Ijumaa, 17 Oktoba 2014

MSAMAHA NI SIFA YA MKRISTO



MSAMAHA NI SIFA YA MKRISTO;




Japo mkristo anasifa nyingi ambazo biblia inaeleza kama tabia za rohoni, kila sifa aliyonayo mtu ina sababu yake na ina kazi yake. Na utajua umuhimu wa sifa hiyo endapo tu itakapoitajika na ikawa haunacho hicho kitu.japo zipo sifa nyingi na muhimu sana lakini mimi nitaangalia upande wa sifa hii ya MSAMAHA.

Kila sifa ni muhimu sana hasa msamaha ni wazi kuna mahali utashindwa kufikia kwa sababu unakuwa ujakidhi vigezo, hivyo unaweza ukapoteza muda wako na nguvu yako katika maombi na bidii katika kusoma neno la Mungu pasipo kujua msamaha kama moja ya kukupa wepesi kufika kule unakotaka.

Kibinadamu kuna hali ya ubinafsi inayoambatana na kiburi, majivuno na kujihesabia haki na katika hali hii utapenda kisasi kiwafikie wale unaona maadui zako na waabike na wakurudie kwa magoti lakini shida pale vile unavyofikiri isiwe vile ikawa tofauti na vile unavyo tamani. Ni meshuhudia watu wengi wakipata tabu magonjwa mathalani kupooza, vidonda vya tumbo na hata shinikizo la damu.

Ni kweli kusamehe sio jambo ambalo la kawaida ni lazima upate wepesi wa kusamehe na penda kutofautisha vitu viwili hivi mtu kusamehe na mtu kukaa kimya kwa maana katika hali ya ukimya kuna wakati tu italipuka tu na mlipuko wake unaweza ukawa mbaya zaidi. Japo watu wengi usema kusamehe mtu ambaye amekuumiza/amekujeruhi inawezekana kwa kusudia au kutokukusudia shida inakuwa namna gani inakuwa msaada kwangu.

Ni vizuri kutambua usipojenga jenga tabia(mazoezi ya rohoni) katika kusamehe ni wazi unajirudisha nyuma tena katika mtego mkubwa kuwa maisha yako kabla ya wokovu kwamba na wewe unahitajika ufanye jambo ili Mungu apate kukusamehe kwa maana nyingine tunasema unajirudisha katika hali ya kifungoni na inasubiriwa ulipe faini ili uweze kutoka gerezani.

Kukubali kuishi maisha ya kutokusamehe ni kukubali kuishi maisha mbali na Mungu na huku ukitegemea yeye ahusike na maisha yako, sawa na kuvunja ushirika na mtu halafu ukategemea yeye ahusike na maisha yako kwa ukamilifu. Hivyo kukubali kuishi maisha ya kutokusamehe ni kukubali kuishi nje ya utawala wake kwakua yeye ni Mungu anayesamehe na kusahau.

Lazima uchukulie hali yoyote ya kutendewa kinyume na ulivyotegemea ni hali ya wewe kujifunza watu halisi wakoje na sio kuanza kuwachukia kwakua hiyo sio maana ya Mungu ya kuruhusu kukupitisha hapo kwani Mungu analengo la kukuumiza bali anataka matengenezo yake yafanyike ndani yako.

Makwazo yapo ilikuzidi kujisimika na Mungu zaidi na sio kisilani na mtu yeyote Mungu anataka umfanye yeye kuwa ni kila kitu kwako na umuone yeye kuliko chochote  na umweke kuwa tofauti na watu wengine katika utekelezaji wake katika ahadi zake na maamuzi yake.

Msamaha ni ishara ya kumpenda Mungu zaidi ya chochote na ndani ya moyo wako hautaki mtu mwingine au jambo lolote ulipende na likafanye kuwa katika maisha yako kwakua unaweza ukaipenda chuki nayo ikawa sehemu katika maisha ikasababisha Mungu akatoka akaiacha chuki itawale kwakua Mungu achangamani na kila kitu bali Mungu anaheshimu maamuzi yako kwakua yote ameyaweka mikononi mwako uzima na mauti.

Msamaha ni ishara ya kuwa wewe ni mtoto wa Mungu uliyebeba tabia zake kwa ukamilifu wenye ubora uliostahiki, kwakua kigezo cha wewe ni mtoto wa Mungu ni mfanano wa tabia zake na zako na moja wapo Mungu angalii ukubwa wa kosa bali yeye ujua ni kusamehe na kusahau tu na sio linguine na wala kisasi sio mategemeo yake.


Imeandaliwa na ;
                           Cothey Nelson, 0764018535, cotheyn@yahoo.com


PENDO LA MUNGU LITAWALE NDANI YA MAISHA YAKO!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni