Ijumaa, 29 Mei 2015

HE KNOWS MY TOMORROW



ANAIJUA KESHO YANGU




Hakuna kitu kizuri kama kuwa na KESHO yenye uhakika, yenye matumaini mema yenye furaha ya kudumu, yenye maisha mengine yenye daraja linguine lilibeba jambo jema katika maisha yako.

Hakuna mtu mzuri ambaye unaweza kukaa nawe katika furaha na kujiamini kama mtu anaye ijari kesho yako……..na katika dunia ya sasa watu wengi wana amini kuwa kesho inatengenezwa na leo na hasa wako watu wengine wana amini pia kuwa kesho inakutegemea wewe!

Ni jambo la kawaida kwa mtu anapoona kesho yake itakuwa ni nzuri au imebeba jambo jema kwa  mtu mathalani mfanyakazi uweza kujibidisha sana pindi anapo ahidiwa kitu kizuri ambacho kitaboresha maisha yake…mfano bosi akamwambia mfanyakazi wake akisema kama ukiendelea na moyo huu kufanya bidii katika kazi nitakupa nyumba,gari au mshahara uliobora zaidi.

Na wengine uweza kushusha bidii zao katika kazi pindi anapotambua kesho yake haina mabadiliko chanya au manufaa katika maisha yake, uwa katika kipindi hiki mtu uweza kuacha kazi anayoifanya………..hauwezi kuendele mbele tu wakati ukijua mwisho wa njia yako kuna shimo litakalo hitimisha maisha yako.

Hakuna jambo la maana sana kama kutambua yuko mtu anayeitambua, kuijali na kuithamini kesho yako ni jambo linalo kukupa kushinda hata kabla ujapigana!

Lazima utambue kuwa yuko Mungu anayeipenda kesho yako na kutaka kuwa ya maana zaidi unavyofikiria……….japo wakati mwingine tunaona sisi kuijali kesho yetu kuliko yeye ambaye anairuhusu kesho ije kwa ajili yako.

Ni seme wazi kuwa kesho yako hauwezi kuielewa na kuibeba na hata kuistahimili pasipo Mungu kuweka wazi kwako…….mkulima japo anaamini baada ya kulima katika kufuata kanuni za kilimo chenye tija lakini bado anaweza asiifurahie kesho yake kwani matatizo mengi yanaweza kujitokeza mfano mafuriko na kuondoa mazao shambani na kupeleka mtoni, wakati mwingine unapozalisha vizuri unaweza ukakosa soko la kuuza, hata mkono wa serikali ukashindwa kukutoa pale ulipo kwa kununua yale mazao na hatimae ukabaki na yohayo mazao na hatimae kuoza na kupata hasara baada ya kupata faida,

Hivyo kuanza vizuri sio kuonyesha kutakuwa na ishara nzuri ya kuendelea katika ustawi wake bali vyote vinamtegemea Mungu!

Hivyo ni seme kesho yako uiweke mikononi mwa Mungu haijarishi nini kitatokea baki hapo kwa kua katika yeye hakuna maumivu bali kuimarisha, hakuna kuachwa bali kuna kukumbatiwa, hakuna kutengwa bali sikuzote kuna kukumbukwa ndo mana Mungu anasema mama anaweza kumsahau mtoto anyonyae lakini yeye hawezi kumsahau mtu wake na kamwe hawezi kukusaliti kwa kuwa ndani yake hakuna kisasi.

Wako watu wanaiweka kesho yao katika mali,wenzi na hata ndugu wa wapendao hivyo kuyaweka maisha yao rehani kwakua hao wote wana kesho yao na inaweza kuwa kuwa ni tofauti na kesho yako………..naomba ni kuhakikishie kuwa hakuna mtu anaweza kuitunza kesho yako kwakua kila mtu anahitaka kesho yenye manufaa yaliyo bora na yenye mantiki na katika hali hiyo unaweza kuwa na mtu ambaye mnashindana katika kuitafuta kesho iliyo bora, sio kesho ya maana sana pindi unaweza mkatembea na msichana mwenzako wote mkawa na kiu inayo fanana katika hayo pakawa shida kutoelewana baada ya kusaidiana mkawa mnakandamizana!

Lazima ujue kesho yako nzuri ni fahari ya Mungu!!

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………..0764 018535

ANAIJUA KESHO YAKO MWACHIE AINDAE!!!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni