Jumanne, 25 Agosti 2015

UPANDE ULIO BEBA USALAMA WAKO



UPANDE ULIO BEBA USALAMA WAKO



Moja ya vitu vinavyopendwa na watu wengi ni usalama!

Kwakua katika usalama kuna utendaji katika uhuru na nafasi ya kufanya jambo lenye ubora wake.tuna fahamu kuwa moja ya kazi ya vyombo vya ulinzi ni kulinda mipaka ya nchi ( kuhakikisha usalama wa nchi wakati wote)

Na hichi ndicho kitu ambacho watu wengi ukitamani sana…..usalama wao pamoja na mali zao, kwakua wanajua katika usalama basi mambo mengi uwa rahisi kufanyika pasipo na ugumu usiokuwa na lazima.

Shida kubwa moja ya watu wengi wanapenda sana kuwa na usalama lakini namna wanavyoenenda wanaufukuzia mbali usalama wao na vitu vyao……….sawasawa mtu anayetumia dawa(dozi) katika hali mbaya lakini bado mtu anatumia kilevi kikali lakini katika hali hiyo bado anaamini Mungu atamsaidia.

Niseme wazi siku inapande mbili yaani usiku na mchana……..na hata dunia inapande mbili yaani uliosalama na usio salama, na hakuna ambaye apendi usalama lakini ugumu uko katika  kudhihirisha kuwa wewe unapenda usalama katika maneno tu au pia katika mfumo mzima wa maisha yako.

Kibinadamu yako mambo mengine mtu anafanya akiwa ametiwa giza akiamini anaona kumbe haoni sawasawa na mtu kuamini anajua kumbe ajui! Ndani ya dunia kuna mtindo ukiishi ambao utaondoa usalama wa maisha yako na kusababisha mambo mengine yazidi kukukabili.

Unahitaji kujua kwamba binadamu wewe ni sahihi kwamba uhuru ulionao unapaswa usifanane na wanyama katika utendaji wako na katika kutimiza hisia zako inakupasa ujue kuwa viumbe vyote vya dunia vinapaswa vijifunze kupitia wewe na sio wewe ujifunze kwao unaweza kukataa kabisa lakini ukweli ni kwamba mambo mengi tunayoyafanya yanafanana na wanyama kwa asilimia kubwa mathalani kupigana hadharani na matendo mengine yanayofanana na hayo.

Kuna maisha ya mengine mtu anaishi unaona mwisho wake wa maisha yake umebebwa na maumivu, kukataliwa na hata kutengwa lakini bado mtu anakuwa anakaza mwendo kuendelea, na ukiwasikiliza wanasababu nyingi wengi wakisema maisha magumu, nilikataliwa na wengine wanasema nimetendwa vibaya hivyo staili ya maisha haya ndio niliyoichagua hivyo na ishi maisha haya sio kama napenda bali inanilazimu.

Niseme kwamba kwa namana yoyote ulivyo, jua yuko mmoja tu ambaye atakupenda vile ulivyo na kutopenda aibu yako iendelee kwakua kwa yeye ulitoka na kwake utarejea, hivyo niseme wazi katika maisha yoyote unayoishi bado Mungu aliyenipenda mimi basi anakupenda nawe tena upendo uleule hakika ni baba mwema.

Niseme maadamu unaishi tu haijarishi uko katika hali gani nini kimeathiri mwili wako, akili yako na kuona kuwa umeharibu mstakabali wa maisha yako napenda ujue kuwa bado unayo nafasi kubwa kwa Mungu aliyekuumba anaweza akainawilisha tena ngozi yako na kuwa zaidi ya ulivyokuwa jana! Huna haja ya kulia na kusononeka sana bali yuko Mungu ambaye kwake yeye kila kitu kina nawilishwa na kuzidi kwa bora.

Mungu anasubiri maamuzi yako tu katika kurejea kwake naye akufanye kuwa mtu wa maana katika viwango vyake. Mungu awezi kukurahumu wala kukuchoka bali anajua kuwa kwa wewe unaweza kuwa mtu mwingine kupitia yeye.

Hivyo Mungu anasubiri umpatie maumivu yako,teso lako na dhihaka yako ili yeye achukue na kukuacha ukiwa huru mbali na mateso…………maana salama yako ndio furaha yake.

Giza katika dunia japo ni sehemu ambayo watu wengi upenda kufanya mambo yao kwasababu kuna maficho yao lakini hawapendi kujua kuwa ndani ya giza kuna upofu uharibifu na mateso yaliyobebwa na huzuni isiyokoma.

Nuru ya Mungu katika dunia hii……… hapo ni sehemu salama japo watu wengi hawapendi kwenda katika njia hiyo kwani haina mvuto lakini niseme kwamba katika nuru kuna nguvu na uimara uliobeba stara ya mwanadamu.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni