SIKU
YANGU;
Ilikwa ni siku ambayo sitaweza kuisahau na wala
sihitamani kuikumba kwanamna ilivyotokea. Ilikuwa siku ambayo ilianza kwa
furaha sana lakini mwisho ulikuwa tofauti na nilivyoitegemea hakika ilikuwa ni
siku ya ajabu na kushangaza sana kwani ilianza kwa kusababisha furaha halafu
mwisho ikiwa ni mateso............... nilikuwa na mdogo wangu tukielekea
vijijini kwetu ambako tulikumbuka sana na tuna amini sana hata wao
walitukumbuka sana pasipo shaka........kwani
wazazi wetu walipiga simu na kuwataarifu ndugu zetu waliopo kijijini
Mbeya walijawa na shauku sana na tarajio
kutuona.
Nasi tuliamka mapema sana mimi na mdogo wangu vick
tuliamka asubui sana na wazazi wetu walitusindikiza mpaka ubungo na kututakia
safari njema na umakini tuwapo safarini na kipindi hicho na kumbuka mimi na
mdogo wangu tulikaa pamoja tayari kuelekea kijiji kwetu, na kumbuka safari
ilianza asubui mnamo saa 12 asubuhi na kipindi hicho abiria wote walikuwa
wamekaaa katika siti zao wakiwa watulivu sana kila mtu akiwa na mawazo tofauti
katika kule alikuwa anaelekea wapo walikuwa wanaenda katika shughuli za
kibiashara, kidini na kuwatembelea wapendwa wao kama sisi tulibeba hilo kusudi
la kuwa salimu ndugu kwani mimi nilitoka mjini Mbeya ni kiwa mdogo sana yapata
miaka 3 na sasa narejea ni kiwa na umri wa miaka 25.
Tulipofika Morogoro maeneo ya mbuga ya mikumi gari
letu lilipata shida na kushindwa kuendelea na safari yake, hivyo abiria baada
ya kusubiri kwa muda wakaanza kushuka taratibu katika kupata hewa
nje.........ila mimi na mdogo wangu tuliofia kushuka chini kwani tulikuwa
tunakumbuka yale maneno ambayo tulioambiwa na wazazi wetu tuwe makini sana
pamoja na kuwa angalifu sana................ITAENDELEA!!!
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson...............................................................0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni