Ijumaa, 24 Aprili 2015

MAUSIANO SALAMA-2



MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAUSIANO YA KIMAPENZI;


Karibu tena katika nafasi ya pili tukiendelea kuhusu swala zima la MAUSIANO, kwakua limekuwa janga na changamoto kubwa katika jamii tuliyonayo kwa kiasi kikubwa na kuzaa matokeo ambayo yameleta muonekano wa pande mbili yaaani POSITIVE SIDE au NEGATIVE SIDE,yote juu ya yote bado tunaona ni matokeo ya yanayotekea katika dunia.

Katika kuendelea na maswali ili kupata hali uelewa wetu hivi kweli unaweza kujishawishi au kushawishika na hata kushawishiwa katika kuingia katika mausiano……….wakati mwingine watu ufurahia au huzunika na wengine walisema kwamba hawakuwa katika utayari wakuingia katika hayo mausiano lakini kutokana na kushindwa kuimiri katika nguvu ya ushawishi kutoka katika upande mwingine wamejikuta wameingia pasipo hiyari yao wenyewe!

Hivyo kutokana na dhana hiyo wako watu wanaojilaumu wenyewe kwa kukubali kushawishika na wako watu wanawalaumu watu ambao waliwashawishi na kufikia katika hali walio kuwa nayo, na wakati mwingine watu wanapoanza uhusiano wao wanakuwa na furaha kubwa pasipo mashaka yoyote na wala kutojua kama ipo siku ambayo watachukizana na kuwa kama maadui wakubwa ambao kama hawajawai kuwepo katika dunia.

Ni kweli matokeo yanapokuwa mabaya katika mapenzi ya wahusika basi kinachofuata hapo ni uhasama wa kudumu na ni watu wa chache tu ambao wanaachana na bado wakaendelea kuusiana kama marafiki katika mausiano mengine mbali na uhusiano uliokuwako hapo awali……na wapo ambao wanadumu katika hili na wako ambao wanashindwa kuimiri kuwa mbali na baadaye kuamua kurudiana tena!

Na amini kabisa yako maumivu makali sana kati ya watu wawili waliopendana sana na baadae kutengana pamoja na hayo yote hayo maumivu hayamshindi YESU alipokuwa msalabani akibeba dhambi za dunia na kututoa mateka katika ufalme wa giza.

MAMBO YA MSINGI KATIKA KUYAJUA KABLA KUCHUKUA MAAMUZI SAHIHI YA KIMAPENZI

I.UTAYARI WA KIMWILI
   
  II.UTAYARI WA KIUCHUMI
                                                   
                                                       III.UTAYARI WA AKILI
            
     IV.KIBALI KATIKA MOYO WAKO
                                                    
                                                     V.KIBALI CHA MUNGU

Haya ni mambo matano ambayo nitaenda kuyanyambua ilikuleta mwanga zaidi katika maamuzi yako na kuleta ujasiri katika maamuzi yako! Na kuwa msaada kwako au katika rafiki zako unaowapenda.

Imeandaliwa na;

Cothey  Nelson……………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni