Jumanne, 19 Januari 2016

UKIIPOTEZEA KWELI UTUMWA UTAKUTESA!



UKIIPOTEZEA KWELI UTUMWA UTAKUTESA

 Kama binadamu unayeishi katika sayari ya tatu (dunia) yenye mchanganyika wa mambo mengi……..kwa hakika bila shaka utakuwa umewai kusikia MTU akisema maneno haya…. kama ningelijua nisingelikuwa rafiki yake! Ningelijua mapema nisingelikuwa mchumba wake au ningelijua nisingelikubali au ningelijua nisingelikataa au ningelijua nisinge liangalia au ningelijua nisingelitazama au nisengelinyamaza kimya……….bila shaka maswali haya uibuka baada matokeo fualni kutokea katika maisha yako.

 Unaweza usione umuhimu wa kujua noti bandia au feki kwakua bado ujakutwa na mkasa wa kupata noti feki na kisha ikakuweka katika mazingira mgumu sana, hivyo usione haja kwanini nijue noti bandia na feki, na wako watu wanaweza wasione umaana wa kusoma kwakua hawajajua pindi asiposoma nini atapungukiwa au hasara gani au changamoto gani zitamkabili, mbali nao kuna aina ya watu kutokana na nafasi walizonazo mathalani cheo, fedha, na mengine mengi hivyo uweza kujisahau  hivyo kutumia muda wao hawawezi kuona umuhimu wake lakini pindi atakapo pita mahali ambapo ataona yuko tofauti  wa vile alivyofikiria na hali halisindipo atakapoona thamani ya kule alikotoka.

Na ni kawaida wanafunzi wengi wanaweza kukosa swali moja kwa sababu ya  kukosa uelewa au kukariri pasipo kuelewa unakuta mtu amekariri tu na pindi anapoingia kwenye mtihani na kukuta swali linafanana na lile analolijua basi ufurahia na kufanya harakaharaka sana pasipo kuwa makini labda kunamitego ambao mwalimu ameuweka na kujikuta kuwa na matumaini ambayo hayapo na mwisho kujikuta anakosa lakini mwelewa sikuzote huwa hana harakaharaka  kwani anaamini anajua hivyo hakuna mitego itakayo msumbua kwakua afanyi sawa na alivyo kariri bali ufanya sawa na alivyoelewa hivyo kupata kunakuwa ni haki yake.

Mambo mengi yanatokea katika maisha mtu yanaweza kuwa mabaya na mwisho wake ukaathiri maisha ni kutokana watu kutojua ukweli halisi kuhusu hicho kitu au huyo mtu!

Niseme vijana wengi wanapata mimba(wasichana au mwanamke) ni kwasababu ya kukosa uelewa wa kweli kuhusu jambo hilo inawezekana kutokana kutojua kinaga ubaga akajikuta akadumbukia katika hali hiyo kwani kunakipindi unaweza sema siku moja hauwezi kupata mimba inawezekana alikuwa anajua lakini pindi alipoingia katika uwanja wa jambo hilo(field) katika mgongano wa hisia akajikuta akisema kuwa kweli nilisema siku moja siwezi kushika mimba lakini hali hiyo inaweza kutokea tofauti na alivyojipa akili na uhalisia ukajitokeza (kushika mimba).

Na wakati mwingine ukweli kwa tendo la siku moja unaweza usipate mimba lakini huo ukawa mwanzo wa mtindo huo kuendelea siku kwa siku katika akili na uku ukisema tuwe makini katika jambo hili au tutumie kinga ili tutunze hekalu la Mungu kwa kuwa unapokuwa katika mfumo huo unaweza kujipa moyo na kujilinda na hata kujiliwaza katika kila jambo unalolifanya pasipo kujua hapo unaelekea gizani haijarishi utaki au unataka lakini yote yatabaki kama yalivyo.

Niseme kuwa mateso mengi watu wanayopitia ni kwasababu waliitupilia mbali kweli na kujitia giza katika akili zao na mwisho mateso yakawa ndio maisha yao pasipo kujali kuwa walikuwa watu wema kiasi gani au walikuwa chagua la Mungu.

Waefeso 4:18 ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao;
Na ni kweli kila binadamu utamani uhuru sana katika maisha yake kwani katika uhuru kuna kujiamini, kunakujisimamia, kunakujiheshimu na zaidi kunakujipenda  lakini nisipende kukunganya uhuru utokana na kweli unayoiishi kutokano na kuijua uwezi kuwa uhuru zaidi na ulimwengu wako unao unaoujua

Yesu alisema “mataifahamu kweli nayo kweli itawaweka huru” nje ya hapo sina neno zaidi kusema kweli uliyo nayo ndio uhuru ulio nao, kwani utofauti wa wewe na mwingine katika kufanya jambo moja utegemea sana uelewa wenu na ndipo apo nazungumzia kweli.

Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Na ndoma usemekana kwamba ukitaka kumsaidia mtu fungua ufahamu wake uwe na nuru na ndipo atambue yuko wapi na anakwenda wapi? Na ndipo mwendo wake uanze kwenda kwa uhakika pasipo kupapasa.

Katika maamuzi yoyote utakayo yachukua kubwa sana kwako ni kutambua usahihi wa jambo hilo sio lile la kuambiwa kwa upande mmoja bali kila kitu kipe muda wa kutosha katika kuwa imara ili uweze kuimiri vishindo vyake.

Imeandaliwa na;

Cothey  Nelson……………………………………………..0764 018535

UHURU HAUTAFUTWI BALI UNAKUJA BAADA YA KUIJUA KWELI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni