Ijumaa, 10 Aprili 2015

NJIA YANGU



HAKUNA KITU KISICHO NA MWISHO;




Laiti tungekuwa tunaona mwisho kabla ya mwanzo tungekuwa watu wengine sana ila kwasababu hatujui mwisho ndo mana tunajiachia mwanzo!

Binadamu yeyoyote anaposikia kauli hii bila shaka anakuwa na hali ya KUJITATHIMINI… ili kuona yuko sahihi kwa Mungu na kwa wanadamu, na kama katika pande zote hakuna mwelekeo mzuri basi mwenye akili uweza kufikiri namna ya kuitimisha katika mwisho ulio bora unaotoa mwanga wa milele ulio na matumani mema.

Mbali na neno la Mungu hakuna kisicho na mwanzo au mwisho bali vyote vina mwisho haijalishi ni kizuri kiasi gani au kibaya kiasi gani? Bali ilimradi kina mwanzo basi pasipo mashaka mwisho wake upo…..ni Mungu pekee yeye hana mwanzo wala mwisho!

Wako watu upenda kuonekana kuwa wako juu wakati wowote, hivyo ufanya kila haina ya udhalimu kuwa hakikisha heshima yake na hadhi inabaki palepale lakini pamoja na hayo yote jua kuna MWISHO ambao haujui na endapo utakukuta na sijui utakuwa wapi au utakua na hali gani na utakuwa unahatima gani?

Na endapo utaishi maisha haya bila shaka utakuwa na maisha yenye mwelekeo unaoeleweka wenye kukupa nafasi nzuri ya wakati ujao………lakini jambo hili sio rahisi kulitambua na kulipa uthamani katika moyo na utendaji wako.

Binadamu wengi wanaishi maisha ambayo wanasema lolote na liwe maana ndicho nilichokiamua na ndicho nitakachokifanya kwa moyo wangu wote na hakuna kile cha kunitenga tena na maamuzi haya niliyoamua….pasipo kujali nini hasa matokeo katika jamii inayokuzunguka na taifa lako kwa ujumla.

Wako watu waliojiingiza katika maisha hatarisho kama ujambazi na hata ukahaba ukiwauliza watakwambia maisha yamechangia ya mimi kuwa vile nilivyo wala haya maisha sio chaguo langu sikuwai kuota ndoto wala kufikiria nitakuwa na maisha haya…..mimi sisemi uache wala kuendelea lakini nipo hapa kukukumbusha kuwa HAKUNA KISICHO NA MWISHO, na sio kuwa na mwisho tu bali huo mwisho utatoa mustakali gani katika maisha yako yaliyobaki!

Katika maisha ya ukahaba yako madhara mengi yanaweza kukupata na ukajuta kwanini niliingia katika uchaguzi wa maisha ya namna hii tukianza upande wako binafsi afya yako inaweza kuathirika katika kiwango kikubwa sana hata ukajuta kwa nini nimezaliwa kwani magonjwa yatashamiri katika mwili wako mathalani ukimwi na magonjwa mengi ya zinaa…na kupelekea mwisho ukawa wa simanzi badala ya furaha na shangwe kwako,familia yako na kwa jamii kwa ujumla na pia unapojihusisha na mambo haya basi hata jamii itakupa picha ambayo italeta simanzi katika maisha yako na mbaya zaidi utajuta namna ulivyotumia vibaya wakati wako.

Unaweza sema fedha haitaisha kwakua endapo itakapoisha basi nitaenda kutafuta nitapata tu! lakini lazima utambue ili fedha iwepo lazima pawepo na chanzo na endapo chanzo….na hikitokea hicho chanzo kikifungwa basi ni wazi ustawi wako utakuwa umefikia kikomo………na najua kabisa kuwa fedha ndio shina la maovu mengi na endapo kutakuwa na na mbadala wa fedha basi pangekuwa na unafuu mkubwa sana japo sangine watu wangekuwa wavivu au chenyenguvu kingetawala kile kisichokuwana nguvu.

►Ni Mungu pekee yeye ana mwisho wala mwanzo na wala ajui nini maana ya kuishiwa kwakua vyanzo vyake havina mwisho na wala hakuna uwezo wowote unauwezo wa kuharibu chanzo mbacho Mungu anakiambata.

Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni