USIKU WA MCHANA;
Ni swali lilogumu na la kushangaza sana pindi mtu
anakuuliza jua uwezekano wa usiku kuingia mchana na isiwe kupatwa kwa mwenzi
bali ikaitwa USIKU WA MCHANA. Na pindi kunapotokea usiku mchana je
kunauwezekano wa kuwa mchana wa usiku, katika hali ya kufikirika hali hii
inaweza kuwa ngumu katika hali ya kutokea bali katika uwezekano wa kutokea
inaweza kutokea kwakua haukujua mchana ila mpaka umeuona na hata usiku ni
hivyohivyo basi hali hii ikitokea basi unaweza kuita mchana wa usiku kwakua
ukiona tu basi jina litatokea kwa wewe kuona.
Tunajua kwamba usiku ni muda wa kumzika baada ya
kuutumikia mchana hivyo uchovu wa akili na mwili basi hapo ndipo kuna kuwa
mahali pa kupumzika, hivyo usiku unapoingia mchana ni wazi yako mambo
utayoshindwa kuyafanya kwa kua ulishindwa kuwa na maandalizi ya hali hii ya
usiku mchana, hii ni hali ya kawaida sana kwani katika hali ya kawaida katika
siku kunapo badilika hali ya hewa mathalani mvua inapokuwa nyingi yako mambo
utashindwa kuyafanya inakuwa tofauti pindi hali ya hewa ikawa nzuri
ikafanikishe yale uliyokusudia.
Ni wazi na kweli kabisa kwa mtu anayetembea mchana
ni vigumu kumudu katika kutembea katika giza nene kwa katika giza nene ndio
ishara ya wewe kujitambua.
Nini hasa maana ya kauli hasa?( usiku wa mchana);
i.kuzama
wakati kuna meli
ni jambo la kushangaza sana meli kuwa salama halafu
wewe ukazama, inajulikana kuwa meli ikishazama basi hapo kuzama ni jambo la
kawaida hasa kwa wale ambao hawajui kuogelea au kutokana na hali iliyokushinda
kutokea.
Hali hii inakuweka katika kipindi kigumu sana kwakua
ujui lipi la kufanya kuona huyu nahodha anajali abiria wake au ajali na kwa
nini? Katika kipindi hiki ukianza kumfikiria nahodha kwa nini ashughuliki na
wewe ni wazi hapo kuzama ni jambo lisilo zuilika au kufa katika maumivu ya moyo
ni jambo lisilozuilika.( nazungumzia maisha )
Na hali hii inatokea sio kwamba nahodha hakuoni na
sio uzembe wako bali kutokana na maamuzi ya nahodha.
ii.
kufa na njaa wakati chakula kipo
sio ajabu kusikia mtu au watu wamekufa kwa kukosa
chakula kutokana na majanga yaliyo wakuta mathalani umaskini, vita au magonjwa
na shida mbalimbali.
Pamoja na hayo pia kunauwezekano kubwa mtu kuachwa
kufa na chakula pasipo kujali uzima wa mtu huyu ndio furaha yake ya kesho. Japo
watu wanapogundua umekufa na huku ulikuwa na uwezo wa kula chakula na chakula
kilikwepo lakini ujala nini shida haijajulikana.
Huu sio wakati mgumu kwako tu bali hata wale
wanakuzunguka kwakua hawajui kwanini ulikufa wakati chakula kilikwepo na wewe
ni mmoja kati ya watu wanaotakiwa kula kwakua kipo kwa ajili yao.
iii.
kuwa hospitali na hali mbaya lakini ukakosa matibabu
Ni hali ya kawaida unapokuwa hospitali na unahitaji
matibabu basi unafikiri ni sehemu muhimu na muhafaka katika maisha katika
kupata matibabu ili kuimarisha.
Unaweza kuwa umelipia gharama zote za matibabu na
wakati unategemea matibabu ya taanza una subiri na kukatamaa na unashindwa
baada ya hapo ufanye nini basi kwakua nafasi yako umeitendea haki.
Wako watu wata weza kuamia sehemu nyingine katika kuokoa
uhai wake na je! Uko wanakokwenda hali ikawa hivyohivyo utafanya nini?
Iv.
Katika maumivu unazidi kukanyagwa
Ni wazi unapokuwa katika maumivu ni matarajio yako
kuwa watu watafukuza nzi, na kukutia moyo na kutafuta kwa dhamiri ya dhati ya
namna ya kukufanya uwe wa maana na bora na kuwa wa maana sana.
Lakini sasa si ajabu katika maumivu makali watu
wanaweza pitisha gleda hili likumalize kabisa hatimae upotee kabisa na sura
yako isiwepo tena.
Imeandaliwa na ;
Cothey Nelson, 0764018535,
cotheyn@yahoo.com
MSHIKE
MUNGU UTATOKA SALAMA!!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni