Jumamosi, 13 Desemba 2014

UMASIKINI WA MACHO



UMASIKINI WA MACHO;





Siku zote macho yanaweza kukutia nguvu au kukufanya dhaifu, hali hii inatokea mtu binafsi anapoona mwenyewe hali ya kutoweza au kuogopa na hata kama watu wanaweza kuona tofauti na vile mtu anavyoona. Kwasababu kile anachokiona mtu ndicho kinachokuwa na nguvu katika kutawala katika maisha yake.


Ukiweza kuyaponya macho yako kuona tofauti na hali ilivyo au namna unavyotakiwa kuona basi hapo ndipo kunakushinda au kushindwa, watu wote walioweza kufanya mabadiliko katika dunia na jamii walikuwa na uwezo wa kuondoa umasikini wa macho kwa sababu aliyaelekeza macho yake kuona upande ulio mpelekea njia zaidi kuelekea upande wa kushindwa.

Kuna uwezekano wa kuondoa umasikini wa fikra au akili sio rahisi kuondoa umasikini wa macho kwani umasikini mwingine uondolewa na elimu mpya inayokukubaliana na akili yako lakini huu umasikini wa macho huu unakuwa katika nafsi yako na pengine unaweza kuwa na mali nyingi lakini bado ukawa na umasikini uliokushikilia katika macho yako.

Ninge penda ujue kwamba huu ni umasikini uliotanda giza katika macho yako na hata kama ukitaka kuchukua hatua kutokana na akili yako ilivyoelewa inakuwa shida kutokana na ukamilifu wa moyo katika kukubali hali inakuwa bado ni ngumu sana.

Wakati mwingine umasikini huu wa macho unaondoa hali ya bidii ndani yako na kuwa na shauku katika kufikia ngazi bora kuliko ulipo japo wakati mwingine unaweza kutamani lakini katika kufanya maamuzi yaliyo ubeba moyo inakuwa ni ngumu.na niseme wazi tu kuwa hali hii hakuoni mtu wala hakujui mtu bali ni wewe pekee unayejihukumu na kuona ni mzigo katika maisha yako na wala uwezi kuona fahari ya wewe kumwambia  mtu mwingine kwakua  hata huyo utafikiri kama atakuelewa na kukupa pumziko ndani ya moyo wako. Utabaki nalo moyoni mwako litakua kama mzigo ambao ujui kama ni mwepesi au ni mzito bali utaubeba.

Hali hii inabebwa na hali halisi katika upeo wa macho yako yaliyo kidhi hali yako inayotakiwa katika kukufanya kuwa uwe chini, ni wazi hakuna mtu anaipenda sana hali hii ila kunakuwa na shida kuwa kama hali hii ni tatizo au ndio maisha tunayotakiwa tuishi hivyo siku zote.
Ilikuondoa umasikini wa macho lazima utambue WAZO LA MUNGU KWAKO.

Na sio wazo lako binafsi au wazo la watu wengine wanaokuzunguka.Usihishi maadamu watu wanakaa duniani ndivyo wanavyoishi, bali jitahidi kujua na kutafuta wazo la Mungu katika maisha yako ili ikutambulishe wewe ni nani? Watu wengi utafuta kwa bidii kuwa na hali nzuri ya kielimu, kufedha na mengine mengi lakini tambua kitu kimoja jinsi utavyojitmbua katika kutambulishwa na Mungu hivyo ndivyo mazingira yatavyoambatana na wewe na sio namna nyingine japo sipo mbali na kutia bidii katika kila jambo jema unalolifanya.

Katika wazo la Mungu juu yako hapo ndipo kunakusafishwa kutoka katika umasiki wa macho na kuwa utajiri wa macho uliojaa utoshelevu wa kiMungu utakaoona wewe katika wakati sahihi na uliosimikwa na Mungu mwenyewe.


Imeandaliwa na;
           

                      Cothey Nelson............................................................................0764018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni