USTAWI
WA KIMUNGU
Kutoka 19:5
Hakuna kitu hatari sana
kama UTII kwakua ndani ya utii mtu uweza kufungua hazina yake ambayo aliiweka
kwa muda mwingi……. akitafuta mtu ambaye atamwamini na kuachia mambo yote ndani
yake.
Mshikamano,
ushirikiano, kuimarika katika yote unabebwa na utii na ni utii pekee ndio wenye
kuashiria kuwa wewe una nafasi gani kwa mtu yaani nama unavyo mtii ndiyo ishara
kuwa kwake kuwa unamthamini kwa kiasi gani?
Unapaswa kujua kuwa
yote unaweza kumfanyia mtu hata Mungu akaweza kukupa neema yake lakini sio
kutokutii…….ni ishara kubwa sana kuwa hauko na yeye na uko mbali nae! Tunajua
tatizo la watu sio kutokutii tu bali ni namna ya kutii na mambo ya kutii watu
wengi wanatii katika baadhi ya mambo tu hivyo kupelekea kushindwa kuonyesha
utii uliobeba moyo wote.
Niseme kuwa pasipo utii
hakuna mwendo ulio wa maana wa wewe na Mungu, hata na mtu yeyote kwakua ndicho
kiunganishi kikubwa katika kufanya mambo ya weze kuwa katika hali yake
stahili…kwa hiyo kama hakuna utii hakuna kwenda!
Japokuwa watu wengi
wanatamani sana kumtii Mungu ili wafike peponi wakiwa wana maana waweze kuwepo
mahali ambapo yeye yuko yaani mahali salama mbali na jehanamu, unahitaji kujua
kuwa katika mwendo huo ni vigumu sana katika mwendo wako wa kumtii Mungu katika
hali ya kupenda na sio msingi utakao kuweka imara!
Kumtii Mungu hiyo ni
ishara ya pekee kuwa wewe ni wake, kwani kile unacho kipenda kweli ni wazi
hauwezi kukitii kinafiki kwakua kwakua unakipenda au unampenda Mungu anataka
umtii kwakua unampenda na unamthamini na kuona yeye ni wa pekee katika maisha
yako, kwakua Mungu anataka nafasi ya kutosha ndani ya maisha yako.
Ni seme tu hakuna maana
ya kujipaka au kujiweka utakatifu kama hauna utii wa kweli mbele za Mungu,
hakuna jambo litakuwa na kibali kwa Mungu endapo tu hutajua thamani ya utii
mbele za Mungu.
Udhihirisho
wa utii!!!
i.kifo
cha matumani ya mwili
kama ibrahimu ilibidi
mwili ufe ili aweze kumpata isaka na sio ishamaeli, siku zote mtu yote ana mtii
Mungu uwa anapoteza matumaini ya mwili wake kuwa hapo ndipo mtu anakuwa awazi
nitavaa nini?
Nitakula nini? Nitalala wapi? Haya ni maamuzi yanafichwa na mtu
ambaye aliye mbeba Mungu kweli kweli na anaye weza kufanya mambo ambayo kwa
hakika watu wengi wanaomtazama hawataona maana ya yeye kufanya hivyo.
Hapa mtu anaweza Mungu
tu katika staa ya maisha yake hana jambo jingine na wala haiogopi kesho bali
kesho inamuogopa yeye.
Ni mtu ambaye anakwenda
kinyume na mfumo ulioko katika hali ya dunia bali yeye amebebwa na uweza wa
Kimungu unaompa kuona katika hali ya kimbingu na kusimama mahali pasipo simamika
kwa mtu mwenye akili timamu.
ii.mateso
ya akili
uwa hakuna akili
itazalisha jibu katika mazingira ya mtu anayemtii Mungu alikubali kwenda na
mbingu, hakika kila siku mazingira hayafanyiki tu bali katika uwepo wake hapo
ndipo kunazaliwa vitu vitu vyote vinavyotakiwa kuwepo.
Wakolosai 3:10
mtu huyu hauwezi kukaa
nae ukapata/ukauelewa ufahamu wake kwakua ufahamu wake umefichwa ndani ya
kristo na kinachoonekana na kristo mwenyewe katika kuyafanya mambo ambayo
hayawezekanai kabisa.
Nikweli hauwezi
kumpendeza Mungu katika mazingira ya kuonekana ya kawaida ya kila siku na
mtazamo wa akili ya kawaida………unahitai kuwa na akili nyingine!
AKILI INAYOANZISHA SIO AKILI
INAYOFUATA!!!
Imeandaliwa
na;
Cothey
Nelson………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni