MAUMIVU
YAKE NDIO FURAHA YANGU;
Sio kibinadamu wala
alipendezi katika uso wa mwanadamu yeyote…..maumivu ya mtu yawe furaha kwa mtu
mwingine na hicho ndicho kinachotutofautisha kati ya mwanadamu na Mungu kwa
mateso na dhihaka yake ili sisi tuwe watoshelevu ulio na usalama wa mwilini na
rohoni.
Isipokuwa kwa mzazi
mwenye mapenzi mema na familia yake yuko radhi mateso yake yawe na tija katika
familia yake tu japo sio siku zote……..na hii ni tofauti kubwa kati ya mwanadamu
na Mungu ambaye alikuja kwa ajili ya wote waliompenda na waliomchukia kwa kujua
au kuto kujua…..lakini yeye aliwajali wote na alikubali dhihaka yake iwe na
tija katika wanadamu wote pasipo kujali rangi, muonekano au uwezo wa uchumi wa
mtu husika.
Tunaona watu wakijitoa
mwanga na kujiua kwa njia mbalimbali lengo likiwa katika kufanya ibada yao kwa
Mungu wao na kile wanachokiamini pamoja na kuleta ustawi mzuri katika familia
zao….kwakua zinakua ni ahadi kwa wale wanawatuma.
Lakini yesu alikubali
kupata maumivu kwa furaha pasipo kinyongo na kujua kile anachokifanya kinaleta
faida katika dunia nzima……na hapo ndipo ilipo furaha yangu na majivuno yangu na
kuwa jasiri sana kwakua yupo aliniye nigharimia na kuniweka katika nafasi yake
tena katika hali ya upendo uliopitiliza.
Maumivu yake yamenipa
mwanga maisha yangu ya sasa na hata ya baadae kwakua toni ya damu yake ina
maanisha maana kubwa katika maisha yangu kwakua ni udhihirisho wa kumleta Mungu katika maisha yangu katika
kunifanya kuwa niwe wake katika maisha ya umilele.
Maumivu yake
yalimaanisha kitu kikubwa katika maisha yangu……….upendo usioweza kujibiwa aliona bora na kuwa tayari kutekeza maisha
yake kwa ajili yangu nimeona huu upendo ambao sitakaa nione wala kupata katika
maisha yangu yote, kwani kila binadamu anaweza akakupenda lakini bado akaweka
kuna sehemu ya mashaka na wewe au hali ya tahadhari kwa lolote litakapotokea
yeye anakuwa salama.
Yohana
15:13
“hakuna
aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki
zake.”
Kiukweli kupitia
maumivu yake leo kunanifanya nione dunia kwana namna nyingine kuona naweza
kufanya jambo la maana likawa jambo jema katika maisha yangu na mbele ya uweza
wake, kwakua bila yeye ingekuwa ngumu ya mimi kujitambua na kuweza kusimama
katika maisha yangu pasipo kuwa na shaka yoyote.
Nguvu yangu katika
dunia hii inatokana na maumivu yake niko
salama sana dhidi ya nguvu za giza kwa sababu ya yeye yuko nami na kama akipo
cha kumshinda yeye basi hakuna kitakacho nishinda!
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson……………………………………0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni