Jumanne, 8 Septemba 2015

JANA SIO LEO



JANA SIO LEO


Hakuna leo bila jana na hakuna maana ya jana bila leo!!!!!!!

Jana na leo tunaita utofauti wa siku, kwa maana siku iliyopita tunaita jana na siku iliyopo aua inayoendelea tunaita leo!!

Kwahiyo unaposikia neno jana na leo sio kitu cha kukushtua au kukushangaza kwa maana umekuwa ukisikia na bado unaendelea kusikia na nzuri zaidi wewe mwenyewe umekuwa shuhuda ukiona jana ikibadilika na hatimae ikawa leo……..asante kwa hilo!

Tutakubaliana kwa dhati kabisa kuwa siku inapobadilika inabadilika na mambo yake na unaweza ukagundua sasa au baadae mathalani mtu anapokuwa akikua ni ngumu kutambua sasa mtu ndio ninakua katika kitendo kinachoendelea sasa bali baada ya muda ataona  mabadiliko ndipo unapotambua mtu huyu amekuwa hivyo inakuwa umeweza kuitofautisha jana na leo…..asante sana!

Hakuna kitu kizuri kama kuishi kwingi maana walimwengu wanaamini kuwa kuishi kwingi ni kuona mengi pasipo kujali hayo unayo yaona unakuwa katika nadharia hipi au katika wakati gani, na japo watu wengi wamekuwa wakijivunia katika ongezeko la miaka kutokana na vitu hivi viwili yaani jana na leo ndio maana watu wamekuwa wakifisha miaka fulani basi hapo uweza kufanya sherehe ya kuzaliwa (happy birthday) hasa watu wenye kutambua maana yake na mwenye uwezo huo na hasa mwenye nafasi hiyo.

Unapoangalia katika dunia ya sasa unaweza kushangaza sana watu wengi wanaolia wanasema jana yangu haikuwa hivi inaweza kuwa ilikuwa ni nzuri au mbaya lakini ni muhimu aitaje kuonyesha jana yake ilikuwa vipi ikaazaa leo yake………hivyo kucheka au kulia sio tatizo bali katika kuonyesha kuwa naye alipitia katika mwenendo wa siku.

Ni kweli mambo mengi yaliyofanyika kipindi cha nyuma ni tofauti kabisa na kipindi cha sasa japo watu wengi wanasema kuwa ni maendeleo lakini unaweza kujiuliza ni kweli yanaleta maendeleo hayo yanayosema au ni geresha tu.

Sikatai yako mambo ya jana ambayo leo yanaonekana kuwa hayana nafasi tena na hivyo imeweza kusababisha katika harakati za maendeleo kuongeza mwendo katika kufikia hatua bora zaidi kuliko ya awali mathalani kutokana maendeleo ya sayansi na teknolojia imesaidia kwa kiasi kikubwa  katika kuwasiliana kupitia hiyo watu wamekuwa wakiwasiliana katika njia ya sauti na hata ya video na hivyo kujenga ukaribu zaidi miongoni mwa watu na watu hama jamii na jamii.

Yapo mengi kutokana na maendeleo haya yameibua mausiano ya kujenga na mausiano ya kubomoa lakini yote ni matokeo ya haya maendeleo.

Katika dunia ya sasa kila kitu kimekuwa ni biashara hata vile haviuziki sasa vimekuwa na sokoni na vimekuwa na uwitaji mkubwa wa wateja, watu wamekuwa wakiuza kila kitu kinachoonekana katika macho ya nyama na hata kisichoonekana…………..sikuizi watu awajali nini wanauza bali wanchojali ni kiuza nitapata kiasi gani! Sasa sijajua kuwa hii ni dunia ya kibepari au mmomonyoko wa madili katika dunia ya sasa.

Samahani sana sipati picha dunia ya leo kama kusingekuwa na ukimwi sijui hali ingekuwaje na hasa katika jamii ambayo watu wengi hawana hofu ya Mungu bali wanaenda kanisani.

Katika dunia ya sasa HESHIMA imekuwa bidhaa adimu na sijui kuwa kama watu wenyewe wana jishushia heshima  au wanashushiwa heshima au heshima yenyewe inashuka? Bado sijapata jibu lakini kwa macho yangu naona heshima ikishuka kwa kiwango kikubwa sana sio mtoto wala mkubwa kila mtu anafanya kadiri anavyoona sawa machoni pake na sio kama inavyopaswa kuonekana kuwa sawa machono pa jamii nzima.

Kwa upande wa watumishi wa Mungu mambo mengi yamekuwa tofauti hasa katika zama za manabii wa kina eliya,samweli na wengi walikuwa kweli wana muakilisha Mungu sasa hivi imekuwa ni tofauti…..watumishi wengi wamejiusisha na utapeli waweze kuendesha maisha yao na sio kufanya kazi ya Mungu wengine wamethubutu hata kutumia nguvu za giza katika kutaka watu wawaamini na kuwaogopa.

Sina ugomvi na watumishi wa Mungu mimi na waamini sana na ninawapenda sana hasa wanaojua wajibu wao na kumtumikia Mungu katika kweli tupu na katika udhihirisho wa Mungu mwenyewe!

Sisemi uahache kumwabudu Mungu kutokana na mambo yanayo endelea katika dunia ya leo niseme usalama wako sio kumwamini sana mtumishi wa Mungu bali ni kufahamu kweli ya Mungu ambayo itakutunza na kukulinda na kukupa mwendo mwingine katika Mungu.

Msikilize mtumishi wa Mungu kwani yeye ndiye amewekwa kwaajili yako ili akuongoze katika kweli ya Mungu lakini yeye anasehemu yake lakini wewe unasehemu sana ya kufanya ili uone matunda unayokusudiwa ……………kwani mtumishi wa Mungu anakupa mbegu na maelekezo yake lakini kutafuta shamba, jembe ni wewe mwenyewe na kupanda kwa kufuata maelekezo yake ni muhimu sana! Lakini kumjua Mungu binafsi ni jambo la msingi sana kuliko yote!

Hakikisha moyo wako haujabeba chuki wa kisirani katika yote bali umuone Mungu katika kila jambo naye akupe raha ya kudumu au ya milele…………….mwamini Mungu naye anaweza kukutoa wewe pale ulipo na kukuweka katika hatua nyingine iliyo bora zaidi.

Nibora wakuone uendi na wakati kuliko kwenda na wakati huku unabeba historia mbaya!! Ambayo itakutesa katika kesho yako………………………….!

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………….0764 018535

                           MUNGU AKIKUBARIKI HAKUNA ATAYE KULAANI                          

Jumanne, 1 Septemba 2015

KUMTEGEMEA MUNGU



KUMTEGEMEA MUNGU


 Mathayo 15:8

“ watu hawa uniabudu kwa kinywa tu lakini mioyo yao iko mbali nami”

Hakuna jambao ambalo Mungu analitafuta/mtu anayemtafuta kama mtu ambaye anamtegemea yeye!!

Mshangao Mungu katika dunia ya sasa!

Ni sawa baba aliye na mtoto ambaye rika la mtoto bado linatakiwa liwe chini ya uangalizi wake lakini yeye anataka ajitegemee mwenyewe pasipo kujua au kuwa na upeo wa kujua kuwa maisha ni nini? Bila shaka hilo litakuwa swali kubwa ndani ya moyo wa baba kwa kutaka kujua kinagaubaga kwa nini mwanangu anafikiria aanze kujitegemea wakati bado rika lake linaitaji kuwa chini ya uangalizi wangu.

Nikubaliane kuwa yako mambo mengine yanatokea katika maisha yetu ambayo sio mpango wa Mungu kabisa lakini tumekuwa tukijifariji tu……..lakini ukweli tumekuwa tukitegemea kitu ambacho akipo au hatukijui vizuri hama ambacho hatuna uhakika sana na mwisho tumekuwa katika mazingira tofauti na ndoto zetu.

Kumtegemea Mungu sio jambo lelemama ukiwa hapa duniani kwani dunia inahitaji uitegemee yenyewe ili ikupe kile inachofikiri kukupa……..nguvu ya dunia imekuwa ikiwavuta wengi  na kusahau kwamba imetupasa kumtegemea Mungu kwa asilimia zote hivi sasa wako watu wanawategemea wachungaji wao, marafiki na mtu ambaye anaamini kuwa atanisaidia lakini uwezi ukalinganisha mtu anayemtegemea Mungu na mwingine asiye mtegemea bali anategemea vitu vingine.

Nyimbo nyingi zime imbwa na kupendwa na watu wengi  katika ujumbe wa kuonyesha faida ya kumtegemea Mungu lakini ukweli baada ya kuimba na kucheza na hatimae kutoka jasho tukaacha hapohapo kwa kujua kuwa kumtegemea Mungu ni nyimbo na wala sio maisha ( nyimbo kugusa hisia zako sio kumtegemea Mungu).

Ukweli katika dunia ya sasa wako watu ambao kwa muonekano na  wingi wa maneno yao unaweza kuona au kuamasika na hata kushawishika kuwa watu hawa wana mtegemea Mungu lakini ukweli muonekano wa mtu na namna mtu anavyojieleza sio dalili au ishara nzuri ya kuonyesha kuwa huyu anamtegemea  Mungu na huyu amtegemei Mungu.

Ujumbe huu hauko katika kuwapima watu na kutambua nani anamtegemea Mungu na nani amtegemei Mungu, bali ni kuonyesha maisha ya sasa yalivyoenda mbali na kumtegemea Mungu hivyo na kukuhatarisha kuwa makini sana katika dunia ya leo hivyo kutambua kwa uhalisi au kwa uhakika namna ya kumtegemea Mungu.

Ukweli kumtegemea Mungu kupo na kunawezekana na kunatenda kazi ni wewe kuamua sasa na anza kumtegemea Mungu kwani hapo ndipo kunazaliwa mkristo ambaye kwa uhakika Mungu ndiye anayemtaka na anamtafuta ili amfanyie ibada ambayo anajua kwa uhakika itampendeza yeye na kuimarisha mausiano yao.

Niseme tu hakuna maisha ya ushindi kwa uhakika mbali na kumtegemea Mungu na kwa namna hiyo ukristo unakuwa wa maana na tishio kubwa katika upande wa giza kwa wewe kuishi maisha ya kumtegemea Mungu.

Lazima ujue uwezi kuondoka katika maisha ya utumwa kwa kuombewa tu au kutabiriwa tu japo mambo yote sio mabaya lakini jibu la uhakika ni kuishi maisha ya kumtegemea Mungu kuliko na udhibitisho wake na sio mtu mwingine.

Kumtegemea Mungu ni kuishi na Mungu kwa namna anavyokukuelekeza au maisha yasiyo na uhai wa akili ya kibinadamu,maisha yaliyo jaa kiu ya kutembea na hatua za Mungu. Haya ni maisha ambayo hayafuati watu waliishije bali mimi ninatakiwa niishije!

Yoshua 1:1-9

Kumtegemea Mungu tunaona yoshua wakati anaachiwa kijiti na Musa…… kipindi cha Musa alipewa fimbo na wingu lilikuwalikimuongoza katika safari yake na Israeli lakini yoshua alipewa neno la Mungu liwe dira yake katika utendaji wake na katika muongozo wake. Yoshua alikuwa na mwendo mwingine na Mungu katika kuyafikia malengo ya Mungu aliyaweka katika maisha yake….!

Uwezi ukamtegemea katika hali ya kubahatisha lazima pawepo na muongozo wa uhakika ukikuongoza kutoka hatua moja na kwenda hatua nyingine inabidi iwe ni ya uhakika na muongozo ulio salama usio sitasita………………..!

Kama kweli unataka kuondokana na changamoto zinazokukabili basi tafuta kwa bidii namna sahihi ya kumtegemea Mungu! Maana hapo ndipo palipo na tulizo lako na furaha ya kudumu.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………0764 018535