Ijumaa, 26 Desemba 2014

UNASIKIA




UNASIKIA NINI?




Unapoona mtu anafanya jambo lolote au kuongea jua kama alijaanza ndani yake basi amesikia na kulikubali na kulifanya kuwa sehemu ya maisha yake au kama sivyo basi kusikia kumechochea kitu katika kufanikisha swala Fulani. Lakini leo siitaki kuzungumzia kusikia tu bali na zungumzia unasikia nini kwakua kile unachokisikia kina mchango mkubwa katika maisha yako............kwakua kwa sehemu kubwa mwanadamu ubadilika kutokana na kile anachokisikia na hata kukiona.

Ni ukweli wako watu wanafurahia maisha yao leo kutokana na kusikia jambo Fulani na akalifanya kuwa katika maisha yake  na vilevile wako watu ambao wanalia sana kutokana na kile alichokisikia sasa amekuwa na maumivu katika maisha yake, ni kweli kusikia sio kitu kibaya bali swala unasikia nini! Na kwa nini umeamua kusikia.


Sitazungumzia faida na hasara za kusikia bali nitazungumzia namna kusikia kunaweza kukutengeneza kama vile ilivyokutengeneza leo vile ulivyo, ukweli kuna mambo mengi yanafanyika kutokana na kusikia maneno kutoka kwa mtu mathalani mtu anakuwa mke au mume wa mtu kutokana na maneno ya mwenzi wake au mtu anaingia katika biashara haramu kutokana na kusikia kama vile ukahaba, madawa ya kulevya na mengine.

Ni jambo la kawaida usitegemee kuwa watofauti na jinsi vile unavyosikia kwakua kile unachokisikia ndicho kina kutengeneza wewe na kuwa na nafasi ambayo uko nay oleo, wako watu ambao ni wakubwa sana katika kiuchumi kutokana na kile walichokisikia kuwa katika maisha yao hivyo jua mafanikio yako yame bebwa na nini ukisikiacho..........nikupe mfano mmoja kuna ndugu na mfahamu alikuwa anapenda kufuatilia maradhi mbalimbali katika mtandaoni ikatokea akavutiwa sana kuuelewa ugonjwa wa kisukari hivyo mwisho akajikuta ule ugonjwa unaanza kushamiri katika mwili wake...........! narudia tena sio swala la kusikia tu bali nini unasikia kinaweza kukufanya chochote sawa na zima ya kile ulichokisikia.


Bila shaka umeona watu wakiwalaumu rafiki zao na wengine wakiwalaumu wenzi wao japo sijajua wewe unaye soma ujumbe huu unamlaumu nani au kumshukuru nani kwa kua lazima pawepo na mawili kati ya kulaumu au kukshukuru kwa maana nyingine ikikosekana moja basi kunalingine litafuata haiwezi ukawa tofauti na hapo! Kwa kusema hivi si chochei swala zima la kulalamika au kuchukia bali mimi na zungumzi namna nguvu ya kusikia ilivyobadilisha maisha yako.


PENDA KUSIKIA NENO LA MUNGU WAKATI WOTE

Kwani hilo neno limebeba ustawi wa Mungu katika maisha yako

Imeandaliwa na;
              
                       Cothey  Nelson..........................................................0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni