UZURI
USIO HARIBIKA
Uzuri ni kitu au jambo
au ni hali? Yote haya ni maswali ambayo mtu anajiuliza pindi anaposikia neno
hili……..wako wanazuoni na wataalamu mbalimbali wanajaribu kutoa maana ya neno
hili UZURI wengine wa kimaanisha ubora au hali ya kung’aa au hali ya
kustahimili au kushamiri katika yote… haya bado kuna maswali ya watu na utofauti
wao katika kunyambua hili neno………na sijui wewe msomaji wangu pindi unaposikia
neno hili sijui akili yako inapata picha gani? Au dhana ipi lakini yote
nakuachia wewe!
Ki kawaida hili ni neno
zuri ambalo pindi unapolisikia mtu anakwambia basi moyo wako unakuwa na
changamko la furaha mathalani mtu akikwambia wewe ni mzuri au umefanya jambo
Fulani ukaambiwa umefanya vizuri! Ni wazi moyo wako utajawa na furaha sana….na
sijajua neno hili mzuri uambiwa wanawake tu au hata wanaume na kama wanaume
wanaambiwa katika muktaza upi au kwa dhana iliyo sawa na mwanamke katika
muonekano ulio bora na wenye kung’aa.
Ni wazi kila mtu
anapojitazama ujiona kuwa yeye ni mzuri japo naamini kuna watu wakijiangalia
kwenye kioo wanaweza kusema wao ni wabaya inawezekana kwakukosa maboresho au
vile anavyojiona au vile alivyoambiwa, na amini hata Yule mwenye kujiona sio
mzuri sana huwa apendi kuambiwa kuwa yeye ni mbaya……..vilevile kwa mtu asiyejitambua
kunakipindi anaweza kuambiwa yeye ni mzuri akakubaliana na hali hiyo kwa
asilimia zote na pia kunakipindi anaweza kuambiwa kuwa yeye ni mbaya bado
akakubaliana na hali hiyo kwakuamini kuwa mwanzo alikuwa mzuri na sasa amekuwa
mbaya akakubaliana kuwa kuna mabadiliko.
Pia katika haya yote
tukumbuke kuwa kuna uzuri wa ndani na uzuri wa nje yaani upo uzuri usio onekana
na uzuri unaoonekana, lakini ningependa sana kuuzungumzia uzuri usio onekana
kama ndio matokeo ya kunawirisha uzuri unaonekana, na ni wazi unapo ujali uzuri
wa ndani basi uzuri wa nje utakuwa unaujali sana japo inawezekana kwa kujua
hama kutokujua.
Na uzuri wa Mungu
unanawilishwa na ufalme wa Mungu ukaao ndani yako katika kufanya maboresho na
ushamiri wa makazi ya ki Mungu katika himaya yako ya ndani katika kutoa
muungozo wa uzuri wako wa nje, kwakusema hivyo uwa si maanishi watu wa
sijigharamie katika mapambo yao ya nje ila fanya yote kuustawi wa muonekano
wako kuwa vyema.
Ila niseme kitu kuwa
muonekano wako wa nje utegemea sana na muonekano wako wa ndani kwakua tunaona
watu mambo yanapo wachanganya hata muonekano wa nje ubadilika kabisa na hali ya
kutojijali uanzia hapo.
Lakini ukiutunza uzuri
wako wa ndani kwa kuhakikisha maamuzi yako yote yanamleta Mungu kuzidi
kujengeka katika utu wa ndani bila shaka Mungu atawezesha kuyamudu mazingira
yote ya nje yasiweze kuharibu uzuri wa ndani na wanje.
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson……………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni