Jumatatu, 4 Mei 2015

MAUSIANO SALAMA-5



MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAUSIANO YA KIMAPENZI;


 Tukiwa bado tunaendelea na mfululizo wetu wa MAUSIANO katika ujumla wake, na leo pia tunaendelea katika sehemu ya tano……………hivyo karibu sana rafiki katika kuendelea kupata mwanga katika kuzidi kusonga mbele!

III.UTAYARI WA AKILI

Hapa ni uwanja hatari sana kwakua katika hali ya akili kupevuka na kutaka kujua kila kitu kwa zaidi sana….na siku zote akili uweza kushawishika na mwili na hata katika kuona,kusikia na hatimae ikazalisha kiu ya kutaka kufahamu kitu zaidi ambacho kinaendelea katika jamii husika japo yako mambo mengi yanaendelea katika jamii husika lakini yako mambo ambayo yanashawishi zaidi na kuwa kivutio katika macho na kinachobeba hisia.

Hivi sasa katika jamii husika kuna mambo ambayo ni kivutio kwa watu wazima kwa maana watu wenye rika kubwa zaidi na vijana kama watu wenye rika la wastani na kundi la watoto, na ndani ya jamii yetu katika ulimwengu wa sasa mambo mengi yasiyo ya maana sana yamekuwa yakitawala katika akili ya watu wengi hasa walio na rika 14 mpaka 35 ambao ndio tegemeo katika jamii husika katika kuleta chachu ya maendeleo katika jamii husika.

Watu wengi wamekuwa wakiichosha akili zao katika kutumia mambo ambayio yanaridhisha miili yao na sio jambo lililo na manufaa sana katika maisha yake mathalani kuangalia picha za ngono na kuanagalia staili za kufanya mapenzi na kuziweka katika maisha yao kwa hakika akili zao zimetiwa giza na kuona giza zaidi ya kuona nuru ambayo italeta matumaini katika maisha husika.

Matumizi hayo ni shida kubwa katika maisha yake pamoja na jamii inayomzunguka hawajui kuwa “MISUSE OF MIND”  ni shida kubwa kuliko jambo lolote lile ambalo wanaoliona wenyewe wanaona kuwa ni kwenda sawa na dunia inavyoenda na sio kuangalia mwisho wa safari ya dunia, ukweli hakuna kitu cha maana na chenye thamani kubwa zaidi ya akili lakini namna unavyotumia akili yako ni ishara kubwa kuwa unajipenda au haujipendi kila kitu unachokiangalia kizuri ujue ni matumizi sahihi ya akili lakini sasa tumekuwa tuko tayari kupokea kila kitu tunacholetewa hivyo hatujui kuwa kinamanufaa kwetu au la! Bali kwakua kimetengenezwa na mtu mwenye ngozi nyeupe kila kitu anachokifanya basi sawa.

Akili inapokuwa na upofu uwezi kujua maana ya msemo huu LINALOWEZEKANA LEO LISINGOJE KESHO  msemo huu una maana yake lakini akili yako inavyotiwa giza uwezi kuona maana ya matumizi sahihi ya akili ambayo italeta maana kubwa sana katika maisha yako

Ukweli akili ya mtu ndio dereva wa maisha ya mtu husika akili ikishachafuka tu hakuna la maana linaloweza kuonekana katika maisha ya mtu husika, hivyo unahitaji kuwa makini sana kuliko sehemu yoyote……unahitaji kuona fahari ya akili yako katika matumizi yaliyo sahihi kuliko chochote kwa maana hakuna fahari ambayo itaipita fahari ya akili uliyonayo kwa maana ni jambo la maana sana kwa mtu kujivunia akili yake katika MUNGU.

Pasipo mashaka tukutane wakati ujao…………………!!!

Imeandaliwa na;
Cothey Nelson……………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni