MAAMUZI
MAGUMU NI MAISHA YANGU
Maamuzi magumu kwa
maana nyepesi ni uchaguzi wa kujigharim!
Uwa hakuna furaha
katika maamuzi magumu katika kila hatua ya awali ya mwanadamu anayoipiga ila
matokeo yake yanaweza yakazalisha furaha, naamini kila binadamu anatawaliwa na
maamuzi katika utendaji wake ya sasa na hata ya baadae yanabebwa na maamuzi.
Kwa sababu unaishi basi
swala la maamuzi uwezi kuliepuka, yapo Maamuzi tunayo yafanya kila siku
tunayaita kuwa haya ni maamuzi ya kawaida ambayo baadhi unajigharim kidogo na
hata mengine haujigharim kabisa………kwa maana yako mengine unakuwa na wasiwasi
sana na mengine unakuwa huna wasiwasi kabisa.
Tuna amini katika
maamuzi magumu tunaweza kufanya jambo kuwa kubwa tena kwa wepesi zaidi katika
muonekane wake, ni jambo la kawaida sana kwa wale walifanya mambo ambayo
yamekuwa msaada sana katika maisha yetu mathalani waliotengeneza ndege,meli na
mengine mengi sio ajabu wengine walitumia muda wao mkubwa katika shughuli hizo
kuliko hata na familia zao,ndugu zao na pia hata marafiki zaohatimae
wakafanikisha ile ndoto yao.
Niseme kuwa katika
maamuzi haya magumu hapa ndipo tunaweza kufanya mambo katika mafanikio makubwa
japo wako watu wanafanya maamuzi madogo huku wakitegemea kupata mafanikio
makubwa…..sio kila jambo rahisi kama hivyo bali tambua kuwa kazi kubwa katika
maamuzi yako ndio yanaleta matokeo makubwa.hivyo utakiwi kuogopa sana katika
maamuzi magumu hasa yakiwana tija katika maisha yako na mbele za Mungu.
Ukweli hatua yako ya
mbele inategemea sana maamuzi yako kwani maamuzi yenye kujigharim kidogo basi
hiyo ni hatua ndogo lakini maamuzi yenye kujigharim sana basi hiyo ni hatua
kubwa katika maisha yako.
Katika maisha
tuliyonayo uwa hatuwezi kufika katika maamuzi yasiyo na kina mathalani serikali
yetu na mambo mengine yafananayo na hilo mengi sana yamekubwa na mfumo ambao
kwa kiasi kikubwa hauja beba haki au usawa bali katika kila jambo jambo
walitendao limejaa udhalimu na ubadhilifu wa mali ya umma katika hili ni seme
tu wazi tunahitaji mapinduzi magumu yanayobebwa na dhamira ya dhati katika
kuleta mabadiliko chanya.
Tukianza na maisha
binafsi hatuna budi kuhakikisha kuwa maamuzi sahihi yaliyojaa kujigharim ndio
chachu nzuri ya maendeleo mathalani wako watu wanaanza na pa dogo lakini mwisho
wao wanategemea kufika mbali sana lakini kama ukiangalia mwanzo wao unaweza
usione mwisho wenye maana sana.
Lakini watu wengi
wanaogopa kuingia katika maamuzi magumu kwani wanaona kama wataonekana wanaanza
moja, na hivyo wataonekana kama wajinga hawajui wanachofanya na kuona kwamba
hawata kaa wafike japo haya ni mawazo au ni maneno ya kawaida sana lakini
yanaweza yakabadilisha mfumo wa maamuzi
wako badala ya kwenda kulia ukaanza kwenda kushoto.
Hivyo imekuwa ngumu
sana kwa watu katika kuamua maamuzi magumu na wengi wamekuwa wakiendeleza hata
kwa yale wanaona wanaelekea sio salama lakini wamekuwa wakijikaza kisabuni
maadamu siku zinaenda na maisha yanadumu basi wanavumilia wakiamaini ipo siku
mambo yatabadilika.
Asikudanganye mtu uwa
mambo mengi hayajibadilishi bali yanabadilishwa na mtu husika au mfumo husika
hivyo kusubiri maji yabadilike ni sawa kusubiri maji ya bahari chumvi ya
badilike alafu maji yawe kama ya mto…………unaweza
ukasubiri sana! Lakini matokeo yake yameshatokea na kamwe haya wezi kubadika.
Unaaja kumcheka
kinyonga kwa sababu ya mwendo wake bali angalia wewe unapo lala yeye anakuwa
wapi lengo lake ni muhimu sana kuliko chochote uwa anajiangalia mwenyewe na
kujikubali yeye kama yeye na hatimae anatimiza malengo yake.
Hakuna anayeweza
kubadilisha maisha yako ila ni wewe mwenyewe!
Imeandaliwa na;
Cothey
nelson…………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni