KESHO INA NILILIA
Biblia
inasema....lakini mtu huyu ndiye nitakaye mwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye
roho iliyopondeka atetemikaye asikiapo neno langu. Isaya 66:2b
Kulia ni jambo la kawaida katika dunia japo kuna
kulia kwa kupenda na kulia kutopenda katika haya yote inabaki neon lile hili
KULIA. Tena kubaliana kwa pamoja kuwa katika sehemu kubwa katika maisha ya
mwanadamu uwa hawapendi kulia na katika kulia kunakuwa na sababu ya mtu
kumfanya jambo hili.
Ni wazi kama jana haitakulilia sio jambo la kujivunia
sana kwani kesho inaweza kulilia haya mambo uwa kwa sehemu kubwa na utaratibu
au mfumo uliokuwako unakutengeneza au unaweza kuetengeneza au kuulekebisha.
Ni jambo lisilopingika mambo ambayo yanayosababisha
kesho yako inaweza kutawaliwa na kilio sio kicheko japo inawezekana kuwa
ulikuwa haupendi lakini uhalisia wake utajitokeza na kuchanua matawi yake;
I.umbali wa wewe na Mungu
Ninapozungumzia umbali wako na Mungu si zungumzi
umbali unao onekana lakini nazungumzia umbali usionekana bali unauhalisia mkubwa
na unadhihirika kwake ni mkubwa sana.
Ni bora uwe mbali na wazazi, walezi, marafiki,ndugu
au jama wakiroho japo siku hizi mtu yuko radhi kuwa mbali na Mungu lakini awe
karibu na marafiki,ndugu au mpenzi.
Uwezi ukawa mbali na mtu halafu ukategemea yale yake
ya husike katika maisha yako hivyo unavyokuwa mbali na Mungu tegemea vya Mungu
kupita mbali na maisha yako japo unaweza kuvipenda lakini utaratibu wake
utasimama kama ulivyopangwa kwakila jambo la Mungu limebeba kusudi lake hivyo
linafanya vile lilivyotumwa.
Kuwa na Mungu ni mbali na kusema mimi na mwamini
Mungu na yupo kwakua naishi kwa nguvu zake bali kuwa karibu na Mungu ni zaidi
ya chochote na vilevile sio swala la kuhisi tu bali ni udhihirisho ulio wa
kutisha uliojaa mema mengi yanayo kuhusu wewe.
Mluhusu Mungu aitawale siku yako ili akutengenezee
kesho yako iliyojaa matumaini isiyokoma na iliyokamilifu sana na iliyobeba
ukamilifu usio pungua.
Na mluhusu vipi!-Nguvu ya sauti yake katika maisha yako;
Je katika maisha yako kipi kina nguvu kuliko kingine
au cha maana sana kuliko sauti ya Mungu ndani yako, unahitajikujua kuwa kile
unachokisiliza na kukikubali inatoa dira katika maisha yako inaweza kuwa dira
sahihi au isiwe sahihi.
Je! Sauti ipi inatisha au ina nguvu kwako;
mwenzi,mchumba,fedha,elimu au ushirika mwingine wowote!
Biblia
inasema....lakini mtu huyu ndiye nitakaye mwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye
roho iliyopondeka atetemikaye asikiapo neno langu. Isaya 66:2b
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson.......................0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni