HUU NI UHURU GANI?
Warumi 5:13
Hapa Duniani kama kuna kitu
kimoja wapo ambacho watu wengi wanapenda sana ni kuwa huru,Na hivyo sio kitu
cha kushangaza mtu uweza kujisikia vibaya sana pindi anapoona uhuru wake unapotea
au unakandamizwa! Na dhana hii imekuwa ikitumika hata katika upande ushirika wa
mtu na mtu ukiwapatinisha watu na wengine ikiwatenganisha wakisema kuwa huyu ni
kiwa nae na kuwa huru sana kuliko ni kiwa na huyu………..hivyo mwisho mtu huyu
atakuwa anapenda kuwa na mtu ambaye yeye anasema anajisikia uhuru nae na
kutokuwa karibu ya mtu ambaye anaona uhuru kwake ni mdogo!
Sikatai mtu kuwa na
uhuru binafsi na hautumie huo uhuru wake kwani karibu kila katiba katika dunia
wanakifungu kina itwa HAKI ZA BINADAMU ndani yake kuna haki ya kuishi na ziko
haki nyingine ambazo kama vile hali ya kuwa huru katika kutoa mawazo,kujumuika
na wengine…..!japo kuna haki zingine zinaendana na wajibu lakini haki hii ya
kuwa huru haiambatani na wajibu wowote zaidi ya kuheshimu uhuru wa mwingine………japo
haki hii ina mipaka yake………..uhuru ulipitiliza uwa ni fujo!! Na hivyo kwakuzingatia
hilo basi wakaweka mipaka ya kutumia hiyo haki ili isiwe shida kwa mtu
mwingine!
Hali ya uhuru imekuwa
na mchango mkubwa hata katika eneo la ndoa kudumu na hata kuvunjika kwahiyo
katika ndoa uhuru umeleta furaha na kwa wengine umeleta dhuruba ambayo
hawakuwai kuitegemea!
Unapokuwa na rafiki
ambaye kila mtu uangalia uhuru wake na kuutumia pasipo hata kuangalia namna
ninavyoutumia uhuru wangu hivi sio kero kwa ndugu yangu ni wazi huo urafiki
wakati wowote na lolote linaweza kutokea.
Uhuru hatari!!!
Huu ni uhuru unausisha
ubinafsi wa mtu na hali ya mtu anapokuwa mahali ambapo akili yake hajabanwa iko
huru kufanya chochote ambacho yeye anakiangalia au anachoamini wala kujali kuwa
hili swala ni kero kwa mwengu!
Hapa si zungumzii hali
ya mtu kuwa huru pasipo shinikizo la nje ila linaweza kuwa ni shinikizo la
ndani lakini kamwe sio la mazingira yeyote.
Katika mazingira haya
mtu uweza kuwa uhuru wa kushangaza;
i.shule
hapa ni mahali pazuri
sana kwa mtu kupata upeo mzuri wa akili yake ili uweze kumsaada katika maisha
yake ya sasa na hata ya baadae ikimfaidia yeye,wazazi,ndugu na hata jamii kwa
ujumla wake.
Lakini uwezi kuamini
mahali hapa pamekuwa na jukumu lingine ambalo vijana wengi kwakua wako mbali na
wazazi wao au walezi wameutumia uhuru wao katika kufanya mambo ambayo
yanawaongezea mzigo badala ya kuwapunguzia yote hayo, kwa kisingizio kuwa moyo
wangu umependa hivyo mimi siwezi kushindana na moyo inabidi ni ufuate tu maana
ni wangu! Vijana wameingia katika shughuli zisizo halali wala wasio paswa
kuzifanya wala kuzifikiria katika rika walionalo.
Secondary panakuwa
mwanzo tu na inaweza ikaonekana au isionekane lakini tunapoingia kwa wataalam
yaani chuoooooooo!! Huku ndiko kunakukubuu na kufuzu kulikopita wakufuzi na
wataalam wakila aina, sijapata jina zuri linaoendana na wakati wa sasa watu
kuwa huru kuona wanaweza kushiriki tendo la ndoa kwa yeyote maadam nafsi yake
imempenda au imemlizia sio hilo basi yako mengi vijana wengi uweza kuona ni
ukisasa kwenda kila tamasha hasa ya kidunia uwa ajali kingilio ni kiasi gani!
Maadam mtu ameshapenda…………..anaweza fanya lolote ili mradi tu aweze kupata hela
atakama kuuza mwili wake na hata kudanya wazazi wake au walezi wake.
Jamani huku kupenda
kumekuwa ni janga sasa tunakoelekea watu wengi watapenda kufa!!!
Lakini mwisho wa safari
itadhihirisha njia gani ambayo umetumia katika kufika hapo kwakua kila
unachokipanda lazima utavuna!
ii.kazini
panaitwa ofisini au
mahali pakuwajibika kwa ajili ya kujenga familia yako au maisha yako na
hawapendao mathalani wazazi au wenzio!
Mtu anapokuwa huku
anaona kuwa amewatiwa giza na wote(uhalali usio na matumizi sahihi ya mipaka)
hivyo anaweza fanya lolote ambalo analojisikia pasipo kujali hii ni sawa au si
sawa anaweza fanya jambo lolote anaweza kuanzisha mausiano ya kimapenzi na
wengi akiwa huko ofisini na anaweza bosi wake na mfanyakazi mwenzake sina
unajua tena mazoea ujenga urafiki na hatimae………!
iii.kijamii
hapa ni sehemu
isiyorasmi kwa mtu kufanya kitu chochote mathalani mtu anaweza mwadilifu kazini
lakini mtaani akawa mtu ,mlevi,mkorofi na hata asiye na upendo katika jamii
yake
huku tunaweza sema
mtaani mtu uweza kuwa huru kwenda popote na kufanya chochote anachojisikia
pasipo kujali nini kitatokea katika maisha yake……unaweza kukuta mtu anaweza
kwenda katika bar na kufanya kile ambacho akili yake itachomtuma…..pasipo
kujali jamii inajifunza nini kwake, au anacha msingi gani katika maisha yake au
anaacha malezi gani katika familia yake!
Kuna wengine wanaweza
kwenda kwenye ngoma na wanakuwa huru kufanya chochote au kufanyiwa chochote,
wako wengine wanaenda katika matembezi na huko wanaweza fanyachochote maadamu
akili zimewatuma kufanya hivyo.
Yaliyobebwa katika
ufahamu wako ndio matunda ya matumizi ya uhuru wako!
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson……………………………………………0764 018535
WEWE NI MATUNDA YA MATUMIZI YA
UHURU WAKO!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni