Jumapili, 4 Januari 2015

MTEMBEO WA KIMUNGU




MTEMBEO WA KIMUNGU;





Kila mtu ujisikia fahari sana pindi anapotembea na mtu maalufu au mwenyesifa njema katika jamii husika au katika eneo Fulani mathalani kazini,shuleni. Lakini pamoja na kutembea nae anaweza kuwa msaada kwa kitambo tu alafu hali yako ya mwanzo ikajirudia kama hapo awali.lakini uko mtembeo wa Kimungu ambao mtu anatembea kupitia hiyo au mamlaka ya kimbingu ndani yake.

Mtembeo wa kiMungu huu unadhihirishwa na mtu husika angali akitembea hapa duniani watu wanamuona ni Mungu anatembea kwa namna isiyo ya kawaida.tatizo linakuja pale ili mweze kutembea na Mungu lazima mkubaliane na kushirikiana katika kila kona inayokuhusu ili kupata kibali chake.


MTEMBEO  WA  KIMUNGU  UNAONEKANA  KWA  MTU  WA  NAMNA  GANI!

Sio kila mtu anayeshika biblia basi anaweza kutembea mtembeo wa KiMungu au anajulikana sana mtaani basi anaweza kuonyesha mtembeo wa KiMungu, kutumiwa na Mungu na mtembeo na Mungu ni vitu viwili vilivyotofauti kabisa na kama watu wanakuwa hawawezi kukabiliana kwa namna yeyote kwani hapo kila mtu anamwelekeo wake.

Mtu ambaye anayetembea katika mtembeo na Mungu huyu anakuwa ni zaidi ya hatari kwa anaweza kusababisha mapinduzi yasiyo zuilika kwa kua alienaye yeye azuiliki kwa chochote kwakua amejikamilisha na kujitosheleza.

Mtu ambaye anatembea katika mtembeo wa KiMungu huyu ni mtu ambaye akili yake imekufa na mwili wake umepoteza utawala wake na hisia zake pamoja na hofu za kibinadamu zimepoteza nafasi katika maisha ya mtu huyu, anakuwa ni mtu ambaye yuko tayari kujitoa kwa ajili ya chochote pasipo kuangalia gharama zipi atakazoingia baada ya tukio hilo.

Huyu ni mtu ajali anakokwenda anaamini anakokwenda yuko tayari kukabiliana na jambo lolote ili mradi tu lile alilokusudia linafanyika kwa ubora wake na kiufasaha au kwa muonekano wa kawaida anaonekana kanakwamba ajali ya maisha yake bali ni kile kilichomzidi kinachomlevya.

Huyu ni mtu ambaye apatiusaidizi wa dunia( elimu, heshima yake na msaada wake) bali atapingu iko nyuma yake katika kuyafanikisha yale yote yaliyo kusudiwa kwa nguvu na msaada wa mbingu.

Nguvu ya mtu huyu inasimama yenyewe na inafanya kwa ubora wa hali ya juu sana kwani hakuna kitu kingine kinachoweza kupingana na nguvu hiyo asili ya nguvu hiyo haina hali ya kushindwa imeshikiliwa na mbingu na tayari kwa ushindi na sio kwa kushindwa.

Mtu huyu amebeba dhamana ya mbingu ambayo inamshikilia pasipo kuchoka wala kumuacha kwakua yeye ndio makao ya hiyo mbingu yohana 14: 23

Hauhitaji kumsiliza ili uamini bali muonekano wake tu utaona mbingu inashuka na kumfunika........na inadhihirika sana katika utendaji wake kwakua ni Mbingu itakuwa ikitembea badala yake.



Imeandaliwa na;
            

                    Cothey Nelson...................................................................0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni