Jumanne, 30 Juni 2015

UHURU WA KUSHANGAZA!



HUU NI UHURU GANI?



Warumi 5:13

Hapa Duniani kama kuna kitu kimoja wapo ambacho watu wengi wanapenda sana ni kuwa huru,Na hivyo sio kitu cha kushangaza mtu uweza kujisikia vibaya sana pindi anapoona uhuru wake unapotea au unakandamizwa! Na dhana hii imekuwa ikitumika hata katika upande ushirika wa mtu na mtu ukiwapatinisha watu na wengine ikiwatenganisha wakisema kuwa huyu ni kiwa nae na kuwa huru sana kuliko ni kiwa na huyu………..hivyo mwisho mtu huyu atakuwa anapenda kuwa na mtu ambaye yeye anasema anajisikia uhuru nae na kutokuwa karibu ya mtu ambaye anaona uhuru kwake ni mdogo!

Sikatai mtu kuwa na uhuru binafsi na hautumie huo uhuru wake kwani karibu kila katiba katika dunia wanakifungu kina itwa HAKI ZA BINADAMU ndani yake kuna haki ya kuishi na ziko haki nyingine ambazo kama vile hali ya kuwa huru katika kutoa mawazo,kujumuika na wengine…..!japo kuna haki zingine zinaendana na wajibu lakini haki hii ya kuwa huru haiambatani na wajibu wowote zaidi ya kuheshimu uhuru wa mwingine………japo haki hii ina mipaka yake………..uhuru ulipitiliza uwa ni fujo!! Na hivyo kwakuzingatia hilo basi wakaweka mipaka ya kutumia hiyo haki ili isiwe shida kwa mtu mwingine!

Hali ya uhuru imekuwa na mchango mkubwa hata katika eneo la ndoa kudumu na hata kuvunjika kwahiyo katika ndoa uhuru umeleta furaha na kwa wengine umeleta dhuruba ambayo hawakuwai kuitegemea!

Unapokuwa na rafiki ambaye kila mtu uangalia uhuru wake na kuutumia pasipo hata kuangalia namna ninavyoutumia uhuru wangu hivi sio kero kwa ndugu yangu ni wazi huo urafiki wakati wowote na lolote linaweza kutokea.

Uhuru hatari!!!
Huu ni uhuru unausisha ubinafsi wa mtu na hali ya mtu anapokuwa mahali ambapo akili yake hajabanwa iko huru kufanya chochote ambacho yeye anakiangalia au anachoamini wala kujali kuwa hili swala ni kero kwa mwengu!

Hapa si zungumzii hali ya mtu kuwa huru pasipo shinikizo la nje ila linaweza kuwa ni shinikizo la ndani lakini kamwe sio la mazingira yeyote.
Katika mazingira haya mtu uweza kuwa uhuru wa kushangaza;

i.shule

hapa ni mahali pazuri sana kwa mtu kupata upeo mzuri wa akili yake ili uweze kumsaada katika maisha yake ya sasa na hata ya baadae ikimfaidia yeye,wazazi,ndugu na hata jamii kwa ujumla wake.

Lakini uwezi kuamini mahali hapa pamekuwa na jukumu lingine ambalo vijana wengi kwakua wako mbali na wazazi wao au walezi wameutumia uhuru wao katika kufanya mambo ambayo yanawaongezea mzigo badala ya kuwapunguzia yote hayo, kwa kisingizio kuwa moyo wangu umependa hivyo mimi siwezi kushindana na moyo inabidi ni ufuate tu maana ni wangu! Vijana wameingia katika shughuli zisizo halali wala wasio paswa kuzifanya wala kuzifikiria katika rika walionalo.

Secondary panakuwa mwanzo tu na inaweza ikaonekana au isionekane lakini tunapoingia kwa wataalam yaani chuoooooooo!! Huku ndiko kunakukubuu na kufuzu kulikopita wakufuzi na wataalam wakila aina, sijapata jina zuri linaoendana na wakati wa sasa watu kuwa huru kuona wanaweza kushiriki tendo la ndoa kwa yeyote maadam nafsi yake imempenda au imemlizia sio hilo basi yako mengi vijana wengi uweza kuona ni ukisasa kwenda kila tamasha hasa ya kidunia uwa ajali kingilio ni kiasi gani! Maadam mtu ameshapenda…………..anaweza fanya lolote ili mradi tu aweze kupata hela atakama kuuza mwili wake na hata kudanya wazazi wake au walezi wake.

Jamani huku kupenda kumekuwa ni janga sasa tunakoelekea watu wengi watapenda kufa!!!
Lakini mwisho wa safari itadhihirisha njia gani ambayo umetumia katika kufika hapo kwakua kila unachokipanda lazima utavuna!

ii.kazini
panaitwa ofisini au mahali pakuwajibika kwa ajili ya kujenga familia yako au maisha yako na hawapendao mathalani wazazi au wenzio!

Mtu anapokuwa huku anaona kuwa amewatiwa giza na wote(uhalali usio na matumizi sahihi ya mipaka) hivyo anaweza fanya lolote ambalo analojisikia pasipo kujali hii ni sawa au si sawa anaweza fanya jambo lolote anaweza kuanzisha mausiano ya kimapenzi na wengi akiwa huko ofisini na anaweza bosi wake na mfanyakazi mwenzake sina unajua tena mazoea ujenga urafiki na hatimae………!

iii.kijamii
hapa ni sehemu isiyorasmi kwa mtu kufanya kitu chochote mathalani mtu anaweza mwadilifu kazini lakini mtaani akawa mtu ,mlevi,mkorofi na hata asiye na upendo katika jamii yake
huku tunaweza sema mtaani mtu uweza kuwa huru kwenda popote na kufanya chochote anachojisikia pasipo kujali nini kitatokea katika maisha yake……unaweza kukuta mtu anaweza kwenda katika bar na kufanya kile ambacho akili yake itachomtuma…..pasipo kujali jamii inajifunza nini kwake, au anacha msingi gani katika maisha yake au anaacha malezi gani katika familia yake!

Kuna wengine wanaweza kwenda kwenye ngoma na wanakuwa huru kufanya chochote au kufanyiwa chochote, wako wengine wanaenda katika matembezi na huko wanaweza fanyachochote maadamu akili zimewatuma kufanya hivyo.

Yaliyobebwa katika ufahamu wako ndio matunda ya matumizi ya uhuru wako!

Imeandaliwa na;

Cothey  Nelson……………………………………………0764 018535

WEWE NI MATUNDA YA MATUMIZI YA UHURU WAKO!!!