Jumanne, 31 Machi 2015

UPOFU WA AKILI



UPOFU WA AKILI



Tunakubaliana sote kwa pamoja kuwa tofauti kubwa ya mwanadamu na mwanadamu na tofauti ya tofauti ya mwanadamu na wanyama sio Akili tu bali matumizi ya AKILI, hivyo hapa kuna vitu viwili kuwa na akili na matumizi ya akili na pia katika matumizi ya akili kuna matumizi sahihi na matumizi yasiyosahihi….matumizi ya akili yanazalisha majina kama haya mjanja,mjinga,mzembe,mvivu,goigoi,mwelevu na hata kuitwa usiyejitambua.

Naamini katika maneno makali ambayo binadamu apendwi kuambiwa ni neno kuwa HUNA AKILI hii ni lugha yenye ukali yanayoathiri mfumo mzima wa maisha ya mtu katika mwenendo wake mzima.japo wako watu wanakataa kuambiwa kuwa wanamatumizi mabaya ya akili zao au kwa lugha rahisi anaitwa mjinga ambalo ni neno lilojaa mauzi kebei na kwa hakika alivutii katika masikioni mwa mtu.

Ninapozungumzia upofu wa akili sina maana kuwa akili iliyokosa mwelekeo au akili iliyokosa njia sahihi yanamna kutatua majukumu yanayo mzunguka,…………..bali hali ya kujua uaribifu wa maisha yako na kwenda katika njia hiyo pasipo kujali kitakachotokea, mtu wa namna hii ataashauriwe na mtu wa namna gani? Bali ushikilia kile alichokiamua/alichokiamini mathalani kuwa katika maamuzi ya kuchukua kuingia katika UJAMBAZI,UCHAWI na hata UKAHABA, mtu wa namna hii sio kitu rahisi kumtoa mtu katika maazimio yake hayo labda mpaka aone madhara yake na anaweza kuona anahitaji msaada na asiupate huo msaada kwani jamii inawakata au inawanyanyapaa na hata kuwatenga kuishi na watu hawa katika hali ya kujiami.

Sikatai wako watu wanajiingiza katika mfumo huo usio rasmi wakiwa na mawazo tofauti wako watu watasema mimi nitafanya kwa muda tu alafu nitaacha na pindi atakapoacha anaamini atakuwa anaweza kujishughulisha katika shughuli nyingine ambayo itampatia kipato katika kuendesha maisha yake….lakini katika mawazo hayo ni wachache sana wanao uwezo kuyatimiza hayo mawzo…zaidi sana wanachokiongea sio kile wanachokifanya inawezekana katika ushawishi binafsi au ushawishi wa wenzao.

Naamini kama akili yako ikiwa njema haiwezekani tu ukaingia katika mfumo huo ambao utahatarisha maisha yako na niseme wazi maamuzi ya jinsi hii aichagui MSOMI au ASIYESOMA  au MASIKINI au TAJIRI wote akili zao zinaweza patwa na upofu wakafanya mambo ambayo yakaongeza giza katika maisha yao badala ya kuongeza nuru….ni wazi kuwa kazi hii hauwezi fanya milele ila sio rahisi kutimiza lile lengo ambalo umelipanga kuwa nitatimiza.

Watu wanaofanya shughuli hizi wengi wanasema wafanya hili sio kwa kupenda bali kunashinikizo ambalo linamsukumo katika kuyafikia maamuzi hayo inawezakuwa maisha, msuko wa mwili wake na hata  katika mtazamo wake au ushawishi watu……….tunaamini kunashughuli nzito kamaukiingia sio rahisi sana kutoka huko mathalani mtumiaji madawa ya kulevya na msambazaji wa madawa ya kulevya anaweza asitoke kutokana na manufaa anayo yapata au kutokana na kuathirika katika mwili wake.

Japo ziko taasisi zilizoazishwa katika kuwasaidia jamii kuondoka na tatizo hili lakini tatizo limekuwa likupungua tu lakini ukweli tatizo limeendelea kuwepo wakati wote na jamii imekuwa ikizidi kuathirika na janga hili pasipo kujua nini cha kufanya.

 Ushauri wangu kwa watu wa jinsi hii……kwanza nitoe shukrani zangu kwa kila taasisi ambazo kiukweli zimejitolea kuhakikisha jamii inaondokana na janga hili na kuwa jamii isiyo na watu wenye akili zilizotiwa giza ambazo kwa muonekano zimekosa njia sahihi, zimekosa mwelekeo na hata kukosa kuthamini kesho yao………lakini kubwa katika yote Mungu anaweza kuyafanya yale ambayo kwa uhalisi yalikuwa ni magumu sana kama mzazi au mlezi na hata ndugu mwamini yesu katika maisha yako awe dira katika maisha yako yote na yeye ataleta nuru kwa wale waliofikia hatima mbaya ambayo jamii haiwaelewi tena……na kwa mtu aliyeathirika katika utendaji niseme sana wewe ni mtu wa maana sana kwani katika biblia yesu aliwapenda waliokataliwa na jamii husika  mathalani wenye ukoma, makahaba na hata watoza ushuru Mungu ni zaidi ya baba anayejua kulea,kujali na kukupa kile kitu ambacho hakuna mtu anaweza kukupa mkabidhi yesu maisha yako na kuamua kwenda kanisani kwa waliokoka na kufundisha neno sahihi la Mungu!

Imeandaliwa na;
Cothey  Nelson………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni