JANA SIO LEO
Hakuna leo bila jana na
hakuna maana ya jana bila leo!!!!!!!
Jana na leo tunaita utofauti
wa siku, kwa maana siku iliyopita tunaita jana na siku iliyopo aua inayoendelea
tunaita leo!!
Kwahiyo unaposikia neno jana
na leo sio kitu cha kukushtua au kukushangaza kwa maana umekuwa ukisikia na bado
unaendelea kusikia na nzuri zaidi wewe mwenyewe umekuwa shuhuda ukiona jana
ikibadilika na hatimae ikawa leo……..asante kwa hilo!
Tutakubaliana kwa dhati
kabisa kuwa siku inapobadilika inabadilika na mambo yake na unaweza ukagundua
sasa au baadae mathalani mtu anapokuwa akikua ni ngumu kutambua sasa mtu ndio
ninakua katika kitendo kinachoendelea sasa bali baada ya muda ataona mabadiliko ndipo unapotambua mtu huyu amekuwa
hivyo inakuwa umeweza kuitofautisha jana na leo…..asante sana!
Hakuna kitu kizuri kama
kuishi kwingi maana walimwengu wanaamini kuwa kuishi kwingi ni kuona mengi
pasipo kujali hayo unayo yaona unakuwa katika nadharia hipi au katika wakati
gani, na japo watu wengi wamekuwa wakijivunia katika ongezeko la miaka kutokana
na vitu hivi viwili yaani jana na leo ndio maana watu wamekuwa wakifisha miaka
fulani basi hapo uweza kufanya sherehe ya kuzaliwa (happy birthday) hasa watu
wenye kutambua maana yake na mwenye uwezo huo na hasa mwenye nafasi hiyo.
Unapoangalia katika dunia ya
sasa unaweza kushangaza sana watu wengi wanaolia wanasema jana yangu haikuwa
hivi inaweza kuwa ilikuwa ni nzuri au mbaya lakini ni muhimu aitaje kuonyesha
jana yake ilikuwa vipi ikaazaa leo yake………hivyo kucheka au kulia sio tatizo
bali katika kuonyesha kuwa naye alipitia katika mwenendo wa siku.
Ni kweli mambo mengi
yaliyofanyika kipindi cha nyuma ni tofauti kabisa na kipindi cha sasa japo watu
wengi wanasema kuwa ni maendeleo lakini unaweza kujiuliza ni kweli yanaleta maendeleo
hayo yanayosema au ni geresha tu.
Sikatai yako mambo ya jana
ambayo leo yanaonekana kuwa hayana nafasi tena na hivyo imeweza kusababisha
katika harakati za maendeleo kuongeza mwendo katika kufikia hatua bora zaidi
kuliko ya awali mathalani kutokana maendeleo ya sayansi na teknolojia imesaidia
kwa kiasi kikubwa katika kuwasiliana
kupitia hiyo watu wamekuwa wakiwasiliana katika njia ya sauti na hata ya video
na hivyo kujenga ukaribu zaidi miongoni mwa watu na watu hama jamii na jamii.
Yapo mengi kutokana na
maendeleo haya yameibua mausiano ya kujenga na mausiano ya kubomoa lakini yote
ni matokeo ya haya maendeleo.
Katika dunia ya sasa kila
kitu kimekuwa ni biashara hata vile haviuziki sasa vimekuwa na sokoni na
vimekuwa na uwitaji mkubwa wa wateja, watu wamekuwa wakiuza kila kitu
kinachoonekana katika macho ya nyama na hata kisichoonekana…………..sikuizi watu
awajali nini wanauza bali wanchojali ni kiuza nitapata kiasi gani! Sasa sijajua
kuwa hii ni dunia ya kibepari au mmomonyoko wa madili katika dunia ya sasa.
Samahani sana sipati picha
dunia ya leo kama kusingekuwa na ukimwi sijui hali ingekuwaje na hasa katika
jamii ambayo watu wengi hawana hofu ya Mungu bali wanaenda kanisani.
Katika dunia ya sasa HESHIMA
imekuwa bidhaa adimu na sijui kuwa kama watu wenyewe wana jishushia
heshima au wanashushiwa heshima au
heshima yenyewe inashuka? Bado sijapata jibu lakini kwa macho yangu naona
heshima ikishuka kwa kiwango kikubwa sana sio mtoto wala mkubwa kila mtu
anafanya kadiri anavyoona sawa machoni pake na sio kama inavyopaswa kuonekana
kuwa sawa machono pa jamii nzima.
Kwa upande wa watumishi wa
Mungu mambo mengi yamekuwa tofauti hasa katika zama za manabii wa kina
eliya,samweli na wengi walikuwa kweli wana muakilisha Mungu sasa hivi imekuwa
ni tofauti…..watumishi wengi wamejiusisha na utapeli waweze kuendesha maisha
yao na sio kufanya kazi ya Mungu wengine wamethubutu hata kutumia nguvu za giza
katika kutaka watu wawaamini na kuwaogopa.
Sina ugomvi na watumishi wa
Mungu mimi na waamini sana na ninawapenda sana hasa wanaojua wajibu wao na
kumtumikia Mungu katika kweli tupu na katika udhihirisho wa Mungu mwenyewe!
Sisemi uahache kumwabudu
Mungu kutokana na mambo yanayo endelea katika dunia ya leo niseme usalama wako
sio kumwamini sana mtumishi wa Mungu bali ni kufahamu kweli ya Mungu ambayo
itakutunza na kukulinda na kukupa mwendo mwingine katika Mungu.
Msikilize mtumishi wa Mungu
kwani yeye ndiye amewekwa kwaajili yako ili akuongoze katika kweli ya Mungu
lakini yeye anasehemu yake lakini wewe unasehemu sana ya kufanya ili uone
matunda unayokusudiwa ……………kwani mtumishi wa Mungu anakupa mbegu na maelekezo
yake lakini kutafuta shamba, jembe ni wewe mwenyewe na kupanda kwa kufuata
maelekezo yake ni muhimu sana! Lakini kumjua Mungu binafsi ni jambo la msingi
sana kuliko yote!
Hakikisha moyo wako
haujabeba chuki wa kisirani katika yote bali umuone Mungu katika kila jambo
naye akupe raha ya kudumu au ya milele…………….mwamini Mungu naye anaweza kukutoa
wewe pale ulipo na kukuweka katika hatua nyingine iliyo bora zaidi.
Nibora
wakuone uendi na wakati kuliko kwenda na wakati huku unabeba historia mbaya!!
Ambayo itakutesa katika kesho yako………………………….!
Imeandaliwa
na:
Cothey Nelson…………………………………………….0764
018535
MUNGU AKIKUBARIKI
HAKUNA ATAYE KULAANI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni