NGUVU YA MTANDAO
Mwanzo 11:1-6
“Bwana akasema,tazama,watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni
moja ………………..wala sasa hawatazuiliwa neno wanalolikusudia.”
Sote tunajua pindi mtandao ukiwa vizuri basi
mawasiliano yanakuwa mazuri na hata huduma zingine uweza kufanyika kwasababu
mtandao umekaa vizuri! Na pindi mtandao unapokuwa chini au unaposumbua basi
yako matatizo yanaweza kutokea kama ucheleweshaji wa taarifa au kutofika kabisa
na pengine uweza kukosa huduma uliyokuwa unahitaka.
Ili mtando ufanye kazi lazima pawepo na
mjumuhisho wa vitu vingi ili viwezeshe mtandao kuweza kutenda kazi katika
ufanisi wake na pindi kifaa au kitu kimoja kinaposhindwa kufanya kazi yake basi
uweza kusababisha ufanisi wa mtandao kuwa chini au kuwa duni.
Katika utendaji ulio na tija na ulio na
uwezekano wa kufanya vizuri lazima wafanye kazi katika mfumo wa kimtandao au
kishirikiana kitim( team work) ufanyaji kazi au utendaji wa shirika.
Ni wazi ili kufanya kazi au jambo katika
ushirika wa kimtandao hatuna budi kila mtu kutambua nafasi yake na kila mtu
lazima haiheshimu nafasi ya mwezake kuona kuwa naye anawajibika katika nafasi
hivyo pasipo na hali ya kuzalauliana au kutoaminiana bali kila mtu awajibike
akatika nafasi yake tena katika ufanisi huku akijua kwa yeye katika kuwajibika
atapunguza mazigo kwa mwingine katika kuwajibika na hivyo kuwa na mchango wa
uboreshaji wa kimtandao na sio kuzolotesha mtandao.
Kufanya kazi katika hali ya kimtandao kunatoa
asilimia kubwa ya kushinda kuliko kushindwa, lakini kufanya kazi isiyo ya
kimtandao kunakuwa na asilimia kubwa ya kushindwa kuliko kushinda na katika
swala zima la kimtandao sumu kubwa ni kutenda jambo katika hali ya ubinafsi na sio shirika.
Ni kweli hulka ya kibinadamu inaweza kusema
mimi naweza hata nikiwa peke yangu ukweli ni ngumu sana hasa kwa jambo la muda
mrefu kwakua katika kufanya jambo kimtandao kunaleta wepesi na
uharaka……….pamoja na hilo pia kama jambo mnafanya kitim lakini hakuna
kushikamana basi bila wasi jambo hilo litakuwa kubwa badala ya kuwa dogo na
litachukua muda mrefu sana badala ya kuchukua muda mfupi.
Jambo hili limekuwa ni shida kubwa katika
utendaji kazi wa watu wengi wako walionza katika ushirika huu lakini baadae
ukagawanyika na wako wanaondelea na ushirika lakini kila siku unapungua ubora
wake na kutoa kiashirio kibaya…….sababu kubwa watu wameshindwa kwenda sawa na
tofauti zao hivyo badala ya kujuana zaidi kukazalisha utengani wa mioyo na
baada utakuja wa mwili.
Niseme mambo mengi yanashindwa kufika mbali
kutokana na vitu viwili yaani mfumo usioeleweka(unstructure) na hatua
yakufanikisha jambo hilo(strategies) hivi ni vitu vidogo sana lakini vina maana
kubwa na uwezeshaji mkubwa katika utendaji wake.
Ni muhimu kama mmeweka utaratibu basi kila
mtu aufuate huo utaratibu na kuhakikisha unatekelezeka na kamwe hakuna mtu
aliyejuu ya huo utaratibu ili kuusaidia huo utaratibu unadumu na kufuatwa
kikamilifu.
Na ni muhimu kujali vitu vyote viwili kwa
pamoja yaani jambo linalo fanyika na wanaofanyakazi hiyo kwakua vyote ni muhimu
katika uzalishaji.
Ilikuwa na
mtandao wenye nguvu ni muhimu kuzingatia yafuatayo: UWAZI,UWAJIBIKAJI NA USAWA!
Imeandaliwa
na ;
Cothey
Nelson……………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni