FAHARI YA KIJANA,
Ninapozungumzia neno FAHARI
uwanazungumzia kitu au hali hama namna
inayokufanya ujivune,ujisikie bora au ujione unastahili. Na katika hili
kuna ushindani mkubwa katika vijana wa pande mbili na wengi wao wakitumia
vibaya wakati wake(misuse of time) na wengine kati yao wanautumia wakati wao
vibaya wanautumia huku wakilia na wengine wakicheka! Lakini yote tunaona ni
maisha na siku zinaenda na hatimae kuishia.
Katika hili naomba
niseme wazi tu……….kunafahari ya kijana katika mtazamo wa kidunia na mtazamo wa
kimbingu(Mungu) na hapa pamekuwa na mvutano usio kuwa wa kawaida kwani hata
waliokuwa nuruni wamekuwa wakijifunza mambo yanaendelea gizani eti wakisema
yako mengine ni mazuri yanayofaa kuigwa, lakini cha ajabu waliogizani
hawajifunzi mambo yaliyo nuruni zaidi ya uigizaji (kutokua na uhalisia).
Wako vijana ambao
wanaamini kuitumikia DUNIA hapo ndipo kunakuwa na fahari ya ujana kwenda sawa
na dunia inavyoenda kuutendea haki basi ndipo ilipo fahari ya kijana na wenyewe
wanaona wako sahihi sana kuliko walio kinyume chao STAREHE katika matumizi
mabaya ya miili yao na matumizi ya fedha isiyofaa na kwa mtu mtumiaji anaweza
kuona yuko sawa lakini wengine walio nyuma yao WANALIA na KUSIKITIKA kwa nini
ndugu huyu kafikia hatua hii.
Na lipo kundi la
wachache linatambua ufahari wa ujana wao kumtumikia Mungu kama ishara ya
kumshukuru Mungu kwa kuruhusu atokee dunia na hata kumlinda na hata kufikia
mahali alipo sasa hivyo anavyojitazama nakuona kule alikotoka na kumuona Mungu
zaidi ya kuona jambo lolote katika maisha yake hivyo anavyojitazama anaona
hakuna namna ya kumshukuru Mungu zaidi ya kutoa maisha yake yawe ya Mungu tu
siku zote za maisha yake! Hakika ni
kundi jema.
Katika pande mbili hizi
za vijana kila mtu anakwambia yuko hapo au anafanya hayo akiwa na sababu za
kutosha sana ambazo wakati mwingine ukimsikiliza vibaya unaweza kusema hata mimi
ningekuwa ni yeye basi nami ningeingia kule huyu alipo, laweza kuwa katika
ufahari wa dunia au mbingu!
Usishangae kijana
anaweza kukaa katika baa,mitaa usiku wa manane wakati wote pamoja na yale yanayofanyika katika baa mathalani
biashara haramu kama madawa ya kulevya au kuuza miili yao ndo mana nimesema
wako watu wanaoutumia fahari ya ujana wao wakiwa wanalia na wengine wanacheka!
Cha ajabu sana unaweza
kuwa kuta vijana walianza kumtumikia Mungu kama fahari yao lakini sasa wako
kuitumikia dunia kama wakiona hiyo ndiyo fahari yao……hii ni mbaya sana japo
hali inatokea na inawatoa machozi watu wengi……kwakua mtu huyo kurudi katika
kumtumikia Mungu sio jambo rahisi maana alishaona fahari ya Mungu na sasa yuko
gizani na akishaingia huko ujikita uko siku zote, hii ni mbaya kwani huzuni ya
Mungu inafanyika furaha kwa ulimwengu wa giza.
Ningependa utambue kama
kijana mwezangu mimi sina tatizo na matumizi ya ujana bali nina huzuni na
hatima yale unayo yafanya…..laiti ungepata neema yakujua hatima ya yale
unayofanya na amini usingeweza kwendelea….kwa mtu mwenye akili awezi weka bidii
kufanya kazi uku akijua jua mwisho wa siku hakuna anachokipata!
►Fahari
ya DUNIA ina mwisho kwakua dunia itaondoka na fahari yake pale itakapo fika
mwisho wake kwakua ilikuwa na mwanzo basi bila shaka kutakuwa na mwisho lakini
fahari ya MUNGU kamwe haina mwisho kwakua haina mwisho wala mwanzo hakika hili
ni fungu ni jema!
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson…………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni