JIFUNZE
KUSAHAU na sio kupotezea!
KUSAHAU NI ZAIDI YA KUSAMEHE
Uwa hakuna ulazima wa kujifunza kitu ambacho sio
kigumu au kinaeleweka kwa wote au kwa urahisi pasipo usaidizi wa mtu
mwingine,na ni wazi pindi unapojifunza kitu uwa kinakuwa sio kigumu tena…….mathalani
mtu anayejifunza kuendesha inawezekana hapo awali aliona kuwa ni kitu kigumu
sana japo nae alikuwa anatamani ndani yake lakini baada ya kujifunza uweza
kuona uwezekano wa kujua zaidi na mwisho uona kuwa ni kawaida sana.
Hili ni jambo ambalo watu wengi utamani kuwa nalo,
japo naamini yapo ambayo binadamu yeyote ambayo apendi kuyasahau na yapo ambayo
uweza kuyasahau……….lakini twende mbele na kurudi nyuma tambua kusahau kutokana
na uwezo wa ubongo mtu husika sio kitu rahisi labda awe na shida katika ubongo
wa mtu husika.
Ningependa kusema kuwa kusahau ni chanzo kimoja wapo
katika kufanya mambo kiufanisi zaidi na uwanja mzuri katika kujenga kitu chema
katika akili yako(ubongo) wako watu wanapita katika kipindi kigumu sana kwa
sababu hawataki kusahau bali utaka kubaki katika kumbukumbu katika ufahamu wao
na ni wazi inakuwa teso baada ya kuwa Baraka………..ninge penda ujue kwamba yako
mambo ukiyakumbuka au kusahau hayaletishida katika akili yako ila yako mambo
ambayo pindi unapoyakumbuka yana haribu hata utendaji wako wa kazi na kufanya
kazi kuwa ngumu hata kama ilikuwa nyepesi.
Kulia kila siku hii ni ishara kubwa sana ya mtu
kutotaka kusahau au kutoona umuhimu wa kusahau au kutojua kwanini nisahau,
siwezi kukataa baadhi ya matendo yaliyo athiri yanaweza baki katika mwili wako
na kuweka alama ambayo kila ukiyakumbuka yanarudisha nyuma kukupeleka katika
lile tukio ambalo likasababisha jambo hilo litokee….na jua katika mazingira
haya kusahau inakuwa ni ngumu tu kwani ukiangalia yale uliyokuwa ukiyafanya hauwezi
kuyafanya tena mathalani ulemavu.
Wako waliofanikiwa katika maisha yao kwa kukubali
kusahau na kujikubali na hali waliyonayo na kuanza kufanya jambo ambalo mwisho
wake likawa Baraka katika maisha yao, kwa mtu huyu ana fikiria katika yale
yanayomkabili kuliko yale yaliyomkabili………..najua kuna wakati unaweza kupitia
jambo ambalo kwa kiasi kikubwa likachanganya akili yako kwa kiasi kikubwa sana
lakini ujajua hatima yako inaweza kuwa kubwa kuliko ilo jambo linalo kukabili
au lililo kukabili.
Lazima utambue ikiwa kweli unamtumikia Mungu na wala
ndani yako hakuna unafiki jua mazingira ,teso shida na hata hadha sio Mungu
japo yeye anaweza kuyaruhusu kufanya jambo likawa Baraka katika maisha yako
kuliko vile unavyofikiria.
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson…………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni