KUNA TOFAUTI KUBWA KATI YA MSUKUMO WA NDOA
(
MIEMKO YA MWILI) NA NDOA YENYEWE!!!
Ni kweli jambo lolote ambalo unaliingia ni wazi
kabisa lazima uone haja ya jambo hilo na endapo hutaona haja ya jambo hilo ni
wazi hautaitendea haki hali yako na nafsi yako binafsi. Ni kweli ndoa ni jambo
la heri sana lakini ni pale tu utatambua kwa usahihi uku ukisaidiwa na Mungu
mwenyewe katika kukuwezesha kuyafikia yale uliyo yakusudia.
Katika dunia ya sasa ndoa nyingi zimekuwa ni safari
au mapitio tu lakini sio maisha ya wawili hao ya milele, tumekuwa tukishuhudia
harusi kubwa lakini mwisho tukiona upweke ukiendelea kuthibitika au watu
wakiama kutoka kwa mtu mmoja na kwenda kuanzisha ndoa na mtu mwingine, watu
wengi wamekuwa wakiishi katika ndoa kwa misingi mfumo wanaojua wao mathalani
mfumo dume, mila na desturi.
Vijana wengi wanaona kuwa sio rahisi kuishi pasipo
kuwa na mwenzi ili kuweza kupunguza makali ya mwili au kwenda sawa na miemko ya
mwili inafika kipindi ambacho watu hawaaminiani wala kukubaliana kuwa kunauwezo
wa kuvimudu vishindo vya mwili katika mabadiliko yao. Wako watu katika
kupunguza miemko yako katika mwili katika kwenda kwa dada poa( changudoa) na
wengine kutokana na kuogopa maradhi mbalimbali wamekuwa wakishaurina kuwa basi
waoe ili waweze kumudu miemko yao katika miili yao.
Niseme wazi miemko katika mwili ni muhimu sana japo
sio kigezo cha wewe kuingia katika ndao ningependa kusema kuwa miemko katika
mwili wako ni ishara tu mwili wako kujiweka sawa kutokana na hatua uliyonayo
kwani kuna hatua ya watoto kuna kuota meno na mengine mengi lakini kuna hatua
ujana katika kuimalika na homoni kujipanga katika hali stahiki ni kitu kizuri
sana hivyo napenda sana kusema miemko ni maandali yaliyo katika mwili na sio
kigezo cha maandalizi ya ndoa, maandalizi ya ndoa yana husisha maandalizi ya
AKILI na UCHUMI na sio mabadiliko ya mwili.
Tumeona ndoa nyingi za watoto wakiingia katika ndoa
pasipo kujua wapo katika ndoa bali msukumo wao mkubwa unategemea sana msukumo
wa mwili katika kuingia katika ndoa, niseme wazi ndoa ni zaidi ya adhabu ya
kihama endapo hauta ielewa au hautua kubali kuelewa inaweza kuwa ni zaidi ya
majanga lakini ukiingia katika hali stahiki inakuwa nizaidi ya asali au
chochote.
Lakini watu wengi wamekuwa wakiingia katika ndoa
kutokana na ushauri na rafiki wanaowazunguka katika kuwaambia kuwa mmeshakua
mnafaa kuishi na mwanamke na wanaweza kukuaminisha kuwa utaweza tu tena wengine
wanaweza kukusifia kwa upeo ulionao.
Nipende
kusema kuwa mabadiliko ya mwili ukuanza wewe na wala Mungu akuweka mabadiliko ili uingie
katika ndoa.
Lazima ujue miemko ni ishara ya kukua lakini sio
swala la kusukma kuingia katika ndoa kwani inaweza kuwa ni jambo zaidi ya
hatari kwakua KUJUA KUSIMAMA SIO KUJUA KUKIMBIA.
Ni wazi swala zima la ndoa lina muhitaji Mungu
kupita kawaida unavyofikiria na hasa katika dunia ya sasa ilijaa mlundikano wa
maisha yasiyo kuwa halisi na wenye ustawi uliokusudiwa.
Miemko ni radha katika ndoa ambayo inaweza kukupa
raha kuona uhitaji wa mwezako katika ndoa katika wakati sahihi lakini sio swala
la kukuumiza kichwa likaondoa usingizi likaondoa kiu yako na Mungu au bidii
katika elimu yako, ni pende kusema kuwa jambo sahihi uja kwa wakati sahihi
unahaja ya kukulupuka.
Japo sio kauli nzuri sana kwako lakini kwangu ni
nzuri sana inayonipa nguvu NDOA ONA KAMA KIFO.............kama kipo kipo
kitakuja tu, kwani kuna mtu anaweza kukikimbilia kifo na kukifurahia ila kama
kipo kipo tu.
BARIKIWA RAFIKI!!!!!!!!
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson....................................................................0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni