ipo hata katika dunia ya leo mathalani pindi mzazi anapotaka kumkabidhi madaraka makubwa mwanaye inawezekana katika kusimamia biashara au shughuli yoyote ni mpaka mzazi awe amejiridhisha ndio amkabidhi au amepatwa na mauti basi mrithi inabidi achukue nafasi japo kuna wakati anaweza kuwa chini ya uangalizi kama anaonekana hatoshi mpaka pale atakapo kuwa na uwezo wa kusimamia hizo shughuli na kuleta matokeo mazuri katika biashara hizo.

Lakini mzazi angalipo hai na akawa na mashaka na uwezo wa mwanae inabidi awe chini ya msimamizi mpaka pale atakapo pata uwezo wa kujisimamia mwenyewe.

“ mrithi wakati wote hawapo mtoto hana tofauti na mtumwa ingawa ni bwana wa yote “ mtume. paulo

Wagalatia 4: 1 Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote;

 2 bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba.

 3 Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.

Unapaswa kujua Mungu anapokuacha mahali fulani mara zote inakuwa ni kwa faida yako maana anajua bado ujawa vizuri na endapo akakuachia ukaenda kupigana unaweza ukashindwa.

Mathalani pindi mtoto anapozaliwa akawa dhaifu na akaonekana kuwa anahitaji joto la mama yake ili aweze kuimarika zaidi ni wajibu apewe hata kama ataonekana anamuonekano mzuri kiasi gani? Maana hiyo inakuwa ni kwa faida yake.

Sio kwamba Mungu apendi kukupa mazuri/ yale unayo yatamani bali anahitaji kuona una iva kwanza ili ufae kukipata kile unachopaswa kukipata.

Ni muhimu sio unachokiona basi unaanza kukitamani kukimiliki mathalani mtoto anapoona ndege na kumwambia baba yake ni nunulie ndege! Ni kweli mtoto anahitaji ndege?

- maana kuna vitu vya muhimu na vitu vya lazima.

Kuna baadhi ya vitu unaweza kuvitamani uwa vimebeba mauti yako ya kimwili au kiroho unaweza kuona kama unacheleweshwa au unanyimwa haki yako lakini sio kweli.

“ najua mawazo ninayo wawazia ninyi ni mawazo ya amani kuwapa tumaini siku zenu za mwisho “ yeremia

 Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Unahitaji kujua kuwa Mungu ni baba mwema pindi unapoamua kuwa chaguo lake basi maisha yako yote yeye ndiye anayaratibisha kwa upendo usioelezeka.

Unapaswa kutambua umuhimu wa kuandaliwa vizuri ( uive ) ili uweze kufit sehemu husika, ni kama chakula kilicho iva vizuri kina kuwa na tija katika mwili wa mwanadamu na sio uharibifu.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………………………………..0764 018535