Alhamisi, 1 Januari 2015

UPENDO WA MASHAKA




UPENDO WA MASHAKA;




Kila mtu ujisikia huru na vizuri sana pindi anapotambua wako watu ambao wana mpenda lakini hali hiyo utoweka pindi anaposikia uhalakini wa upendo wake juu yake, hivyo baada ya kujiachia anaanza kuishi kwa tahadhari sana na sio kujiamini tena, katika hali hii mtu uona ni bora asiwe na mtu ambaye anayempenda kuliko kuwa na upendo usio na muafaka mzuri katika maisha yao.

Watu wengi wamekuwa wakiishi kwa tahadhari sana hasa katika ulimwengu wa sasa binti anamashaka na upendo wa baba yake, mvulana anamashaka na upendo wa mama yake hata kaka na dada wamekuwa wakiishi katika wasiwasi, na chimbuko hili linatokana na baada ya kutendwa au habari ya kusikia kwa watu ambayo inakupa hofu katika mausiano yoyote.

Upendo huu wa mashaka uwa upo katika sehemu zote katika urafiki na hata katika uchumba watu wamekuwa wakiishi kwa tahadhari sana katika maisha yao wako watu waliotendwa na marafiki zao mathalani binti kumwambia mchumba wake rafiki yake na baadae kusalitiwa na hata kwa wavulana katika kuambiana au kutambulishana mchumba wake unakuta watu wanasalitiana.

Sio katika hili tu hata katika shughuli mbalimbali watu waliaminiana katika shughuli Fulani mathalani muuza duka kumwibia boss wake au watu kudhulumiana fedha zao kutokana na utofauti uliopo katika maslai binafsi. Watu wengi wamekuwa wakishilikiana katika hali ya mashaka mpaka waaminiane inachukua muda mrefu sana lakini ni ngumu kuendelea kumwamini.

Katika dunia ya sasa watu wamekuwa wakiishi katika hali ya kutofurahi na kujiamini utafikiri watu wanafanya kazi za madawa ya kurevya katika hali siri na kutokuaminiana kwa hofu kubwa.
Ukweli dunia ya sasa kuwa na mtu katika upendo usio na wasiwasi ni ngumu sana ki ukweli kunavita kubwa sana katika kutambua yupi ni sahihi na yupi si sahihi!

Unaweza ukampata rafiki ambaye anaweza kuwa si urafiki wa mashaka kwanza lazima ujue jambo la kwanza na la muhimu sana WEKA UPENDO WAKO KWA MUNGU;

Hili ndilo kila kitu kwako unapo mpenda Mungu bila shaka Mungu atakupenda na hata kupa marafiki ambaye yuko sahihi ambaye atafanyika Baraka na amani katika maisha yako, na rafiki sio lazima akupe hela wala chochote bali ni vile alivyokupa nafasi ndani ya moyo na namna anavyokuelewa.

Lazima ujue kuwa hakuna wa maana sana kama URAFIKI NA MUNGU kwani ndilo jibu sahihi katika maisha yako. Ishi na Mungu katika maisha yako yote hakika utakuwa salama sana, na kila jambo.

Usichukue hasira ya haraka wala usiwe mtu ambaye unamawazo mabaya bali zaidi sana muelewe mtu kwa msaada wa Mungu, maana ni Mungu pekee ndiye anajua wewe unahitaji nini? Na atakuwa Baraka katika maisha yako.

Kingine lazima utambue kuwa ustawi wa maisha yako ni bora kuliko mtu yeyote kwakua ustawi wako umebebwa na Mungu na sio kitu kingine............yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana.



Imeandaliwa na;
     

                  Cothey Nelson......................................................0764018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni