Jumatatu, 29 Septemba 2014

USIKU WA MCHANA



USIKU WA MCHANA;



Ni swali lilogumu na la kushangaza sana pindi mtu anakuuliza jua uwezekano wa usiku kuingia mchana na isiwe kupatwa kwa mwenzi bali ikaitwa USIKU WA MCHANA. Na pindi kunapotokea usiku mchana je kunauwezekano wa kuwa mchana wa usiku, katika hali ya kufikirika hali hii inaweza kuwa ngumu katika hali ya kutokea bali katika uwezekano wa kutokea inaweza kutokea kwakua haukujua mchana ila mpaka umeuona na hata usiku ni hivyohivyo basi hali hii ikitokea basi unaweza kuita mchana wa usiku kwakua ukiona tu basi jina litatokea kwa wewe kuona.

Tunajua kwamba usiku ni muda wa kumzika baada ya kuutumikia mchana hivyo uchovu wa akili na mwili basi hapo ndipo kuna kuwa mahali pa kupumzika, hivyo usiku unapoingia mchana ni wazi yako mambo utayoshindwa kuyafanya kwa kua ulishindwa kuwa na maandalizi ya hali hii ya usiku mchana, hii ni hali ya kawaida sana kwani katika hali ya kawaida katika siku kunapo badilika hali ya hewa mathalani mvua inapokuwa nyingi yako mambo utashindwa kuyafanya inakuwa tofauti pindi hali ya hewa ikawa nzuri ikafanikishe yale uliyokusudia.

Ni wazi na kweli kabisa kwa mtu anayetembea mchana ni vigumu kumudu katika kutembea katika giza nene kwa katika giza nene ndio ishara ya wewe kujitambua.

Nini hasa maana ya kauli hasa?( usiku wa mchana);

i.kuzama wakati kuna meli
ni jambo la kushangaza sana meli kuwa salama halafu wewe ukazama, inajulikana kuwa meli ikishazama basi hapo kuzama ni jambo la kawaida hasa kwa wale ambao hawajui kuogelea au kutokana na hali iliyokushinda kutokea.

Hali hii inakuweka katika kipindi kigumu sana kwakua ujui lipi la kufanya kuona huyu nahodha anajali abiria wake au ajali na kwa nini? Katika kipindi hiki ukianza kumfikiria nahodha kwa nini ashughuliki na wewe ni wazi hapo kuzama ni jambo lisilo zuilika au kufa katika maumivu ya moyo ni jambo lisilozuilika.( nazungumzia maisha )

Na hali hii inatokea sio kwamba nahodha hakuoni na sio uzembe wako bali kutokana na maamuzi ya nahodha.

ii. kufa na njaa wakati chakula kipo

sio ajabu kusikia mtu au watu wamekufa kwa kukosa chakula kutokana na majanga yaliyo wakuta mathalani umaskini, vita au magonjwa na shida mbalimbali.

Pamoja na hayo pia kunauwezekano kubwa mtu kuachwa kufa na chakula pasipo kujali uzima wa mtu huyu ndio furaha yake ya kesho. Japo watu wanapogundua umekufa na huku ulikuwa na uwezo wa kula chakula na chakula kilikwepo lakini ujala nini shida haijajulikana.

Huu sio wakati mgumu kwako tu bali hata wale wanakuzunguka kwakua hawajui kwanini ulikufa wakati chakula kilikwepo na wewe ni mmoja kati ya watu wanaotakiwa kula kwakua kipo kwa ajili yao.

iii. kuwa hospitali na hali mbaya lakini ukakosa matibabu

Ni hali ya kawaida unapokuwa hospitali na unahitaji matibabu basi unafikiri ni sehemu muhimu na muhafaka katika maisha katika kupata matibabu ili kuimarisha.

Unaweza kuwa umelipia gharama zote za matibabu na wakati unategemea matibabu ya taanza una subiri na kukatamaa na unashindwa baada ya hapo ufanye nini basi kwakua nafasi yako umeitendea haki.

Wako watu wata weza kuamia sehemu nyingine katika kuokoa uhai wake na je! Uko wanakokwenda hali ikawa hivyohivyo utafanya nini?

Iv. Katika maumivu unazidi kukanyagwa

Ni wazi unapokuwa katika maumivu ni matarajio yako kuwa watu watafukuza nzi, na kukutia moyo na kutafuta kwa dhamiri ya dhati ya namna ya kukufanya uwe wa maana na bora na kuwa wa maana sana.

Lakini sasa si ajabu katika maumivu makali watu wanaweza pitisha gleda hili likumalize kabisa hatimae upotee kabisa na sura yako isiwepo tena.




Imeandaliwa na ;
                           Cothey Nelson, 0764018535, cotheyn@yahoo.com

MSHIKE MUNGU UTATOKA SALAMA!!!!!