Jumanne, 18 Agosti 2015

MVUTANO KATIKA KUISHI



NAISHI KWA RIDHAA YA NANI?



Hakuna kitu kizuri kama kuishi hasa kuishi katika maisha unayoyataka, kwani kila binadamu ana uhuru wake na matakwa yake………….ni jambo lililowazi kuwa binadamu yeyote ili aishi anahitaji kutambua mambo matatu yanayoonyesha/dhihirisha utashi wa kuishi kwake;

a)kuishi kwa matakwa ya nafsi

b)kuishi kwa matakwa ya dunia

c)kuishi kutokan na utu wako

hivi ni vitu vitatu ambavyo ukiangalia kwa jicho la haraka haraka utaona kama kunakuingiliana au kushabiliana lakini ukweli kwamba uko utofauti mkubwa katika kila kitengo na utendaji wake.

Katika utendaji au maamuzi ya mwanadamu yeyote yanaathiriwa na vitu hivi vitatu au kushawishiwa na na vitu hivi…………..unaweza usiwe tayar i(utu) lakini nafsi yako ikakushawishi na unaweza usipende lakini nguvu ya dunia ikakushinda  na hatimae ukaamua au kutenda pasipo kupenda au pasipo utayari ulio kamilifu.

Watu wengi wanakuwa na shauku katika kutenda jambo ambalo litakalo furahisha moyo wake au kuleta fahari katika maisha ya mtu husika lakini nguvu ya dunia inaweza kupindua maamuzi yake au lile kusudio lake.

Hii ni moja ya shida inayoikabili dunia kwa sasa kwani nguvu ya dunia imekuwa na uweza hata kuliko maamuzi ya mtu husika au nafsi ya mtu mwenyewe, hii ni vita imekuwa ikila muda mwingi na kuchosha watu wengi kutokana na mwenendo wake ni tofauti kabisa na hali ilivyo au vile anavyotaka.

Wako watu walijitahidi kuwa wakarimu,wenye upendo lakini hali hii haikudumu bali nguvu ya dunia ikawa vaa na kujikuta katika kuwa na tabia sawa na dunia ilivyowaweka ndani yao kuwa na kisilani,chuki na malipizo yasiyo na akili au yasiyoangalia mwendelezo wenye maana.

Watu wengi wamekuwa wakijifunza mara baada tu yakuona yaliyotokea kwa wengine hasa upande wa hasara na wengine wanajifunza mara baada ya jambo jema kutokea kwa mtu lakini walio wengi wamekuwa wakishindwa kuweza kuenenda sawa na walivyojifunza kwa wengine wakajikuta kudumbukia mara ambapo dunia ikawazamisha

Matahalani mtu amejifunza au kuona mtu alivyoathirika na ukimwi na mateso aliyoyapata lakini kutokana na ushawishi wa dunia basi nae akajikuta anazidiwa na ile nguvu ya dunia na hatimae naye kujikuta kaingia katika mateso hayohayo.

Ni vitu viwili tofauti kati ya kujifunza na kutendea kazi hivi vitu havilingani kwani watu wengi wanayojifunza sio yale wanayoyatenda………..mtu anaweza kujifunza kuwa sumu ya panya inaua lakini mtu kwakujua kuwa kuwa ni kinywa sumu ya panya nitakufa lakini bado anakunywa na huku akiwa tayari kufa bila shaka inakuwa nguvu ya dunia imemzidi.

Ni lazima ujue kwamba kuishi uku ukienda kinyume au kutoenda sawa na nguvu ya dunia unahitaji Nguvu kubwa, maarifa ya kutumia hayo nguvu na kuwa mwepesi kwenda sawa na wimbi la mbingu!

Vijana wengi wanapotea,wazee wengi wanapotea kwasababu na kushindwa kuimiri nguvu ya dunia na hatimae kuwazamisha katika maji yenye kina kirefu na kushindwa kumudu.

Kujifunza mambo ya dunia haitoshi ni lazima ujifunze habari sahihi za mbingu! *Kwani dunia inakamilika kunapokuwa mbingu na nchi.

“mjue sana Mungu ili uwe na amani ndipo mema yatakapokujilia” ayubu 22:21

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni