USISUMBUKIE NYONGEZA
Nyongeza ni shukrani ya
muuzaji au ishara ya kujali na
kukukaribisha kwa mara nyingine tena kwani wewe ndio maendeleo ya
biashara yake au shughuli zake!
Nyongeza ni matokeo ya
kununua kitu, na ukubwa au wingi wa nyongeza utegemea ukubwa au wingi wa bidhaa
ulizonunua lakini kwa kiasi kikubwa utegemea maamuzi ya muuzaji, japo watu
wengi wanapofanya manunuzi bila shaka utegemea nyongeza kana kwamba mtu
aliyefanya kazi anadai mshahara wake na pindi anapokosa nyongeza uweza kusema
moyoni mwake kuwa hapa sirudi tena!
Sikatai nyongeza
inaleta raha katika moyo wako na kujua kuwa muuzaji anatambua na kuthamini
mchango wangu katika shughuli yake au biashara yake.
Sikatai kitu kimoja
kinachoweza kuwavutia wateja ni nyongeza na vilevile kitu pekee kinachoweza
kuwapunguza wateja ni kukosa nyongeza, japo kuna maeneo unaenda na bila shaka
unatambua kwa uhakika kuwa hapa hakuna nyongeza
lakini kuna bidhaa nzuri bila shaka itakulazimisha na kukushawishi
kwenda na kupata hiyo bidhaa japo kunawezekana kuwa na punguzo ambalo unaweza
kulifananisha na nyongeza kama ushawishi wa kuzidi kununua bidhaa hapo katika
siku nyingine.
Japo kuwa nyongeza
inaweza kutafsiriwa kama msaada kwa masikini kwani kunatofauti kubwa katika
masikini anavyo lalamika na tajiri anavyolalamika kwani sauti zao ni tofauti na
fikra zao ni tofauti kwani yuko mwenye uhakika atakama asipoongezwa bado
anaweza kushiba vizuri na kutosheleza kiu yake lakini sio wote, maskini wengi
pindi wanapokosa nyongeza na huku wakitegemea nyongeza basi hapo manung’uniko
uweza kuufinika moyo wake.
Mathayo
6: 31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule
nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa
sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki
yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho
itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake
Katika dunia ya sasa
mambo mengi tunayoona dunia inavyoangaika na hivyo hivyo wana wa Mungu wanaangaikia,
kila siku usiku na mchana, mateso yao yanazidi hata wamataifa kwakua hao dunia
inawapatia bali walio wa Mungu wanasumbuka kwakua hawajaijua njia sahihi
yakupata.
Maombi ya mtu anayesema
anamwamini Mungu ndio anaomba mtu asiyeokoka mathalani utakuta mtu mtu anataja
sifa za mwenzi anayetaka kuwa naye na hata kumshawishi Mungu aseme na mwenzi
ambaye yeye anamuona kuwa anafaa.
Viko vigezo ambavyo
kiukweli sio vya kweli kwa mtu kutambua mtu ananipenda kweli mathalani hataweza
niruhusu nilale njaa, chochote nitakachomwambia
atakubali kwakua ananipenda, atajigharimu kwa ajili yangu tu kwa kila
kitu, ataangalia mambo yangu na kuandaa mkakati wa kunisaidia, atahusika na
maisha yangu kwanza, salama itatawala kwangu, nitamsumbua nione kweli
ananipenda kama hataweza basi atakuwa ANIPENDI KWA DHATI, hivyo sitakubali kuwa
mchumba wake.
Hali hii imepelekea kwa
mtu kuwa mchaguzi sana na kushindwa kupata mahali atakapo dondokea patakapo
leta raha ya kudumu katika maisha yake.
Mbali na hilo muonekano
umekuwa ni tatizo kwa watu wengi kutokana jamii kuibua kitu ambacho kwa
uhalisia hakina maana yoyote katika ndoa mathalani six parts, magari, hela za
kutosha, asiwe mbaili,sexy(mwenye mvuto) lakini ukweli wanaujua walio katika
ndoa kama hivi vyote vinamchango katika kuboresha ndoa au la!
Katika haza za kila
siku mathalani mtu anapokuwa amepanga nyumba au chumba basi hapo kutokana na
kero za mmiliki au jirani yake uweza kusema eheMungu nisaidie na mimi nijenge nyumba
yangu na moyo wangu utatulia na kustarehe hayo mawazo kila mtu uweza kuwa nayo
awe ameokoka au ajaokoka anaweza kuzungumza tena kwa machozi.
Unaweza kukuta
mwanafunzi aliyeokoka anatumia njia zisizo halali ilikufauru mtihani wake
mathalani kuandaa dhana ili kuweza kumsaidia katika mtihani ili pindi
anaposhindwa aweze kutumia dhana hiyo kama mkombozi wake.
Jambo hili kwa kiasi
kikubwa limetoa tofauti kati ya mtu anayemwamini Mungu na asiyemwamini Mungu
kwani mwendo wao katika mambo mbalimbali umekuwa sawa tu wala hakuna utofauti
wowote
Ni jambo ambalo ni teso
la moyo wa Mungu kuona lilealilolikusudia limekuwa ni tofauti au kuwa kinyume
kabisa na vile alivyokusudia kwani Mungu anatamani kuona moyo wako unaambatana
na yeye lakini imeambatana na vitu vingine.
Mwanzo
6:6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo
Mungu kuna jambo
analolitaka tulifanye katika kumwamini Mungu ili yeye ajidhihirishe katika
maisha yetu kwani yeye Mungu anapenda kujidhihirisha kupitia sisi kwani ndio fahari
yake kuona sisi tunamwelekeo uliojaa matumaini na uhakika katika njia yake sio
ya ulimwengu huu.
Jifunze kwenda na wingu
la Mungu na sio wingu la dunia japo ni ukweli mwili utaona uko nje ya mwelekeo
uliosahihi lakini ni kuhakikishie kuwa hapo uko SALAMA. Ni kweli watatangulia
lakini mwisho watakuhitaji na kuona wewe ndio mshauri wao mkuu.
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni