Ijumaa, 25 Aprili 2025

WAZO LA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO:

 



Moja ya kitu kigumu katika maisha ya mwanadamu ni kutambua mawazo anayo kuwazia au anayomuwazia mtu mwingine.

Laiti tungetambua mawazo ya mtu kabla ya kufanya jambo hasa linalo onekana lina sura ya wema bila shaka baadhi ya watu tusingekubali kupokea wema wao kwa kutambua mawazo yao mabaya juu yake.

Pia tungepata uwezo wa kutambua mawazo anayokuwazia hata rafiki yako wakati wote kuna baadhi ya watu unaweza kushindwa kuamini kweli huyu ni rafiki yangu au ni mtu mwingine tu.

Bila shaka katika ulimwengu wa mawazo ndio uliobeba uhalisia wa kweli kuliko kile anachokisema kwa maana sio wakati wote kile anachokisema kimeshikana na moyo wake.

Ni kweli mawazo yako kwa mtu ni fumbo lakini sio mbele za Mungu, kwakuwa mawazo yako kwake ni sauti kubwa isiyo na mwangwi hivyo kwa Mungu sio fumbo.

Wote mkifanikiwa kuwaza mamoja bila shaka umoja wenu utakuwa na nguvu sana kwakuwa utakuwa umeshikwa na kitu ambacho akiwezi kutanguliwa.

- uharibifu wa makundi mengi huanzaia katika mawazo yao.

 

Naam Mungu hafurahishwi tu na utendaji wako kwake bali wazo lako jema limebeba ukamilifu katika kusudi lake.

Mwanzo 1:5 Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.

 6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.

 

Ni kweli mawazo katika ulimwengu tuliyo nayo yanaweza kubadilika wakati wowote, hivyo huwezi kushangaa mtu aliyekuwa anakuwazia mema katika kweli usishangae kesho akaanza kukuwazia mabaya mpaka unaweza kufikiri hawa ni watu wawili tofauti.

Lakini wazo la Mungu juu ya maisha yako kamwe haliwezi kubadilika na wakati mwingine hata wewe ukibadilika bado wazo la Mungu lina kungojea urudi ili mema yake yaweze kumiminika kwako.

 Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si  mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Unapaswa kujua na kuweka msingi wako katika wazo la Mungu na sio katika mawazo ya wanadamu yanayoweza kubadilika wakati wowote.

Yakupasa kujua wazo la Mungu limebeba ukamilifu wa maisha yako na wema haukomi kamwe.

Na endapo ukafanikiwa kuishi katika wazo la Mungu bila shaka utakuwa salama ni kama samaki kuishi baharini maana hapo anayapata maisha yake.

Unapaswa kulijua wazo la Mungu katika maisha yako katika mapana yake ili hofu na mashaka visitawale katika maisha hata utakapo pita katika mazingira magumu.

Unapaswa kumwelewa Mungu kwamba ni yeye pekee ambaye wazo lake halishindwi kutimia katika maisha yako, ahadi yake ni kweli na amina.

 

Unahitaji kumwamini Mungu naye aweze kujidhihirisha katika maisha yako.

 

² hakuna mtu aliyeweka matumaini kwa Mungu alafu akaaibika

Zaburi 37:25 Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.

 

Unahitaji kuyaishi mawazo ili yaweze kudhihirika katika mwili.

Maisha yako yameanza katika wazo la Mungu hivyo unapoishi katika wazo lake basi hapo unaendeleza maisha yako katika chanzo chake sahihi.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………………………………………..0764 018535