SIONI THAMANI YA DHAHABU
Ni kweli thamani ya dhahabu inaweza kushuka au kupanda katika soko la dunia lakini haitabadilisha maana ya madini hayo kuitwa dhahabu!
Hata kama mtu haishi sehemu iliyo karibu na migodi, au ajui migodi inapatikana wapi lakini bila shaka ameshaona dhahabu na kusikia japo inawezekana kupitia tv na hata radio kwa namna hiyo anaweza pata fununu kuona kuwa dhahabu ni kitu cha thamani japo inawezekana kuwa ajui kwa uhalisia thamani yake ni kiasi gani na wengine ambao hawajaona dhahabu yenyewe bali wanaweza kuona vitu vilivyotokana na dhahabu mathalani pete viatu makochi na vitu vingine baadhi ya nchi zimekwenda mbali sana hata kutengeneza gari la dhahabu!
Wachache wetu ambao wameweza kujaliwa kuona na hata kushika na wengine hata kuishi kutokana na bidhaa hiyo hivyo utakavyosema sioni thamani ya dhahabu bila shaka hawata kuelewa kwani wengine kupitia dhahabu wameweza kuishi maisha wayatakayo na hata kusafiri nchi ambayo yeye mwenyewe anataka kwenda pasipo kujali gharama yake…..hivyo furaha ya maisha yake kwa kiasi kikubwa bidhaa hii inachangia.
Dhahabu ni aina ya madini yanayopatikana nchi nyingi lakini mojawapo ni Tanzania hasa katika maeneo ya shinyanga, arusha n.k katika dhahabu watu uweza kupata fedha,heshima pindi watu wanapoona umeivaa katika muonekano maridadi na zaidi kuweza kuishi katika maisha wayataka.
Japo ni kweli dhahabu ni bidhaa ambayo inaweza kujibu maswali mengi hasa ya kuichumi na kuzalisha furaha katika moyo wa mtu lakini ni seme ukweli kwamba haiwezi kujibu maswali yote katika maisha ya mwanadamu mathalani afya,mwenza sahihi,furaha ya kudumu na staa katika maisha yako!
Nini maana ya kauli hii sioni thamani ya dhahabu!
Nakubaliana na mawazo ya wengi kuwa dhahabu inathamani kubwa sana lakini kuna wakati unaweza usiione kabisa thamani yake kutoka na sababu mbalimbali zitakazo jitokeza.
Dhahabu kwa maana tajwa ni kitu chochote ambacho unaweza kuona mwanzo kilikuwa na thamani katika maisha yako lakini baadae ukaona thamani yake haipo tena na hapo ndipo inazaliwa kauli hii SIONI THAMANI YA DHAHABU! Hivyo dhahabu inawezekana kuwa gari nzuri, mwenzi, nyumba, kazi, rafiki,cheo au hata watoto.
Kuna wakati unaweza kuona bora uwe peke yako kwakua kila kitu unachokiangalia kinakupa au kinatoa maana tofauti na hile maana unaijua au unayoitaka, kwa hiyo kila unapoona hapo maumivu uzaliwa hapo.
Hichi kipindi watu wote wanaweza wasikuelewe ila wewe binafsi unajielewa kupita kawaida na bila shaka kila tendo unalo lifanya linakuwa limebeba maana yake kwako japo wengine wanaweza wasiielewe Mathalani ndoa yenu ilikuwa na furaha sana lakini mara baada ya kipindi kifupi kupita unaanza kuona shutuma kwa ndugu wa mwenzi wako inawezekana kwa muonekano wako, kukosa watoto na hata kwa maneno yako hakuna zuri wanalolionatoka kwako japo unajitahidi kuonyesha upendo wa dhati kwao.
Bila shaka umeshaona kuona mtu anakila kitu ambacho binadamu anachotakiwa kuwa nacho lakini bado akawa amegubikwa na huzuni isiyo ya kifani na maji adimu kutoka machoni ya kitiririka na wakati mwingine hata mikono kuishiwa nguvu na kulegealegea pasipo kuwa na mwegeo wowote.
Hichi kipindi wakati mwingine yale mambo ambayo ulikuwa unayaona kuwa hayana maana kwako hapo unaweza kuyapa maana kubwa sana kwako ambayo inaweza kuwa mshangao kwa walio wengi kwanini mambo aliyoyakanyagia chini sasa yamekuwa ya maana sana kwako.
Japo ni kweli katika kipindi hiki unaweza kuwatambua walio wa kweli kwako na wasio wakweli kwako ndipo uweza kuona wengi wakiomba likizo kwako mpaka pale utakapokuwa vizuri tena ndipo warejee tena kwako.
Kwa waliona imani kama yangu lazima hapo nione hapo ni kipindi cha kumwelewa Mungu katika nafasi nyingine tena katika kukuweka katika nafasi ambayo yeye mwenyewe ameikusudia.
Huna haja ya kuchoka kwakua Mungu yupo katika kukutengeneza na kukupa upya wa mwelekeo mwingine katika maisha yako na kuona Mungu kuwa ndio mwenza wa yote na endapo utasimama nae bila shaka utakuwa salama.
Lazima uwe na nguvu ya ndani yakuona thamani ya dhahabu iliyopotea inarudi tena katika kiwango cha juu zaidi.
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………….0764 018535
OLD IS GOLD FOREVER