Ijumaa, 22 Mei 2015

UFANYE WOKOVU KUWA NI KITU BORA



UBORA WA WOKOVU


 Kufanya wokovu kuwa kitu cha kutamanika au kuvutio na chenye maana kuliko chochote hilo ni jukumu lako……..na unaweza kudaiwa endapo tu! utafanya wokovu ukaonekana hauna thamani katika maisha ya mwanadamu, kwa maana ya wokovu wenyewe umepita viwango vyote vya ubora wa dunia na hata wa mbingu.

Mungu ameshamleta mwanae wa pekee ambaye ni yesu kristo kwa ajili ya ulimwengu kama zawadi yenye thamani kubwa kuliko chochote na ili kuwapatia wanadamu nguvu na kuimarika katika yeye.

Ukweli sio kitu chepesi kuonyesha wokovu kuwa ni kitu bora katika mahali ulipo unaposoma,unapofanya kazi na hata unapoishi na majirani zako kwa kuwa watu utaka kuona utofauti uliopo kati yako na mwingine au na yeye……mathalani unaweza kuwa umeajiriwa na bosi ambaye ajui wokovu maana yake nini? Anaweza kukujia na kutaka kuona maana ya wokovu kupitia wewe japo! Anakulipa mshahara kwa maana nyingine anachangia jeuri yako au furaha yako.

Ki ukweli wako watu wanaishi maisha katika wokovu kiasi kwamba marafiki zake au ndugu zake na hata mahali anapofanyia kazi wasione maana ya yeye kwenda kanisani au kujiita au kujitambulisha ameokoka kwakuwa hawaoni tofauti kati yao na yeye  na hivyo kuwa ni  changamoto kwake katika kuwafanya jamii inayo mzunguka katika bidii katika kujua zaidi fahari yake katika imani au mwenendo wake!

Wako watu ambao wamekuwa wakijitenga na watu wasio mwamini Mungu katika imani yao  kama wazazi wake, familia yake kwa ujumla na hata wafanyakazi wenzake na kuona hao watu hawapaswi kuchangamana nae…na akiona kuwa huo ndio ufahari wake wakujitenga na wasio amini!  

Wamekuwa wakiishi maisha hayo na kuona huo ndio wokovu.

Ukweli kwamba wokovu umepewa wewe ili kwanza uwefaida kwako na ukawe faida kwa wengine na hivyo basi kama usipo ona wakovu kuwa wa faida kwako ni wazi hakuna mtu ataona kuwa wokovu ni kitu bora sana kwakua wewe umeanza kuona kuwa sio kitu bora.

Sio furaha ya Mungu kuona wokovu unakuwa kuwa sio kitu bora kwa maana kwake yeye ni kitu bora sana kuliko chochote hivyo anaamini kuwa kitakuwa cha maana sana kwako na katika jamii wanayokuzunguka kwakua katika yeye hakuna kinachoshindikana……japo havifanyiki kwakua umesha mpokea bali namna unamfanya aweze kuwa msaada kwako na kwa wengine.

Lazima ujue kuwa pindi waokovu unapokosa nguvu katika jamii inayokuzunguka tambua kuwa hiyo ndio huzuni ya Mungu kuliko chochote kile ambacho unaweza kuwaza au kufikiria katika njia yeyote.

Ni vizuri ujue kwamba furaha ya Mungu ni kuona wewe unafurahi na hivyo hata furahi kuona wewe binafsi unaona wokovu kama janga au mateso katika maisha yako na ikiwa yeye ameachilia ni kitu chenye ushindi zidi na chenye thamani kubwa kuliko kitu chochote ulimwengu wa sasa na hata wa baadae!

Unaweza kuufanya kuwa wokovu kuwa ni kitu bora sana na wengi waka mfuata Mungu kupitia wewe binafsi kwa namna unavyoenda mbele za Mungu kwa ukamilifu kuliko chochote.

Kuna vitu viwili nataka ni viweke wazi japo kuwa sitavielezea kinagaubaga;

i.baba wa kiroho
huyu ni mtu muhimu sana hakikisha unamsikiliza na kuona kupitia yeye upo vile ulivyo na utakuwa zaidi kwakua katika yeye unamuona Mungu.
Hakikisha unamshirikisha katika jambo jema na hata baya na kuona kile atakachofanya au kukisema katika yote muone kuwa ni baba bora na wa maana sana katika maisha yako.
Popote unapoenda hakikisha moyo wako uko vizuri na yeye japo wakati mwingine yeye kama mwanadamu anaweza akafanya yale yasio upendeza moyo wako lakini katika hali yoyote jua ni baba mpaka pale Mungu atakapo amua jambo jingine katika maisha yako

Ii. Roho mtakatifu
Huyu ni zaidi ya baba wa kiroho na mtu mwingine yeyote kwani nafasi yake hakuna mtu atakaye weza kufanya, Mungu amempa heshima kubwa sana….dhambi zote unaweza kusamehewa lakini sio dhambi ya kumkufuru Roho mtakatifu!! Hapa kuna nini ni jambo la kushangaza sana.

Lakini katika yote msikilize ili akupe dira yako hatua zako furaha yako na maisha yako kwa ujumla wake, na ukimuelewa na kumkubali kamwa hauwezi kuchoka, kupotea na hata kuto timiza ndoto yako.
MWAMINI YEYE UTAKUWA SALAMA!!!
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson………………………………………………. 0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni