MAMBO
YA KUZINGATIA KATIKA MAUSIANO YA KIMAPENZI;
Tukiwatunaendelea na
hatua inayofuata katika kuleta mwanga katika fahamu zetu na hatima kuwa na
maamuzi yaliyosahihi ilikuleta mafanikio katika swala zima la mausiano na leo
tuko katika sehemu ya nne, na yote haya ni katika kuhakikisha na fanyika baraka
kwako na kwa jamii yetu kwa ujumla.
II.UTAYARI
WA UCHUMI
Hii hali ya utoshelevu
wa kiuchumi imekuwa janga katika jamii husika, kwani watu wanafikiri uwezo wa
kijimudu katika uchumi imekuwa moja ya sababu katika mtu kuingia katika
mausiano ni kweli kabisa katika mausiano hasa ya kimapenzi swala zima la uchumi
muhimu sana!
Lakini katika jamii
yetu wametumia fedha au uwezo walionao katika kujionyesha umaridadi wao na
kuweza kutumia fedha kwa namna wanavyofikiri pasipo kujua hayo ni matumizi
sahihi au sio sahihi,wako waliowengi wametumia fedha katika kubadilisha
wanawake wakiamini kuwa baada ya kuwa na fedha hivyo msichana yeyote unaweza
kumpata haijarishi yuko katika maadili au sivyo bali ana amini katika nguvu ya
fedha anaweza kubadilisha mazingira yeyote pasipo kujali chochote au hata
athari baada ya kitendo hicho………na mbaya zaidi hivi sasa hata wanawake wamekuwa
wakitumia fedha zao katika kubadilisha wanaume kadili ya jinsi mtu anavyoamua kulingana
na fedha zake au uwezo wake ili kutimiza matakwa ya nafsi yake.
Najua kuwa hakuna kitu
kigumu kama mtu kuishi tofauti na hadhi aliyokuwa nayo kwa sababu kila hadhi
katika dunia ya sasa kila hadhi ina namna ya kuishi japo wako watu wanaishi
vile wanavyoona kunamwelekeo mzuri wa maisha na wako watu wanaishi katika ulimbukeni
na kutumia uwezo wao vibaya tofauti na hali ilivyo au vile inavyotakiwa!
Nipende kusema tu kwamba
uchumi na mausiano HAKUNA muungamaniko
wa moja kwa moja au kutoa fursa wa wewe kuingia katika mausiano kwa sababu
unauchumi wa kutosha japo sichochei kwa mtu yeyote kuingia katika mausiano
ukiwa hauko na mipango thabiti ya uchumi uliyonayo…….kwakua kuna kuwa na uchumi na matumizi ya uchumi!!!.
Niseme kuwa na uchumi
ni haki yako kwakua unahuhitaji katika kuendesha maisha yako ya kila siku
lakini katika upande wa mausiano unahitaji kutambua kwa msaada wa Mungu na
uelewa wako katika kubaini lilojema na lenye mwisho uliojaa matumaini.
Niombe ujue kwamba
mausiano sio maisha japo ni muhimu ila wako watu wanaishi katika maisha yao
kila siku pasipo kuwa na mausiano hayo ya mapenzi wako wametoka katika mausiano
ya kimapenzi kutokana na maumivu waliyo yapata au mateso na ukatiri
waliofanyiwa katika maisha yao……hivyo hawawezi kusahau na hivyo wameamua kuishi
maisha yao wenyewe kama wanavyoona kuwa watapata matumaini na amani katika
mioyo yao.
Kuwa na uchumi mzuri ni
kitu kimoja na kuingia katika mausiano ya kimapenzi kunahitaji wakati wake
haupaswi KUCHANGANYA!
Wakati
ujao……………………!!!
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson…………………………………………….0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni